Adui namba wani wa Mwafrika ni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adui namba wani wa Mwafrika ni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlenge, Feb 26, 2010.

 1. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  ... Mwafrika mwenyewe!
   
 2. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #2
  Feb 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Ukienda kwenye ofisi yoyote, hasa yenye watu wenye asili mbalimbali, Mswahili mwenzio ndio anakugandamiza badala ya kukusaidia.

  Safari ndefu.
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ujinga, maradhi, umaskini, uroho wa mali, uroho wa madaraka na kukosa roho ya uzalendo ndio maana tunapelekeshwa na wageni ndani ya mipaka yetu hadi tunachekwa na wenzetu.
   
 4. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #4
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mswahili akimiliki mali ya thamani kubwa: Maswali, umepata wapi? umewezaje? mbona mshahara wako mdogo tunaujua.... keleeeele! Mzungu, Mwarabu, Mhindi, Msomali akiwa na mali nyingi, hakuna hata mtu anayeuliza amepataje... hata kama huo 'mshahara mdogo' yeye hana: tumefanya umasikini kuwa ni sehemu ya jadi yetu....

  Jaribu kushika Kamera uwapige picha Waswahilii wenzio uone cha mtema kuni! "Unataka kwenda kutuuza?"

  Lakini akija Mzungu, Waswahili haohao watacheka "Wazungu bwana, kwa kupenda kupiga picha!"
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu adui wa kwanza wa Waafrika ni Viongozi wa nchi mbali mbali za Afrika ambao wengi wameweka mbele maslahi yao binafsi au ya vyama vyao na kusahau maslahi ya nchi zao. Mifano ya Viongozi hao ni kama Mobutu aliyeifilisi nchi yake, Abacha aliyeiba mabilioni ya pesa, Mkapa aliyeiba Kiwira na kusaini mikataba ambayo haina maslahi na Tanzania na pia chini ya uongozi wake kutokea ufisadi wa hali ya juu ikiwemo Meremeta, Mwananchi Gold, Rada, Ndege ya Rais n.k., Kikwete ambaye chini ya uongozi wake ameshindwa kuwachukulia sheria zozote zile mafisadi mbali mbali wakiwemo wale wa Richmond. Na ipo mifano chungu nzima ya Viongozi kama hawa katika nchi nyingi za Afrika.
   
 6. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #6
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Bubu Ataka Kusema,

  Yupi nafuuu. Anayesaini mikataba mibovu lakini yeye (hatujui kama anakula) hali rushwa, au yule ambaye anasaini mikataba hiyohiyo mibovu, lakini naye ana 'panga' lake? Mobutu namsifu angalau kwenye mikataba alikuwa na yeye anajigemea na kujimegea, tofauti na ilivyo kwa watawala wa nchi fulani ambao wanasaini mikataba ileile sawa na aliyosaini Mobutu, ila wao mgao wao ni sifa tu... ('ukitaka kula nguruwe... wote wanakula 'nguruwe' ila Mobutu anajichagulia walionona).

  Mkapa na Kikwete biggest blunder waliyofanya ni mkataba wa EAC. Hayo matatizo mengine inayosemekana wamefanya, mostly I'd attribute it to uwezo wao wa utawala ulifikia kikomo, mafisi mafisadi yakatumia nafasi hiyo, without their (witting) support.

  The bottom line is, hao watawala wote walioko Afrika ya Watu Weusi ni Waafrika wenzetu.

  Hivi, pride and prejudice aside, kama tungeamua kumleta Bill Clinton, George Bush, Tony Blair, au Ehud Barak, watu ambao wana uzoefu wa kutawala vizuri kwenye nchi zao, kitu gani kibaya ambacho wanaweza kukifanya ambacho Watawala wetu weusi wenzetu hawawezi kukifanya au hawakifanyi? (HINT: Kwa ajili ya 'sifa kwa taifa', tutamchagua ceremonial Mswahili wa kusindikizwa na misafara, na kutembea juu ya zulia jekundu 'kwa niaba yetu')
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uongo!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Sidhani kuna anayesaini mikataba mibovu mwenyewe asinufaike. Si ajabu wote hawa ni shareholders wa Barrick na makampuni mengine ya uchimbaji madini yaliyo Tanzania.
   
