Adhana ya swala ya asubuhi kupigwa marufuku Israel

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
1,067
570
e6e2271f137ea20cc3c5db301b2f308a.jpg


Serikali ya Israel imetangaza mpango wa kufanyia marekebisho kanuni ya marufuku dhidi ya matumizi ya vipaza sauti kwa ajili ya adhana misikitini.



Mabadiliko hayo yataruhusu adhana kutolewa kupitia vipaza sauti kati ya saa 7.00-23.00 pekee. Kwa kifupi, adhana ya swala ya asubuhi itaendelea kuzuiwa nchini humo.

Israel iliamua kutangaza mabadiliko hayo baada ya kupingwa na chama cha Kiyahudi cha Yahudot HaTora chenye itikadi kali za kidini.

Waziri wa afya Yaakov Litzman ambaye ni mwanachama wa Yahudot HaTora, alitoa maelezo na kuarifu kupinga marufuku hayo kwa kuhofiwa yanaweza pia kuathiri shughuli zao za kiibada.

Madabiliko hayo pia yanalenga kuathiri Waislamu pekee na kutojumuisha ibada za Kiyahudi nchini humo.

November 20,2016
 
Back
Top Bottom