Bubu Ataka Kusema,
Yupi nafuuu. Anayesaini mikataba mibovu lakini yeye (hatujui kama anakula) hali rushwa, au yule ambaye anasaini mikataba hiyohiyo mibovu, lakini naye ana 'panga' lake? Mobutu namsifu angalau kwenye mikataba alikuwa na yeye anajigemea na kujimegea, tofauti na ilivyo kwa watawala wa nchi fulani ambao wanasaini mikataba ileile sawa na aliyosaini Mobutu, ila wao mgao wao ni sifa tu... ('ukitaka kula nguruwe... wote wanakula 'nguruwe' ila Mobutu anajichagulia walionona).
Mkapa na Kikwete biggest blunder waliyofanya ni mkataba wa EAC. Hayo matatizo mengine inayosemekana wamefanya, mostly I'd attribute it to uwezo wao wa utawala ulifikia kikomo, mafisi mafisadi yakatumia nafasi hiyo, without their (witting) support.
The bottom line is, hao watawala wote walioko Afrika ya Watu Weusi ni Waafrika wenzetu.
Hivi, pride and prejudice aside, kama tungeamua kumleta Bill Clinton, George Bush, Tony Blair, au Ehud Barak, watu ambao wana uzoefu wa kutawala vizuri kwenye nchi zao, kitu gani kibaya ambacho wanaweza kukifanya ambacho Watawala wetu weusi wenzetu hawawezi kukifanya au hawakifanyi? (HINT: Kwa ajili ya 'sifa kwa taifa', tutamchagua ceremonial Mswahili wa kusindikizwa na misafara, na kutembea juu ya zulia jekundu 'kwa niaba yetu')
Wakati wa Nyerere Tanzania ilikuwa inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Kimsingi kila Mtanzania alikuwa anajua mwelekeo wa nchi. Kama alikuwa anakubaliana nayo siasa hiyo, au iwapo ilifanikiwa au la, hili ni suala la mjadala.
Swali la msingi, sasa hivi Tanzania tunafuata siasa gani?
Ujamaa?
Ubepari?
Ukabaila?
Neo-liberalism?
Post neo-liberalism?
Bora liende?
Mradi kunakucha?
"If you don't stand for anything, you'll fall for everything", so they say. Do Tanzania now stand for anything?