Adui yako Sio Mwislam, Sio Mkristu, Sio kabila lingine: Ni FISADI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adui yako Sio Mwislam, Sio Mkristu, Sio kabila lingine: Ni FISADI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Azimio Jipya, Oct 23, 2010.

 1. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kulingana na Mjadala maarufu alio toa Dr Slaa Jioni ya leo ni wazi kuwa Mgawanyiko mkubwa wa Kijamii kwa Watanzania umesababishwa na UFISADI MKUU ambao Dr aliwahi kuwataja wahusika vinara KUMI na leo Kamuongeza wa KUMI NA MOJA.

  Its a shame wote wliotajwa kushindwa kuchukua hatua ya kujisafisha hadi leo. Wamebaki WANATETEMEKA kwa WOGA MKUU wamechanganyikiwa wanajikusanya kujaribu kujiosha na kufichiana siri... kwa gharama ya Kutugawa Watanzania kwa matabaka yote kuanzia kidini, kisiasa, kikabila, kikanda..nk. tusikubali watanzania, kwani tumekuwa wamoja miaka yote huko nyuma na hatukufarakana.

  Kama tumemeuelewa Dr Slaa, hatuna haja ya kugombana Kidini wala kikabila; Watanzania tujiunge tuwafanyie kweli MAFISADI kumi waliotajwa, Maadui wa Taifa hili sio waislam wala wakristu wala tofauti zetu nyingine. Ni mafisadi.... tupambane nao kwa nguvu moja bila kutengana mpaka watueleze kwanini hawajamchukulia Dr Slaa hatua hadi leo kama walivyokuwa wamedai. Adui yako Si Mkristu, Si Muislam na wala sio Mtu wakabila lingine ... NI FISADI... aliyeshindwa kujisafisha baada ya kutajwa hadharani... Mtanzania wa leo ..Usidanganyike...!

  Tushukuru Mungu kwa kumleta Dr na kutoa ufafanuzi huu muhimu dakika hizi za mwisho...Tuelewe na tuchukue hatua tujenge Uzalendo, Heshima, Matumaini na Umoja wa Kitaifa kwa kutambua Adui Mkuu wa Umoja wetu Ni FISADI.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena hapo.
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Na fisadi ni ccm
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Na sote tuseme................AMEN.

  Mafisadi wasifikiri sisi ni wapumbavu au wajinga ila ni watu wenye akili timamu na uvumilivu wetu wasifikiri ndiyo sababu ya kutuzuga na udini au ukabila ili tusahau dhambi kubwa walizotufanyia............
   
 5. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh, huu ujumbe sijui Dr jana aliutoa au vipi maana mimi sikuwa na namna ya kupata mdaharo. Maana unafaaa uwafikie watanzania wote siyo wanaJF pekee yao.
   
 6. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hilo ni neno na FISADI ni CCM
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna aina ngapi za ufisadi? je kuna ufisadi wenye nafuu?
  [​IMG]
  Fisadi Kiwembe
   
 8. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  fisadi ni ccm, chagua slaa chagua chadema
   
 9. l

  lwangwa Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli amenena sasa dawa ya mafisadi ni kutaifisha mali zao kokotre ziliko kisha tuwapeleke keko hasa rostam azizi lowasa na washirika wake
   
 10. l

  lwangwa Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we subiri jumapili ijayo tumuoneshe ushujaa huyo kaka yako anayefunga safari kwenda kubembe bkwenye bembea huko haiti amewaacha watanzania wanakufa kwa njaa
   
 11. J

  John10 JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kutumia Udini katika kampeni zake inaonyesha kabisa Dr. Slaa ni MDINI.
   
 12. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni kitu gani kinachokufanya useme kuwa Dr ni mdini!??? explain!!
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ruta S`;

  Kustawisha jamii na kufikia kilele cha juu kabisa cha maendeleo si swala la ushabiki wa hisia na fikra!
  Ni uwezo wa Kiufahamu na Kiutu unao tuwezesha kutizama na kuona kinachotakiwa kuonekana na kukifanyia kazi kwa faida ya jamii yote.

