Adui ni KIRUSI, njooni tumkabili sasa!

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,696
3,472
Hatua ya kwanza katika vita yoyote huwa ni kumjua adui yako; nguvu yake na udhaifu wake. Sisi tumemjua ni kirusi kwa jina COVID-19, Sasa kwakuwa ni kirusi basi tushirikishane 'mbinu mbalimbali za kivita' kumkabili kuliko kuilaumu tuuu serikali wakati maisha ni yetu!

Fanya haya kuzuia maambukizi ya vimelea na kuimarisha kinga yako.

1. Ukiamka asubuhi lamba kijiko kimoja kikubwa cha asali mbichi!
Utafiti umebaini kuwa asali inavichocheo vinavyoweza kukukinga dhidi ya vimelea hasa virusi, pia asali imejaa "antioxidants" zinazoondoa kemikali zinazodhoofisha kingamwili(free radicals) hivyo kuongeza kinga ya mwili.

Itapendeza zaidi kama utachanganya hiyo asali kijiko kikubwa na unga wa mdaladini kijiko kidogo maana mdaladini na asali vinafaida sawa, kuongeza kingamwili na kuzuia vimelea vya magonjwa!

Maudhi(Side effects).. Asali inauwezo wa kuingia mfumo wa neva wa kati(CNS) Hivyo huleta Usingizi baada ya kutumia ndio maana napendekeza kijiko kimoja tu ili usisinzie kazini wakati ni zama za kazi tu, Mdalasini ukichanganywa na asali huongeza 'Ashki Majnuni' (hamu ya mapenzi) na kuongeza uzalishaji wa manii. Ni vema kuyajua hayo mapema.

2. Maji ya vuguvugu na limao
Kila siku asubuhi kamulia limao ktk maji ya vuguvugu glasi moja, kunywa.. limao ina vitamini C nyingi inayosaidia kuzuia vimelea vya maradhi hasa virusi na kuondoa kemikali zile ziitwazo free radicals hivyo huongeza kinga ya mwili.

3. Unga wa majani ya mlonge..
Unachota kijiko kikubwa unachanganya kwenye uji kikombe kimoja.. inaongeza sana kinga ya mwili.

4. MAZOEZI YA MWILI NA KUNYWA MAJI KWA WINGI (ni muhimu kwa afya)
Nb. Ukiweza kupata vyote hapo juu tumia kwa kupishanisha tu muda maana ni tiba lishe (no drug interactions) kufanya kimojawapo ni kheri pia.

Karibuni muongeze mbinu, adui ni kirusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom