Adui mkubwa Afrika ni "ignorant leaders", "just" kujua kusoma na kuandika

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Unaweza kushangaa Afrika ilivyojaliwa rasilimali na hali ya hewa nzuri lakini ni bara linaloongoza kwa kuwa na watu masikini, watu wenye maisha ya dhiki kuliko mabara mengine yote.

Tujiulize tatizo ni nini?

nikirejea msemo wa Julius Malema wa Afrika kusini alisema " Afrika inaongozwa na vipofu wasiojua ni wapi wanakotaka kuipeleka afrika"

ni jambo lisilpingika kuwa viongozi ndio madereva wanaoongoza safari za maendeleo na kama tunataka kupiga hatua za maendeleo tunatakiwa kubaini pa kuanzia kutatua matatizo yetu. Na hapo si pengine bali kuondokana na viongozi "ignorant, wasiojua ni wapi wanatakiwa kuzipeleka nchi zao bali wajue kusoma na kuandika tu"

maendeleo yanaakuja iwapo kodi na mapato mengine ya wananchi yatatumika kwa tija lakini unategemea nini kama kiongozi elimu yake ni kujua kusoma na kuandika tu!

matokeo yake ni kutumia fedha za wananchi kufanya mambo yasiyo na tija.
 
Heading :
leders = leaders
Ndo hivyo mkuu. Viongozi wa kibashite bashite tu ndo wanatakiwa.
 
Imagine raisi anakuambia yeye ni dereva wa lori, hajali ya njiani na watu wanapiga makofi.. Nadhani hata raia wanaoishi katika bara hili tuna matatizo..
 
Hao wanasheria na PhD holders si wameliingiza hii taifa kwenye mikataba mibovu

Iptl
Acacia
10%

Na ufisadi kibao wa EPA ,escrow, Richmond, radar,nk

Case study ni hapa Tanzania tusiende mbali

Tanzania imeharibiwa na wasomi

wasomi,PhD holders nk ndio wameiharibu nchi na ufisadi kila corner ,tusimtafute mchawi

Wachawi ni wasomi wetu na sio wasiojua kusoma wala kuandika tusiwasingizie
 
Waliingia mikataba hiyo ya ovyo baada ya kuona viongozi wakuu ni " vihiyo". Kina Carl Peters n.a. Chief Mangungo wa leo.
 
Adui mwingine uliyemsahau ni baadhi ya Wana JF wasiojua kusoma na kuandika kujidai wao ni Wataalamu na Wabobezi wa Masuala mbalimbali.
 
Hao wanasheria na PhD holders si wameliingiza hii taifa kwenye mikataba mibovu

Iptl
Acacia
10%

Na ufisadi kibao wa EPA ,escrow, Richmond, radar,nk

Case study ni hapa Tanzania tusiende mbali

Tanzania imeharibiwa na wasomi

wasomi,PhD holders nk ndio wameiharibu nchi na ufisadi kila corner ,tusimtafute mchawi

Wachawi ni wasomi wetu na sio wasiojua kusoma wala kuandika tusiwasingizie

mimi bado nadhani wewe huoni tatizo la nchi yetu nini?

usitazame tanzania ina wasomi wangapi bali tazama ni watu gani tunawapa madaraka kuwatumia wasomi hawa.

hakuna kitu kibaya kama kuongozwa na ana ignorant person. kwa msomi huwa anajiamini hivyo hata kushauriwa anashaurika na kusikiliza lakini ana ignorant kwake ushauri huwa anaona kama kafedheheshwa.

kiongozi anaongoza kwa kuwaelekeza wataalamu waende wapi, sasa kwa mbumbumbu wao hawana vision na hivyo anachoambiwa ndicho anakamata.

ni tatizo kubwa sana kuongozwa na na mtu asiyejua chochote, kwake ni kutafuta maneno mazuri tu ya kuongea kwenye jukwaa.

mbumbumbu akiambiwa kiongozi anatakiwa kuwa mstari wa mbele basi yeye abadhani kama ni kilimo aende kwa wakulima ashike jembe alime mbele wananchi wanamfuata nyuma, hizi ni tafsiri za kishenzi tulizoletewa na viongozi mbumbumbu hawa wa kujua kusoma na kandika tu.

kiongozi kuwa mstari wa mbele ni kwa sababu kiongozi ndiye anayetakiwa kuplan ahead ya wananchi wanaokja nyuma wakitekeleza. hawa mbumbumbu mipango hakuna unamkuta eti kijijini ameshika jembe akihamashisha kilimo.

hata uwe na wataalamu chini yake wangapi huyu mbumbu anachowalazimisha wataalamu ni kila mmoja kutumia bajeti ya serikali kuandaa shamba hivyo wataalamu wanapoteza na rasilimali kuandaa mashamba na sio kuandaa pembejeo, kuandaa masoko, kuandaa elimu kwa ile dhana ya kila mdau anaplay role yake na sio wadau wote kugangania kitu kimoja tu kilicho ovious.

unaposema wataalamu ndio wanaharibu sijaelewa ni wakati gani tuliwaondoa hawa mbumbu na tunaweka watu makini wakapanga mipango tukafeli?
 
Back
Top Bottom