  Watanzania inabidi tuone chanzo na msingi wa mgawanyiko wetu na kutambua ni nani sasa hivi tayari anafaidi mgawanyiko huo na kwanini angependa uendelea hata kwa gharama yeyote.

  Tuone ni nani anataabika kwa unyonge na kuvuna maumivu ya kutosha kutokana na mgawanyiko huo.

  Hivi ni huyo mkristu na muislam aliye fukara, mgonjwa na maskini asiyejua mlo wa siku moja ataupata wapi? Au ni huyo Fisadi aliye kiuka misingi ya uongozi bora na kuruhusu uwekezaji mbovu wa mali ya asili ya Taifa na kuifaidi yeye, familia na marafiki zake?

  Hivi wanao faidi mali ya asili ya taifa kifisadi, wametengana kulingana na makabila yao? umewasikia wakigombana kwa udini wao? Umesikia wapi Fisadi wa Kikristu akipipambana na Fisadi wa kiislam, umeona wapi Fisadi waliobobea wakitofautiana katika biashara haramu kwa sababu eti sio wa Kabila moja? au kwa kuwa rangi za ngozi hazilandani?

  Itambulike na kueleweka fika ; Kwa nini iwe sasa baada ya miaka karibu 50 ya Uhuru wa taifa hili swala la ukabila, udini, ukanada nk vinaanza kuonekana kuwa na sauti?

  Jibu ni kuwa Taifa la Tanzania halijawahi kufikia katika uongozi mbovu kama leo. Tanzania haijawahi kuubusu na kuupakata ufisadi kama leo! Uovu wa kuikubali na kuihalalisha rushwa na kuulinda ufisadi uko kileleni.

  Si upuuzi tu bali ujinga na uzuzu kuchukulia jibu rahisi la tatizo hili na kuanza kunyoosheana vidole vya udini na ukabila kwani Fisadi asiye na chembe ya aibu na hekima yoyote hicho ndicho anachotaka Ili kujidumisha katika kuwatumia na kuwatawala wakristu na waislam waliolala na kutawaliwa ufukara, umasikini, usugu wa magonjwa na dhuluma zote na kutokuwa na sauti yeyote juu ya mali na utajiri wa Taifa lao;

  ITABULIKE KUWA UFISADI WAO HAUTIKISWI NA UDINI, HAUYUMBISHWI NA UKABILA, RANGI YA NGOZI AU NYWELE, UKANDA, LUGHA YA KINYWA AU MWILI! WANACHOJALI NI KUFANYA UFISADI.

  TUAMKE; Tutambue kuwa ufisadi ni uovu na wanao utumia na kuwekeza kwenye ufisadi huo hawatenganishwi na udini, ukabila, ukanda, rangi zao, lugha zao nk.. Swali kwanini sisi tunodhulumiwa tunatengwa na kuburuzwa na tunakubaliana kuvunja UMOJA NA MSHIKAMANO WETU?
   
 14. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  eti!!!!!

  Fisadi kiwembe...loh!
   
 15. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  kibunango!Hatudanganyiki!,Hovyooooooooo![/
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Originally Posted by John10
  Kwa kutumia Udini katika kampeni zake inaonyesha kabisa Dr. Slaa ni MDINI.  Fafanua kidogo ili tukuelewe,because your arguement is baseless!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwanachama kamili wa Ufisadi: Lazima asijali dini ya mwanachama mwingine wala kabila lake,! Ila lazima fisadi huyo atumie hali hizohizo kuwatenga na kuwagawanya wale anaowatawala na kuwatumia.

  Kuwa fisadi lazima uwatenge kwenye makundi ya udini na ukabila wale unaowatumia na kuwaaminisha kwenye makundi madogo madogo mengi inavyowezekana. Lakini wale wanaofadi ufisadi kamwe na ni mwiko wao kwa wao kujali na kutilia maanani dini zao na makabila yao.

