Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,241
- Wazee na viongozi wetu wengi wameshindwa kuleta mabadiliko hapa Tanzania na Africa kiujumla hata baada ya kuishi na kusomea Ulaya. Je, vijana tunaorudi sasa hivi tutaweza?
- Bila shaka elimu ni muhimu maishani, lakini elimu inavyoonekana kiujumla ni kama imeshindwa kuleta mabadiliko Africa. Je, hili tatizo linatokana na aina ya elimu watu wanayopata, tabia zetu wenyewe au kuelemewa na mazingira na demands za jamii?
- Je, unafikiri vijana wengi wakirudi kwa mkupuo hapa Tanzania kutokea Ulaya tutaona mabadiliko? Je, mabadiliko haya yatadumu kwa muda gani?
- Naamini kuna "western adopted cultures" kwa vijana zizizofaa Africa. But what are these and where do you draw a line?
--------- Chanzo cha maswali hapo juu kwa kifupi ni ifuatavyo: ---------
Bila shaka viongozi wetu wengi Tanzania na Africa kwa ujumla ni wasomi waliobobea. Na wengi wao walipata kusomea nchi za Ulaya magharibi, mashariki na wengine wengi Marekani.
Viongozi na raia wengi wanaporudi, wanarudi na mitizamo mipya kimaisha, na wengi wao wanarudi na elimu kubwa za madarasa.
Kitu kikubwa ambacho huonekana baada ya mtu kurudi kutoka Ulaya ni cultural interaction yake kwa wale anaowakuta hapa nyumbani. Traditionally, mtu anaporudi kutoka Ulaya anakuwa anaogopeka au kuheshimika kinamna yake. Academically, anakuwa anaogopeka sana tu kama si kuheshimika. Socially, kuna mchanganyiko wa mambo. Anaweza akaogopeka na kupendwa kutokana na tabia yake kiujumla, anaweza akaheshimika na kupendwa, anaweza akaogopeka na kudharaulika au anaweza kudharaulika jumla jumla.
Naomba tujadiliane katika hili. Ahsante.
SteveD.
Samahani ningependa kuandika kwa kirefu, ila muda na kipaji cha kuandika kirefu sina.