Adungwa sindano sehemu ya haja kubwa kwa kuwa kikojozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adungwa sindano sehemu ya haja kubwa kwa kuwa kikojozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Jun 25, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamtafuta mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Lwiche Kitongoji cha Mazwi katika Manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma ya kumchoma sindano iliyowekwa maji ya moto mtoto mwenye umri wa miaka sita kwenye sehemu yake ya haja kubwa kwa madai kuwa ni kikojozi. Mwanamke huyo aitwaye Severia Mpepo anatuhumiwa kumfanyia unyama huo mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali juzi majira ya saa moja asubuhi. Kitendo hicho kisicho kawaida kilisababisha mtoto huyo ambaye ni wa kiume kupiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa majirani kabla ya kuzimia na kukimbizwa na wasamaria katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya matibabu.

  Kwa mujibu wa majirani wa mtoto huyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema kuwa tukio la kuunguzwa linafuatia mateso mfululizo aliyokuwa akiyapata kutoka kwa mama mlezi wake, Severia ambaye amekuwa akimlea kwa kipindi cha miezi sita tangu kufariki kwa mama mzazi wa mtoto huyo. Majirani hao walisema mtoto huyo aliletwa kwa mlezi huyo na babake mzazi anayefahamika kwa jina la Peter Matalanganya kufuatia ushauri wa rafiki yake ambaye ndiye mume wa Severia aliyemshauri kuwa ampeleke kwake ili apate kumlea baada ya mkewe kufariki dunia.

  “Tunasikia kuwa huyu mtoto aliletwa hapa na babake miezi sita iliyopita baada ya mamake kufariki, lakini kuanzia alipofika huyu mwanamke amekuwa akimtesa sana mara amnyime chakula, mara amchape na juzi ndio kahitimisha kwa kumfanyia huu unyama wa kumwunguza katika sehemu yake ya haja kubwa, kwa kweli huyu mama hafai na ni muuaji mkubwa,“ walisema majirani hao.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Saduni Kabuma alikiri kumpokea mtoto huyo hospitalini hapo na kupatiwa tiba ambapo katika uchunguzi alionekana kuwa ameunguzwa katika sehemu za haja kubwa na maji hayo kiasi cha kumsababishia malengelenge. Dk. Kabuma alisema kuwa taarifa alizopata kutoka kwa ndugu wa karibu waliomfikisha hospitalini hapo zimedai mama mlezi wa mtoto huyo alichukua uamuzi huo wa kinyama kwa kuwa kijana ni kikojozi wa kupindukia.

  Naye Daktari aliyempokea mtoto na kumpatia huduma ya matibabu katika kitengo wagonjwa wa nje, Dk. Revocatus Kasoni alisema kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na kuongeza kuwa bado yupo katika uchunguzi wa kitabibu zaidi. Alipoulizwa na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake kutaka kufahamu undani wa tukio hilo alikiri kutenda unyama huo, lakini alisema hakutenda kwa makusudi bali alikuwa anampatia mtoto huyo tiba ya ugonjwa wa tumbo kwa kumpiga bomba. Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kuwa mama huyo bado hajakamatwa na Jeshi hilo linaendelea kumsaka mama huyo ili sheria ichukue mkono wake iwapo ikibainika kuwa alitenda uovu huo.

  HabariLeo | adhalilishwa kwa kudungwa sindano sehemu ya haja kubwa
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Ukatili huu dhidi ya watoto twatakiwa kuupinga kwa nguvu zote...inashangaza na kuuma pale binadamu anapokuwa na tabia ya kinyama kama hii...
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hii inauma sana,

  Huyu mama anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria haraka sana. Hata hivyo hata baba wa mtoto hawezi kukwepa lawama. Hivi wanaume wa Kitanzania hawawezi kuishi na watoto wao wenyewe hadi wawe na wake au ndugu wa kike? Ni bora na muhimu sana kila mtu alee mtoto wake mwenyewe!
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Maskini malaika wa watu pole sana. huyo mwanamke anafaa hata kunyongwa ni muuaji mkubwa.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Du kwa hiyo dawa ya kikojozi ni sindano ya mk.undu?
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Naunga hoja mkono na natamani sana jeshi la police liwe lingeshamtia mkononi huyu dogo aliyeleta madhara haya wandungu. Mhh! Inasikitisha.
   
 7. Mfatiliaji

  Mfatiliaji Senior Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mh pole mtoto,ni unyama mkubwa usiovumilika katika jamii,mtuhumiwa akamatwe na apewe adhabu kali iwe fundisho na kwa wengine wanaonyanyasa watoto.
   
 8. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole kwa mtoto,huyo mama mkatili achukuliwe hatua kali.Ni kawaida ya baadhi ya watoto kukojoa
   
Loading...