Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
MAJIBU YA KATIBU MKUU WA ACT WAZALENDO ADO SHAIBU ALIPOULIZWA KUHUSU KAULI YA CHADEMA KUSIMAMISHA WAGOMBEA ZANZIBAR.
Kwenye Mkutano wake na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa ACT Wazalendo baada ya CHADEMA kutangaza mchakato wa wagombea wa Urais Zanzibar.
Ado Shaibu: CHADEMA ni chama cha siasa. Kina haki ya kujiandaa na uchaguzi ikiwemo kuandaa wagombea wa ngazi zote sehemu yoyote ya nchi ikiwemo Zanzibar.
Ado Shaibu: Mara baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA kutangaza kufungua milango ya ushirikiano wa vyama, siku inayofuata nilimwandikia barua kupokea hatua hiyo kwa mikono miwili na kuonesha utayari wa ACT Wazalendo.
Ado Shaibu: Tunahitaji ushirikiano wa vya vyama vya upinzani na wapenda demokrasia wotr ili kuing'oa CCM madarakani 2020 na kuleta mabadiliko kwenye maisha ya wananchi.
Ado Shaibu: CCM haipendi umoja wa vyama vya upinzani. Itafanya kila njia kutugawanya. Sisi ACT Wazalendo tumetamka mara nyingi kuwa tupo tayari kwa umoja na tutasimamia hilo.
Imeandaliwa na:
Janeth Rithe, Naibu Katibu, Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma, ACT Wazalendo.
07 Juni 2020.