Adui number moja wa Tanzania huyu hapa

Jul 27, 2012
41
28
Tatizo number moja linalotukabili watanzania ktk nchi yetu ni 'WOGA WA KUTHUBUTU". utakuta watu wanatokwa na povu jingi ktk media esp. mitandao ya kijamii na magazeti ktk kulaani au kukemea na kuonyesha msimamo wao ktk jambo flani, lakini wengi wetu tunaishia "kuenjoy" kusoma tuu mawazo yao kisha tunatupa kama story ya udaku. tungeweza kuthubutu kutenda ktk kila tunenalo tungekuwa mbali. utasika mtu flani ajiuzulu, asipojiuzulu hakuna kinachofanyika. Hii ndio imewapa hawa viongozi wetu kiburi cha kuona wao ni wao wengine vinyesi. Kama tungeungana kimatendo si kwa kumbwela I'M SURE Tz ingekuwa nchi moja nzuri but WOGA WA KUTHUBUTU umetufanya tueendelee kuwa maskini na mtaji kwa wengine. tumeshuhudia nchi za wenzetu zilivyofanya mapinduzi kwa kuhakikisha viongozi makanjanja yanatolewa hata kwa migomo ya wananchi but kwa Tz hii itakuwa ndoto za abunuasi.

Conclusion:
Ni heri tukanyamaza kuacha uovu utamalaki kuliko kulia lia kila siku wakati tukijua hata opportunity ikija huwa hatuwezi fanya chochote kujikomboa.So ninaweza sema SHAME ON US KWA KUWA NA WOGA WA KUTHUBUTU.:blah:
 
kwa jina lako linavyoeleza inaelekea kuwa leo utakuwa ulizidisha ile DOZI ya sigara kubwa

Anyway hongera kwa kuthubutu kuanzisha uzi jamii forum
 
Ni kweli nakubaliana na wewe. Utasikia watanzania wanasema "Tunatoa siku saba la sivyo...". Siku saba zinapita inakuwa kama hawakutoa tamko lolote!
 
Hivi mkuu zile siku saba silishaisha au bado? jamaa walisema wataufurusha ubalozi wa Marekani! mpake leo wapi?
 
Tatizo number moja linalotukabili watanzania ktk nchi yetu ni 'WOGA WA KUTHUBUTU". utakuta watu wanatokwa na povu jingi ktk media esp. mitandao ya kijamii na magazeti ktk kulaani au kukemea na kuonyesha msimamo wao ktk jambo flani, lakini wengi wetu tunaishia "kuenjoy" kusoma tuu mawazo yao kisha tunatupa kama story ya udaku. tungeweza kuthubutu kutenda ktk kila tunenalo tungekuwa mbali. utasika mtu flani ajiuzulu, asipojiuzulu hakuna kinachofanyika. Hii ndio imewapa hawa viongozi wetu kiburi cha kuona wao ni wao wengine vinyesi. Kama tungeungana kimatendo si kwa kumbwela I'M SURE Tz ingekuwa nchi moja nzuri but WOGA WA KUTHUBUTU umetufanya tueendelee kuwa maskini na mtaji kwa wengine. tumeshuhudia nchi za wenzetu zilivyofanya mapinduzi kwa kuhakikisha viongozi makanjanja yanatolewa hata kwa migomo ya wananchi but kwa Tz hii itakuwa ndoto za abunuasi.

Conclusion:
Ni heri tukanyamaza kuacha uovu utamalaki kuliko kulia lia kila siku wakati tukijua hata opportunity ikija huwa hatuwezi fanya chochote kujikomboa.So ninaweza sema SHAME ON US KWA KUWA NA WOGA WA KUTHUBUTU.:blah:
Hatuna militias ndiyo tatizo,na hakuna recruiters wala idea hiyo.

Kungekuwa na uwezekano wa kuwa train wapiganaji,basi wa kujitolea ni wengi tu.Kama ni kuuwawa,watu wameshauwawa,lakini hakuna mpango wowote wa uanzishaji wa kikosi cha kupambana,no training camps,no recruiting of the freedom fighters.Be it inside the country or outside.Hilo tu ndo litakata mzizi wa fitna.Kabidhi watu AK47s' halafu ndo useme ni waoga.

Hata huko kulikotokea mapinduzi watu walikuwa na paipu za kupambana.Ni sehemu chache tu ndipo walitegemea nguvu ya umma peke yake.Nadhani Egypt,maybe na Tunisia,lakini kote uko walipata sapoti za mataifa ya nje na ndiyo maana serikali zao ziliogopa kuwauwa.Na zile zilizofanya hivyo,wapinzani walikabidhiwa silaha,ie Libya.
 
Nadhani adui mkuu ni ujinga. Watanzania wengi hawana weledi wa kujua sababu hasa ya matatizo yao, na zaidi, jinsi ya kupata ufumbuzi . Ni wakaao mijini tu ndio kidogo wamefungua macho sana kwa sababu wanaona LIVE jinsi wakuu wanavyotumbua na kuuwa.
Lakini Watanzania walio wengi hawaishi mijini. Kuondoa mfumo mzima, na wala sisemi serikali tu, kwa 'nguvu ya umma' kunahitajia 'Mexican wave' yaani ikianza Dar inapokewa Arusha, Dodoma, Tanga, Morogoro, Mtwara....mijini na vijijini. Hakuna hiyo 'mass awareness' bado. Ah, acha wale mpaka Yesu atakaporudi!
 