 9. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,931
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Rushwa.
   
 10. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wenye visa ni watu,kwahio ni sisi waafrika ndio maadui no. wani
   
 11. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,681
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Afrikacans, hawana uzalendo, kila kiongozi mbinafsi, wenye utajiri hawautumii kuwasaidia wanyonge bali kujineemesha. tujifunze kutoka kwa matajiri wa nchi zilizoendelea mfano, MacDonald, IKEA, na wengine hawa utajiri wao umetoa ajira kwa watu wengi lakini sisi na manji wetu ummmmmmmmmmmmmmmmmmm
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  ni mwafrika mwenyewe, huyu anayejiita mzawa idd simba, wakati huo ni waziri wa viwanda na biashara, kuna kampuni moja ya simu, ndo ilikuwa inaingia bongo hii, walifanya kiji meeting flani pale movenpick enzi hizo sheraton hotel. kuna jamaa napiga nae mzigo yeye alikuwa waiter pale miaka hiyo alipewa ahudumie hiyo convoy. anasema waliongea mambo mengi tu na ujumbe toka wizarani. wale wawekezaji walipoulizia kuhusu salary takwimu zikoje kulinganisha na makampuni mengine, mzawa akadakia eti hawa waswahili hawahitaji kulipwa vizuri, wakilipwa pesa nyingi hawafanyi kazi kabisa, jamaa anasema kidogo adondoshe glass wazungu nao wakabaki wameduwaa tu.
   
 13. A

  ASSEY New Member

  #13
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Adui ni Mwafrika mwenyewe
   
 14. S

  Selemani JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 875
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  When the opposition fight against themselves, you have essentially defeated them.
   
 15. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #15
  Feb 28, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Wakati wa Nyerere Tanzania ilikuwa inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Kimsingi kila Mtanzania alikuwa anajua mwelekeo wa nchi. Kama alikuwa anakubaliana nayo siasa hiyo, au iwapo ilifanikiwa au la, hili ni suala la mjadala.

  Swali la msingi, sasa hivi Tanzania tunafuata siasa gani?

  Ujamaa?

  Ubepari?

  Ukabaila?

  Neo-liberalism?

  Post neo-liberalism?

  Bora liende?

  Mradi kunakucha?

  "If you don't stand for anything, you'll fall for everything", so they say. Do Tanzania now stand for anything?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Siyo siri sasa hivi tunafuata Ubepari lakini Viongozi wanalificha hilo hata katiba ya CCM inadai bado tunafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
   
 17. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #17
  Feb 28, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Ubepari is not all bad, same as Ujamaa is not all roses. But we need to choose whichever policy we want to follow.

  Looks like after demonising 'Ubepari' for ages, we cannot now majestically profess it.

  The result is 'Ubemaa' system -- we selectively apply "good" part of 'ubepari' principles to 'Wawekezaji', foreigners and a class of individuals, while applying 'bad' portions of 'Ujamaa' to the greater majority of people.
   
 18. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,306
  Likes Received: 789
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona topic umeeiita "Ubepari ni Unyama" halafu unauliza tunafuata nini tena?

  Sisi ni mabepari namba moja duniani , serikali imeukumbatia ubepari kuliko hata hao waliouanzisha nadhani. Tena ni special brand ya ubepari ambayo bila "wawekezaji" haiiendi!
  Lakini watanzania at heart wengi ni socialists bado, so tunajifoji.

  Nadhani system nzuri iko katikati somwhere btwn socials and capitalism kama wanavyofanya Canada, UK na nchi nyingi za Scandinavia.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Feb 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Tunafuata ufisadism..
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ubepari si unyama bali ni mchakato kufikia malengo fulani. Ukiamini hivyo kuna wanaoamini kuwa usoshalist na ukomunist ni uhayawani. Rejea maandiko yanayohusiana. Lenin katika safari ya kuufikia ukomunist alitoa kauli kwa kusema we are making one step back in order to make two steps forward. Akimaanisha kuwa bila jamii kuwa na viwanda na uzalishaji ambayo ni sehem ya ubepari, hawataweza kufikia vishen yao iliyosema from each according to his produce to each according to his needs. Hapo ina maana ukomunist Ukiyatafakari hayo utaona ubepari ni kipengele muhimu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...