"Adolescence" Neno linalotumika kuangamiza jamii ya mwanadamu

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,298
Adolescence ni neno la kimombo ambalo humaanisha umri kati ya utoto na utu uzima. Inakadiliwa miaka kati ya 10 hadi 19.

Umri huu umeitwa majina mengi ikiwemo foolish age kwa maana ya umri wa ujinga.

Kiukweli neno hili ni mtego mkubwa ambao wanadamu wameingizwa bila kujua.

Vijana umri huu wanaamini wanaouhuru wa kufanya mambo ya kiutu uzima bila kuwa na utayari na majukumu ya mtu mzima.

Kiukweli hakuna kitu kama umri wa ujinga.

Kuna mtoto na mtu mzima tu.
Mtoto akoisha barehe na kuwa na uwezo wa kuzaa na kuzalisha sio mtoto tena, wala hayupo kwenye kundi la adolescence bali ni mtu mzima.

Unaposhiriki tendo la ndoa jua utazaa au zalishwa. Unatakiwa ujue kuna majukumu ya kuzaa na kuzalisha.

Unapoamua kuvuta bangi, kuacha shule na kuanza starehe. Jua umefanya maamuzi hayo kama mtu mzima sio adolescent. Kuwa tayari na majukumu ya uamuzi huo.

Jamii ikielewa hivyo tutawasaidia vijana wengi.

Msingi wa hoja yangu.

1: Katika lugha kongwe kama Kiebrania hakuna huo msamiati au kundi hili halitambuliki maana ni kitu kilichochomewa kuchochea ujinga na kukwepa majukumu.

*Kuna watu wakubwa sana duniani walifanya mambo ya maana katika umri wa kundi hili akiwemo

1: Alexander Mkuu. aliyetawala dunia nzima.

2: Yusufu wa kwenye Biblia aliyekuwa waziri mkuu Misri. Enzi hizo Misri ilikuwa kama US.

3: Wanafunzi wa Yesu karibu asilimia 80 walikuwa katika umri huu lakini huwa tunawasoma kama ni watu wazima wakomavu.
4: Shemeji yangu aliniambia juzi huko kwao bariadi ndani kabisa Kabinti kalikomaliza darasa la saba kanaweza kuendesha na kulisha mji au familia yenye watu hata kumi. Atalima, ataandaa unga, ataingia porini kutafuta mboga za majani, atachota maji na mji wote utakula na kushiba hata kwama mzima. Ni shambulizi la kiasikolojia lililotupwa kwa wazazi kuwapa service ya kitoto watu wazima waliobarehe majumbani.

Na wengine wengi.

Sasa taifa liachane na hii sumu ya kuwaona watu wazima ni watoto. Hata kama ni tegemezi wawe tegemezi kwa wazazi au shuleni lakini waambiwe sio watoto na wao wanaweza kufanya mambo makubwa hata kuwa marais wa nchi ikiwa katiba itabadilishwa.

Nimemaliza...

Yangu ni hayo, karibuni kwa maoni na maono
 
Eneo ambalo lilikuwa na ushawishi wakati huo mkuu.

Ni sawa utawale Dar, Mwanza,Dom,arusha,kilimanjaro. Unakuwa umetawala Tanzania.
Hahaha pamoja kaka, nlikua naweka chumvi. Maneno yako ni ya kweli,

Kabla ya kufa kwake, Alisema;

"When you bury my body, don't build any momentum and keep my hands outside so that the world knows that the person who won the whole world had nothing in his hand while dying.”

Tafsiri yake,

"Mkiuzika mwili wangu, msijenge mnara na muweke mikono yangu nje ili dunia ijue kwamba mtu alieishinda dunia nzima, alikufa akiwa hana chochote mikononi".
 
Back
Top Bottom