376742_4374625292472_701228060_n.jpg
 
Tatizo number moja linalotukabili watanzania ktk nchi yetu ni 'WOGA WA KUTHUBUTU". utakuta watu wanatokwa na povu jingi ktk media esp. mitandao ya kijamii na magazeti ktk kulaani au kukemea na kuonyesha msimamo wao ktk jambo flani, lakini wengi wetu tunaishia "kuenjoy" kusoma tuu mawazo yao kisha tunatupa kama story ya udaku. tungeweza kuthubutu kutenda ktk kila tunenalo tungekuwa mbali. utasika mtu flani ajiuzulu, asipojiuzulu hakuna kinachofanyika. Hii ndio imewapa hawa viongozi wetu kiburi cha kuona wao ni wao wengine vinyesi. Kama tungeungana kimatendo si kwa kumbwela I'M SURE Tz ingekuwa nchi moja nzuri but WOGA WA KUTHUBUTU umetufanya tueendelee kuwa maskini na mtaji kwa wengine. tumeshuhudia nchi za wenzetu zilivyofanya mapinduzi kwa kuhakikisha viongozi makanjanja yanatolewa hata kwa migomo ya wananchi but kwa Tz hii itakuwa ndoto za abunuasi.

Conclusion:
Ni heri tukanyamaza kuacha uovu utamalaki kuliko kulia lia kila siku wakati tukijua hata opportunity ikija huwa hatuwezi fanya chochote kujikomboa.So ninaweza sema SHAME ON US KWA KUWA NA WOGA WA KUTHUBUTU.:blah:

Mkuu ni kweli opportunity zilizokuja zakutufanya tufanye mapinduzi ni epa,karamagi na mikataba ya madini,mgawo mkubwa wa umeme,mgomo wa madaktari,kutekwa kwa ulimboka,mgomo wa walimu.nk.
 
Tatizo nini mkubwa kumeshakuwa na madalaja ya kipato,huu ndio ukweli sikia kaka kunawatu ambao wana mali zao kwahiyo unapo sema swala la mahanda mano anafikilia mali zake kuwa amani ita toweka alafu atashindwa kula mali zake,alafu kuna wenzangu na mimi ambao atunakitu sisi uwa waongeaji na wachangiaji wa kuu sehem mbali kwenye migomo umuoni mtu,sasa kunawale waliochoka kabisa kimaisha wale ndio utawakuta kwenye maandamano mbalimbali,tubadilike jamani without action tutafanywa kama watumwa katika nchi hii.
 
.......
Hata huko kulikotokea mapinduzi watu walikuwa na paipu za kupambana.Ni sehemu chache tu ndipo walitegemea nguvu ya umma peke yake.Nadhani Egypt,maybe na Tunisia,lakini kote uko walipata sapoti za mataifa ya nje na ndiyo maana serikali zao ziliogopa kuwauwa.Na zile zilizofanya hivyo,wapinzani walikabidhiwa silaha,ie Libya......

Ni matumaini yangu kuwa hautushauri tutumie njia ya kupewa silaha na mataifa ya nje kufanya mageuzi kama walivyofanya hao wahuni wa Bengharz-Libya ya Africa.

Kufanya mageuzi kwa namna hiyo sio ufreedom fighting bali ni ufreedom fooling. Ni kujikabidhi mikononi mwa utumwa wa kujitakia.

Mageuzi halisi ya kimaendeleo kuelekea kujikomboa ni yale yanayoondoa dhana zima ya kuwa tegemezi. Lazima utegemezi upigwe vita kwanza ndiyo tutajijengea heshima. mageuzi lazima yaratibiwe na sisi wenyewe. Kama mageuzi hayo yanahitaji silaha ambazo sisi hatuna, na inatulazimu kwenda kununua silahi hizo mataifa ya nje, basi silaha hizo tuzinunue kwa pesa zetu wenyewe katika masoko ya mataifa hayo.

Sio habari ya kupewa silaha halafu unasema asilimia thelathini ya rasilimali za nchi yetu tuna kupawewe uliyetupa silaha, asilimia hamsini tunakupa wewe uliyefanya uratibu n.k. kwa maisha yote ya uhai wa nchi yetu. Huo na sisitiza sio ufreedom fighting bali ni ufreedom fooling
 
Sasa mbona ume ficha ID kama wewe ni kidume???nyie ndio wale hata mtu akijamba mnakimbia eti mabom ya mbagala!!!
 
Wakuu Jmushi1 na Sijali,

You very positive to change. Watz tumeanza juzi kujitegemea kufikiri hata katika mambo ya msingi, kipindi chote rais ndo alikuwa anafikira za nchi. Huwezi tegemea leo Mtz ajue hayo yote kama hakufundishwa kuwa jasiri tangu miaka hiyo.

Wenzetu tangu miaka ya 1950 wanaishi katika hali ya kupingania haki, wamemtoa mkoloni kwa bakoro, wakawatoa marais hata kuwaua pale wanapoharibu.

Sisi tuna miaka 20 zaidi ya kuweza kufanya vitu hivi. Habari zinazowafikia watu wa tz ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi.

Tunahitaji elimu kwa jamii hasa ya kujitambua na kujua haki za msingi.
 
Tatizo nini mkubwa kumeshakuwa na madalaja ya kipato,huu ndio ukweli sikia kaka kunawatu ambao wana mali zao kwahiyo unapo sema swala la mahanda mano anafikilia mali zake kuwa amani ita toweka alafu atashindwa kula mali zake,alafu kuna wenzangu na mimi ambao atunakitu sisi uwa waongeaji na wachangiaji wa kuu sehem mbali kwenye migomo umuoni mtu,sasa kunawale waliochoka kabisa kimaisha wale ndio utawakuta kwenye maandamano mbalimbali,tubadilike jamani without action tutafanywa kama watumwa katika nchi hii.

hapo points kaka
 
Back
Top Bottom