  Sirahisi kwa fisadi kuwashinda waislam na wakristu walioungana katika kupambana naye kama ilivyokuwa jambo la kweli na hakika kwenye historia ya awali ya taifa la Tanzania.

  Niambie; Kitu kama azimio la arusha lingewezekana vipi kama wakristu na waislamu hawakuwa kitu kimoja ?

  Uhuru, umoja na utulivu wa Taifa ungewezekana vipi kama kabila na kibali lingejitenga?

  Hakika ambaye anafaidi hapa ni Fisadi peke yake! Anapata MAFICHO YA UDHALIMU WAKE!!

  Hakuna heshima yeyote kwa wakristu na waislamu kuacha kuelewana na kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wote waliohusika na EPA, KAGODA nk wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

  Lakini umoja huo wa Kidini, Kikabila, Kimajibo nk ...utakuwa mwiba mkali kwa Mafisadi wanojua fika kuwa wamehusika na dhuluma hiyo. Hivyo watakuwa na kazi moja tu! Kuliko kuumbuka, watajijengea makundi na mitandao imara bila kujali dini zao na makabila yao na hata rangi zao ili kuyumbisha taifa kwa namna itakayowafanya waokoke dhahama ya kukabiliana na ukweli!

  Nani haoni hilo? Nani anabisha? ... Kwa faida ya nani??

  Hatutegemei Watanzania kuingia kwenye mtego wa kijinga na unaodhalilisha utu na ubinaadamu wetu kirahisi rahisi tu! Tunataka mafisadi wawekwe hadharani na mbele ya vyombo vya haki na sheria.
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Watu Kumi tu ndani ya nchi hii wanatuyumbisha sisi kiasi hiki? kwa nini? Narudia tena watu KUMI TU Kati yetu 40m tunawashindwa kuwazibiti?
   
 19. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kama ni kumi tu!

  Chukulia katika kiwango cha juu kabisa watakuwa ni makabila 10 tofauti, dini 10 tofauti, rangi 10 tofauti, majimbo 10 tofauti nk

  Lakini hata sikumoja hawatafarakana kwa tofauti zao.

  Watabaki kuwa 10 kama mafisadi waliokubuhu kwani hiyo ndio silaha yao kuu dhidi ya wanyonge na hohehahe Milioni 40, wanaokufa kwa umasikini wa kupindukia, wanaougua magojwa sugu bila hata asprin, wanaoteseka kuwasomesha watoto wao shule za Kata nk.

  Kama kuna anayewajua; wafanyei utafiti wa kina ni hakika kwa kiasi kikubwa wana dini tofauti lakini kamwe hawatafarakana kidini hata kama watanzania wote watafarakana.

  Kama kuna anayewajua ; Kafanye utafiti utagundua kuwa wala hawajui kabila la kila mmoja wao... ila kinachowekwa mbele ni kuliibia, kulifedhesha na kulidhalilisha Taifa kwa ufujaji wa mali ya asili kwa ajili ya jamii nzima.

  Hao wakuu 10;

  Watakuwa na nguvu kubwa kutawala na kumiliki vyombo vya ulinzi na usalama na kamwe hawatafarakana hata kama makabila na dini zote Tanzania vitafarakana. Watatumia kila njia na hata kuomba misaada kwa mafisadi nje ya Taifa hili kuwawezesha adhama yao!

  Mtanzania bado hujafunguka machao na kuamka toka usingizi mzito na kurejesha mshikamano wa Tiafa lako?

  Bado unafikiri adui yako ni Muislam? Mkristu? Mtu asiyekuwa na rangi ya ngozi inayofanana na yako ? Au asiyekuwa wa kabila lako?..nk!

  Hapana! Huko ni kupotaka na kujisaliti Uwanadamu wako!
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nafikiri unweza kutufafanulia... ikiwezekana kwa ushahidi!
   
Loading...