Adui mkubwa wa CUF na NCCR ni CHADEMA, si CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adui mkubwa wa CUF na NCCR ni CHADEMA, si CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EL+RA=UFISADI, Dec 6, 2010.

 1. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Adui mkubwa wa CUF na NCCR ni CHADEMA, si CCM!:angry:

  Imekaaje hii. Hivi hii ni kwa sababu ya njaa kali, kutokuwa na akili au wivu wa kitoto
  (siblings rivalry?).

  Inakuaje leo hii vyama vya siasa vya CUF na NCCR viione CHADEMA kama adui wake mkuu badala ya chama tawala CCM?

  Taarifa zilio wazi zinaonesha kuwa viongozi wakuu wa CUF akiwemo Mwenyekiti wake Ibrahim Lipumba na aliyekuwa kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, na wengineo wana chuki kali sana na CHADEMA.

  In fwact, CUF iko karibu sana na CCM na wako tayari kupokea maagizo kutoka chama tawala ili kuibomoa CHADEMA.

  Angalia haya mambo:

  1. Lipumba mara kadhaa amekiponda CHADEMA na alikuwa wa kwanza
  kumpa mkono wa pongezi Kikwete wakati amejuwa fika kuwa aliiba
  kura kwenye uchaguzi.

  2. Hamad Rashid alionesha hasira, jazba na chuki binafsi dhidi ya
  CHADEMA kwenye mdahalo wake na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman
  Mbowe. Pengine hii inatokana na yeye kutolewa kwenye ulaji wa kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni baada ya ushindi wa CHADEMA kupata wabunge wengi.

  3. Wabunge wa CUF walikuwa wako tayari kuona mtu wa CCM anakuwa spika wa Bunge badala ya CHADEMA. Hii imetokana na CUF kumpigia kura Anne Makinda kuwa Spika badala ya Mabere Marando wa CHADEMA. CUF walimpigia Makinda licha ya kutoa guarantee kwa maandishi kuwa CHADEMA kuwa watamuunga mkono Marando.

  4. James Mbatia wa NCCR Mageuzi anakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la ubunge Kawe ambapo Halima Mdee wa CHADEMA ameshinda. Lengo ni nini? Uchaguzi urudiwe ili CCM ishinde?

  5. Siku zote CUF na NCCR wamekuwa wanazungumzia haja ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Baada ya kuona CHADEMA imessimama kidete kwenye harakati hizo, eti wao wanakaa pembeni.

  Yaani huwa natamani nishike bakora niwachape hawa wasaliti wote wa demokrasia nchini kama CUF, NCCR, TLP, UDP na wengineo.

  Kwa ufupi, wakati CHADEMA inapambana ili ichukue dola na kuongoza serikali, CUF na NCCR wanapambana kuwa chama kikuu cha upinzani chini ya utawala wa milele wa CCM.

  Je tutafika? Kuna haja kweli ya kuwa na umoja wa vyama vya siasa wakati CUF na NCCR ziko mfukoni mwa mafisadi wa CCM?

  Nadhani jawabu ni kuwa CHADEMA ndiyo chama pekee cha upinzani nchini ambacho hakijanunuliwa na CCM, suluhisho ni kwa chama hiki kiendelee jitahada zake peke yake kisipoteze muda na viongozi njaa wa CUF na NCCR Mageuzi.
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kifupi sijasoma hata contents! Ila una uhakika taito iko sawa?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na adui mkubwa wa CCM ni Chadema -- siyo CUF, NCCR au utumbo mwingine wa vyama.
   
 4. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapa ndiyo inakuja ile dhana ya MY ENEMY's ENEMY IS MY FRIEND. Kwa kuwa adui wa CCM ni CHADEMA na adui wa CUF na NCCR Mageuzi ni CHADEMA, basi CUF na NCCR wameamua kuwa maswahiba wakubwa wa CCM.
   
 5. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa ufupi CUF na CCM ni vyama tawala ... hilo halipingiki. Mzee wa kilaracha alianza kampeni za ubunge kwenye vikao vya CCM, eti aachiwe jimbo. Mbatia nae haonekani kama anatofauti na Mrema. Sasa mpinzani aliebaki wa ukweli ni nani? CHADEMA pekee ...
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  My baby is nearly 2.

  He knows all that.
   
 7. E

  Epifania Senior Member

  #7
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Political immaturity, bado safari ni ndefu sana Tanzania. Ole wa watoto na wajukuu zetu watakaobaki kwenye magofu kwa sababu ya uongozi dhalimu.
  By the way, I like ur name; EL+RA= UFISADI
   
Loading...