Adui wa watanzania sio umasikini, ujinga na maradhi bali ni kuridhika haraka

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Miaka nenda rudi tumeimbishwa na wanasiasa kuwa adui mkubwa wa watanzania wengi ni umasikini, ujinga na maradhi Mimi nilichogundua sio kweli tatizo kubwa ni kuridhika haraka.

Mfano tumeridhika na dawa za wazungu ndio maana hatugundui zetu, tumeridhika na elimu ya wazungu ndio maana hatuna yetu , tumeridhika na kakilimo ketu na kakipato ketu na makazi yetu Mungu atupe nini.

Mainchi matajiri watu wake hawaridhiki haraka ndio maana kutwa hugundua na hutaka kwenda mbele zaidi kwenye maeneo yote ya maisha iwe kilimo,biashara,kipato,ufundi,elimu nk.

Akina bakhresa Ni mabilionea sababu hawaridhiki kiwango Chao Cha kutoridhika Kiko juu.

Kiwango Cha kuridhika haraka watanzania wengi ngozi nyeusi kiko juu kuliko wahindi,waarabu na wazungu.
 
Miaka nenda Rudi tumeimbishwa na wanasiasa kuwa adui mkubwa wa watanzania Ni umaskini, ujinga na maradhi Mimi nilichogundua sio kweli tatizo kubwa Ni kuridhika haraka

Mfano tumeridhika na dawa za wazungu ndio maana hatugundui zetu, tumeridhika na elimu ya wazungu ndio maana hatuna yetu , tumeridhika na kakilimo ketu na kakipato ketu na makazi yetu Mungu atupe Nini


Mainchi matajiri watu wake hawaridhiki haraka ndio maana kutwa hugundua na hutaka kwenda mbele zaidi kwenye maeneo yote ya maisha iwe kilimo,biashara,kipato,ufundi,elimi nk.

Akina bakhresa Ni mabilionea sababu hawaridhiki kiwango Chao Cha kutoridhika Kiko juu

Kiwango Cha kuridhika haraka kwa watanzania ngozi nyeusi kikoo juu kuliko wahindi,waarabu na wazungu
Safi sana, kama ulivyo ridhika wewe kwa kulipwa Buku 7 ukajitoa kabisa ufahamu
 
Akili za ccm utasikia tu.

Kutoka huku 7 mpaka 10 huridhiki??

Tupeleke ombi kwa Slowlow
 
Nakuunga mkono kwenye hili. Kuna ukweli. Ni vema tukajitafakari upya.
Yaani hata mitoto iwe ya mswahili awe bosi ofisini , kwenye siasa au dini au au bunge au mahakama inabweteka inaridhika na success ya wazazi walipofikia kazi Yao kula kulala !!! Hata ndugu ana relax anataka kula Cha nduguye aliyefanikiwa !!! Hata awe mtoto wa Reginald Mengi au bilionea mama Rwakatare!!! Watoto wa wenzetu wa akina bakhresa au Dewji hawaridhiki Wana fight kampuni iende juu zaidi.
 
Hasa mkuu mungu kanipa afya nzuri sisumbuliwi na gonjwa lolote,nina kibanda changu na fenicha zote, kazi na mshahara mzuri,wifu mzuri watoto wanasoma na kula vizuri afya tele,Nchi amani tele kwenye account nina tumilioni kadhaa savings kwanini nisiridhike?
 
Yaani hata mitoto iwe ya mswahili awe bosi ofisini , kwenye siasa au dini au au bunge au mahakama inabweteka inaridhika na success ya wazazi walipofikia kazi Yao kula kulala !!! Hata ndugu ana relax anataka kula Cha nduguye aliyefanikiwa !!! Hata awe mtoto wa Reginald Mengi au bilionea mama Rwakatare!!! Watoto wa wenzetu wa akina bakhresa au Dewji hawaridhiki Wana fight kampuni iende juu zaidi.
Nadhan kuna haja ya kubadilisha style ya malezi.
Instead ya kuwa tegemezi. Tuwafundishe kujitegemea wasije tegema wajukuu mbeleni.
 
Biashara za hao ni kuwa wanaifanya ndio maisha yalivyo kiuhalisia
Biashara ni lazima ikuwe na iwe ya muda mrefu na hata kurithishana
Biashara za mswahili akifa na biashara inakufa au ana biashara ndogo na miaka nenda rudi iko palepale kama kiosk
Ndio maana wao biashara target ni kuzitanua aggressively
Anaanza na biashara ndogo akijua itaendelea na kukua na kurithishana hata kama ni miaka 200
Zipo biashara nyingi zinafanya mambo makubwa na kuendelea kuwa za kimataifa kwa malengo mapana tofauti na weusi ambao iko hapohapo
Huo ndio ukweli ambao baadhi hawataelewa kabisa
 
Back
Top Bottom