Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,384
41,394
Unajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.

Unajua mapenzi yana nguvu sana, kuna baadhi ya scenarios zinatokea kwa watu hadi unajisemea kwamba "its over between these two" lakini unakuja kuwa surprised after awhile unakuta wako pamoja as if nothing happened.

Nina jamaa yangu ashawahi mkuta mpenz wake amebananishwa uchochoroni na jamaa, ilikuwa usiku tunatoka kuangalia mpira, na kama tungechelewa kidogo tungekuta wanafanya mapenzi. Jamaa alikuwa disappointed sana kiasi kwamba nikajua ndo mwisho wa penzi lao, ila after siku kadhaa naona wako pamoja as if nothing happened. Sikumshangaa jamaa,japo yule Shem wangu Wala simchangamkii kama ilivyokuwa zamani.

Point ya kuandika huu uzi ni kwamba, ikitokea umegombana na mtu ambae uko nae katika serious relationship, tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki, nakusihi hutakiwi kuyaanika mabaya yake Kila sehemu, maana kesho ni fumbo.

Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.

Kuna wale watu ambao kipindi upo kwenye mapito ndio waliokuwa faraja Yako, ndio waliokuwa wanahakikisha hujidhuru, wanahakikisha furaha yako inarudi, so ikitokea wewe umemsamehe, wao wanaweza wasimsamehe. Na kutomsamehe kwao kunatokana na kumbukumbu zao jinsi ulivyokuwa unapitia hali ngumu sababu ya huyo mtu wako. Au jinsi wao walivyokuwa hawafanyi mambo yao kwa uhuru ilimradi kuhakikisha wanakufariji wewe.

Wewe utampa second chance,ila wao hawatakaa wampe hiyo nafasi. Na inawezekana wasimpe tena ule uzito waliokuwa wanampa awali.

That's All (Ni hayo Tu).

Analyse
 
Unajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.
Kabisa ni mbaya sana
 
Faida za kuwa elezea ni nyingi kuliko hasara.

Iwapo wataona haina haja ya kusamehe kutokana na madhara au damages wanazoziona zinazoweza mfika siku zijazo wakati wowote ndugu yao ni bora kutorejea.

Mauaji mengi ya wanandoa hususa wake mara nyingi ziliamza dalili na ishara za wazi lakini zikapuuzwa bila kuamua kukaa mbali mwanamke au bila kushirikisha
Wazazi na ndugu wa damu ili kushauriwa kuondoka kabla ya kumfika mazito.

Akumulikae mchana usiku atakuchoma.
 
Sipo against na kuwaelezea watu, ila naongelea sio Kila mtu anatakiwa kuambiwa Kila kitu kwa uwazi. Hayo mauaji yanatokea ni pale mtu anapoamua kufa na tai shingoni, kwamba anahifadhi stress zake mwenyewe
 
Yeah, unajua kuna muda unahisi baadhi ya ndugu zako au watu wako wa karibu hawana hamasa na mwenzi wako au hawampi uzito, ila hujui sababu. Kuna watu Bado wanakumbukumbu za matukio ya zamani
Hii ni sawa uwe na washkaji zako afu mtu atokee akuzingue then wewe upotezee then wao wajue utasikia '" yaani akuzingue mshikaji wetu wa damu lazima tumtie adabu baba ake na wewe acha kukaa kilokole"
Utakuta wamepiga mtu huko.
 
Mambo ya chumbani kwa wanandoa yanabakia chumbani...

Ukishirikisha tu ndugu, yani mtu wa tatu...
Umekaeibisha vitaa...
Na huwa ipo hivyo. Japo kuna muda unaweza hitaji ushauri wa kimawazo ili kupunguza uzito wa unaokukabili, ila yahitajika kuchagua wa kuongea nao. Wengine yafaa wawe watazamaji tu
 
Hii ni sawa uwe na washkaji zako afu mtu atokee akuzingue then wewe upotezee then wao wajue utasikia '" yaani akuzingue mshikaji wetu wa damu lazima tumtie adabu baba ake na wewe acha kukaa kilokole"
Utakuta wamepiga mtu huko.
Kwa hii scenario Iko tofauti kidogo. Maswala ya mahusiano hata washkaji huwa wanayaangalia kwa mbali
 
Back
Top Bottom