figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Adui zetu wakubwa barabarani sio Polisi bali ni Madereva wenzetu.
Kusema kweli adui zetu wakubwa barabarani ni madereva wenzetu kuliko hata hao Polisi tunaowaona maadui. Dereva anatumia nguvu nyingi kuchukua tahadhari dhidi ya Polisi kuliko hata dereva mwenzake. Kwa nini Polisi baadhi yetu tunawachukuliaga kama maadui na kimsingi si maadui zetu?
Polisi hata akikusimamisha:
1. Haumizi mguu wako na kukufanya mlemavu.
2. Haondoi uhai wako na kukufanya mfu.
Atakushughulikia kwa taratibu tu au hata kama atachukua chochote bado viungo vyako unabaki navyo na uhai wako unabaki nao. Sasa tuje kwa hawa wenzetu. Kwa nini tunasema maadui ni wenzetu tena tunaowaamimini?
Dereva mwenzio:
1. Hakawii kukuletea gari upande wako akakugonga ukapoteza mwelekeo.
2. Hakawii kuingilia nafasi yako barabarani kwa kuovateki bila umakini.
3. Hakawii kukugonga kwa nyuma kwa kufuata kwa karibu sana.
4. Hakawii kukuuzia tela uhangaike nalo.
5. Hakawii kuyumba na kuangusha mzigo ukaangukia gari lako kutokana na uzembe wa uendeshaji au kufunga mzigo.
6. Hakawii kukubania ili ukutane na kicheche.
7. Akimaliza kutengeneza gari haondoi mawe au miti ya tahadhari aliyoweka.
8. Gari lake limeharibika haweki tahadhari yoyote njiani.
9. Anakupiga na mwanga mkali wa taa na usione kabisaa.
10. Wakiongozana kama ni malori 5 hawaachi nafasi kabisa ya kuingia kati yao pale dereva mwingine anapo ovateki.
11. Ni dereva mwenzio ndiye anayekuchomekea kwa pupa zake barabarani.
Matokeo ya matendo hayo ni kukusababishia ulemavu au kifo. Mwogope dereva mwenzio, Usimwamini sana, jiamini wewe tu, chukua tahadhari dhidi yake.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.