Adui namba moja wa wa wakulima ni hivi vitu vinaitwa vyama vya msingi na vyama vya ushirika

Eng Jay

Member
Sep 11, 2019
17
45
Kilimo ni biashara, kilimo ni kazi, kilimo ni ajira. Huu utaritibu wa uwepo wa vitu vinavyoitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi havimsaidii mkulima bali vina muangamiza. Huu utaratibu wa uwepo wa vyama vya ushirika ulibuniwa na Serikali ya awamu ya kwanza kama njia ya kuimarisha sera ya ujamaa. Ni sera iliyoshindwa na toka enzi hizo hadi leo havijawahi kuwa na manufaa kwa mkulima zaidi ya wizi na ufisadi.

Angalia mazao yote ambayo hayapitii kwenye hivi vyama yanaendelea vizuri. Lakini yale mazao ambao yanasimamiwa na vyama hivi yanadorora siku hadi siku.

Kimsingi hata uwekezaji mkubwa kwenye haya mazao haupo kwa sababu watu hawawe zikuwekeza kwenye mazao haya sababu ya kuogopa urasimu na dana dana.

Wafanya biashara waachwe wanunue mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima, halafu utaona jinsi mazao haya yatakavyo shamiri.

Mh. Magufuli wewe ni mtu wa reforms..tafadhali vunjilia mbali vitu vinaitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi. Acha kilimo iwe kazi huru, biashara huru na ajira huru. Hapo utakuwa umewasidia wakulima
 
Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
2,000
Naunga mkono hoja,ushirika ni kitu cha hovyo Sana.
Wanaofaidika ni viongozi wa ushirika siyo wakulima.
 
Samson Ngomboli

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
750
1,000
Katika vitu vinarudisha nyuma wakulima ni hivi vinajiita vyama vya ushirika,vilikuwa vimekufa vikifa na mabilioni ya wakulima,saizi wamevifufua tena bado ni vigoi goi na visivyo na msaada kwa mkulima kazi yao ni Kula jasho la mkulima bila huruma.😬😪
 
Eng Jay

Member
Sep 11, 2019
17
45
Vyama vya wakulima vibaki kama platform tu za kuzungumzia maswala ya kilimo, kama vilivyo vyama vya wafanyakazi au wafanyabiashara. Mbona mishahara ya wafanyakazi haipiti kwenye vyama vya wafanyakazi?.

Sijui ni nani alibuni huu ujinga. Halafu tunaendelea kuung'ang'ania as if hakuna njia mbadala. Tunafanya jambo lile lile kwa njia ile ile tukitegemea matokeo tofauti.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,709
2,000
Kilimo ni biashara, kilimo ni kazi, kilimo ni ajira. Huu utaritibu wa uwepo wa vitu vinavyoitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi havimsaidii mkulima bali vina muangamiza. Huu utaratibu wa uwepo wa vyama vya ushirika ulibuniwa na Serikali ya awamu ya kwanza kama njia ya kuimarisha sera ya ujamaa. Ni sera iliyoshindwa na toka enzi hizo hadi leo havijawahi kuwa na manufaa kwa mkulima zaidi ya wizi na ufisadi.

Angalia mazao yote ambayo hayapitii kwenye hivi vyama yanaendelea vizuri. Lakini yale mazao ambao yanasimamiwa na vyama hivi yanadorora siku hadi siku.

Kimsingi hata uwekezaji mkubwa kwenye haya mazao haupo kwa sababu watu hawawe zikuwekeza kwenye mazao haya sababu ya kuogopa urasimu na dana dana.

Wafanya biashara waachwe wanunue mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima, halafu utaona jinsi mazao haya yatakavyo shamiri.

Mh. Magufuli wewe ni mtu wa reforms..tafadhali vunjilia mbali vitu vinaitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi. Acha kilimo iwe kazi huru, biashara huru na ajira huru. Hapo utakuwa umewasidia wakulima

Naunga mkono hoja, hivyo vyama ni sehemu ya kuleta urasimu usio na msingi na ni vyama vilivyojaza wanasiasa matapeli. Kila mtu aachwe akauze atakapo na anayetaka kujiunga na hivyo vyama ajiunge kwa mapenzi yake.
 
bayayi

Member
Oct 28, 2018
42
150
Akili ya mtu mweusi haiwazi kuendelea bali inawaza namna yakurudishana nyuma ebu fikiria mfumo wa toka enzi za awamu ya kwanza mpaka leo hatujajua madharake na bado tunautukuza na tunaamini utakomboa wakulima.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
14,905
2,000
Napinga hoja.
Kitu pekee kinachoweza kumfanya mkulima awe walau na nguvu kidogo ya kupambana sokoni na mabepari ni hivyo vyama vya ushirika.

Vyama vya ushirika vinay umuhimu mkubwa sana kwa wakulima sema sera mbovu za ccm ndiyo zinazozorotesha ushirika kwa kuvitumia vyama vya ushirika kama daraja la kusimika mizizi ya ccm kwa wananchi.

Kama unavyojua ccm ilivyojaa laana na mafisadi badala ya kuviinua ndiyo huvitia najisi tu.

Niishie hapa kesho nitajibu kwanini vyama vya ushirika viimarishwe mara dufu na siyo kufutwa kama unavyopendekeza
Kilimo ni biashara, kilimo ni kazi, kilimo ni ajira. Huu utaritibu wa uwepo wa vitu vinavyoitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi havimsaidii mkulima bali vina muangamiza. Huu utaratibu wa uwepo wa vyama vya ushirika ulibuniwa na Serikali ya awamu ya kwanza kama njia ya kuimarisha sera ya ujamaa. Ni sera iliyoshindwa na toka enzi hizo hadi leo havijawahi kuwa na manufaa kwa mkulima zaidi ya wizi na ufisadi.

Angalia mazao yote ambayo hayapitii kwenye hivi vyama yanaendelea vizuri. Lakini yale mazao ambao yanasimamiwa na vyama hivi yanadorora siku hadi siku.

Kimsingi hata uwekezaji mkubwa kwenye haya mazao haupo kwa sababu watu hawawe zikuwekeza kwenye mazao haya sababu ya kuogopa urasimu na dana dana.

Wafanya biashara waachwe wanunue mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima, halafu utaona jinsi mazao haya yatakavyo shamiri.

Mh. Magufuli wewe ni mtu wa reforms..tafadhali vunjilia mbali vitu vinaitwa vyama vya ushirika na vyama vya msingi. Acha kilimo iwe kazi huru, biashara huru na ajira huru. Hapo utakuwa umewasidia wakulima
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom