Adhabu ya viboko ilijenga taifa lenye nidhamu kuanzia mashuleni mpaka majumbani !

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,076
15,921
Nakumbuka kipindi kile cha shule ya msingi tulikuwa na mwalimu anaitwa Mr Kitunga ukiambiwa unaenda kuoga fimbo zake mikojo inakutoka kabla ya kufika kwenye adhabu yenyewe na ukifika shule tayari watu wapo mstarini ni vyema urudi hospitali kwenda kuchukua cheti cha dokta uzuge unaumwa

Hali ile ilijenga nidhamu ya hali ya juu na kutochelewa shule na ndio watu waliitumia kujenga nidhamu na uwajibikaji mpaka makazini

Lakini kilipokuja hiki kizazi cha laktojeni na vyama vingi vya siasa kila kitu kimebadilika, taifa limekuwa na vijana wa hovyo wa kuvaa kata K. Hata ukimtuma mtoto wa jirani anakukatalia bila soni.

Toto halijawahi kupigwa hata kibao akiadhibiwa na mzazi wake basi ni kwa njiti ya chelewa,matokeo yake ndio hawa wanaona Rais John Magufuli kila alifanyalo anawaonea hawawezi kuwajibika wala hawana nidhamu wala uzalendo mwisho wa siku anafikia kuchoma shule moto.

Ni vyema sasa ifikiriwe kurudisha adhabu ya viboko ili watoto wanyooke tuondoe taifa legelege,nidhamu ichukue mkondo wake

Ni hatari siasa ikimeza kila jambo eti leo mwanasiasa anasimama na kutafuta kiki kisa mwanafunzi kaadhibiwa na mwalimu ambaye ni sawa na mlezi wake.
 
1
Kwa kuwa yule jamaa kampongeza mvunja sheria na mavuvuzela mmeamka sasa kufuata upepo kwamba waziri Jafo hana maana tena na hakusoma hizo shule? Kifupi Basi Taifa lina viongozi wa ajabu na hawaaminiki.
Ukweli utabaki kuwa ukweli,nidhamu ilikuwa juu wakati wa adhabu ya viboko.

Kwa hiyo wewe unawapongeza wachoma shule
 
Umefanya nimkumbuke mwal. wangu Mkuu Mr. Hamis aka Macho nusu, alinijengea spirit ya kusoma kabla ya kula na kabla ya kulala, mana mbali na kutumia fimbo zisizokuwa na idadi alitumia mateke na makofi pale anapokuita ubaoni na ukashindwa kufanya hesabu ingawa zilikuwa hadhabu zilizopitiliza ila alinijenga sana sana, pengine asingekuwa yeye hadi leo ningekuwa napambana na jembe la mkono kijijini kwetu uko kwenye mikorosho ambayo wanasiasa wameamua kutafutia kick.
 
Ukiwa na Fikra za kizamani Enzi zile za kutazama Muda kwa kufuata kimvuli cha Jua basi Fimbo utaziona ni Halali kwa Mtoto na utahisi zinaweza kumjenga Mtoto awe na Tabia njema..

Shule Binafsi hawatumiii Fimbo lakini ndio zinazo ongoza kwa kutoa Matokeo mazuri ,endeleeni kuishi kitwana tu.
 
1Ukweli utabaki kuwa ukweli,nidhamu ilikuwa juu wakati wa adhabu ya viboko.

Kwa hiyo wewe unawapongeza wachoma shule
Well said, ile self-discipline ilikuwa ya hali ya juu, ukiambiwa nenda kasome unakwenda kweli kusoma mana usipotii unajua kabisa unaenda kukutana na nini, hata ile reasoning capacity ilikuwa juu kwa wanafunzi huwezi kuta ujinga ujinga pengine tofauti na product hizi zinazozalishwa kipindi hiki.
 
Adhabu yoyote ni lazima izingatie kufunza zaidi.kutoa adhabu jumuishi hasa kwa kosa la moto unaweza kubomomoa badàla ya kujenga.kuna mmoja tu alichoma,moto huchomwa na mtu na haina mshiki wa kosa kama makosa mengine.kuwa na jazba ni mbaya hasa unapokuwa na nia nzuri.kama kweli shule imechomwa na mtoto ni nani huyo ndipo adhabu zifuate kwa kuzingatia maadili.wazazi wa kwanza ni walimu mbona hawapati adhabu.
 
Well said, ile self-discipline ilikuwa ya hali ya juu, ukiambiwa nenda kasome unakwenda kweli kusoma mana usipotii unajua kabisa unaenda kukutana na nini, hata ile reasoning capacity ilikuwa juu kwa wanafunzi huwezi kuta ujinga ujinga pengine tofauti na product hizi zinazozalishwa kipindi hiki.

Mlikuwa mnasoma au kukariri?
Mbona sasa tunaambiwa ufaulu unaongezeka kila mwaka?.
Nyakati zenu kutokana na mazingira ilibidi nitumie muda mwingi kusoma kwani kila kitu kwenu lilikuwa kipya machozi kwenu. Mlikuwa washamba .
Nyakati hizi mpaka mtoto anafika la kwanza kila kitu anajua. Wakati kipindi chenu hata baiskeli tu umeiona Mara ya kwanza kwenye picha kitabuni.
Unataka mtoto wa leo akae tu atumie muda mwingi kukariri kisa na wewe ulifanya hivyo?.
 
wapi mwalimu Justin Pais Mukagugo s/m 1998.

wanaitetew uzungu piteni mbali kabisa. kiboko kilileta nidhamu sana. hadi majumbani, kazini na mitaani tukiheshimiana kwa mwongozo wa viboko.

anayekumbuka enzi za jeshi la jadi wakijiita sungu sungu aje hapa na shuhuda.

mitoto ya sasa hamna kitu kabisa.

madeko toka kuamshwa kakiwa chekechea, shule msingi sekondari. ngoja aoe au aoelewe akutane na mwenzake nusu madeko: ndio wanazaa zezeta kabisa.

rejea michango ya vizazi vya kileo humu majukwaani uone jinsi wanavyoanika matusi na faragha zao bila kinyaa. ona jinsi wadasa wanavyotuvalia kimitego bila kujali wazazi wao wanaona utupu huo.

kiboko kipewe heshima, kirudishwe tu. sitalaumu wema, rhoda na amina wangu wakikung'utwa viboko shuleni pale wanapobainika kukosea. tena akijileta kwangu kujitetea namzimua upya kujazia dozi.

udumu sana mwl. Alice Alfred Msambi ulinijaza 'mboko' za kutosha 1999 mbele ya parade na ukaniagiza nimlete mzazi bila kujali mimi ni kiongozi serikali ya wanafunzi. angalau leo najitambua.
Umefanya nimkumbuke mwal. wangu Mkuu Mr. Hamis aka Macho nusu, alinijengea spirit ya kusoma kabla ya kula na kabla ya kulala, mana mbali na kutumia fimbo zisizokuwa na idadi alitumia mateke na makofi pale anapokuita ubaoni na ukashindwa kufanya hesabu ingawa zilikuwa hadhabu zilizopitiliza ila alinijenga sana sana, pengine asingekuwa yeye hadi leo ningekuwa napambana na jembe la mkono kijijini kwetu uko kwenye mikorosho ambayo wanasiasa wameamua kutafutia kick.
 
wanaopata raha na kuifurahia safari ni abiria. lakini upande wa injini na tairi sukuba zinazikumbana nazo ni siri. kuniaminisha ya private schools iwe mada nyingine kwa mapana yake.
Ukiwa na Fikra za kizamani Enzi zile za kutazama Muda kwa kufuata kimvuli cha Jua basi Fimbo utaziona ni Halali kwa Mtoto na utahisi zinaweza kumjenga Mtoto awe na Tabia njema..

Shule Binafsi hawatumiii Fimbo lakini ndio zinazo ongoza kwa kutoa Matokeo mazuri ,endeleeni kuishi kitwana tu.
 
wapi mwalimu Justin Pais Mukagugo s/m 1998.

wanaitetew uzungu piteni mbali kabisa. kiboko kilileta nidhamu sana. hadi majumbani, kazini na mitaani tukiheshimiana kwa mwongozo wa viboko.

anayekumbuka enzi za jeshi la jadi wakijiita sungu sungu aje hapa na shuhuda.

mitoto ya sasa hamna kitu kabisa.

madeko toka kuamshwa kakiwa chekechea, shule msingi sekondari. ngoja aoe au aoelewe akutane na mwenzake nusu madeko: ndio wanazaa zezeta kabisa.

rejea michango ya vizazi vya kileo humu majukwaani uone jinsi wanavyoanika matusi na faragha zao bila kinyaa. ona jinsi wadasa wanavyotuvalia kimitego bila kujali wazazi wao wanaona utupu huo.

kiboko kipewe heshima, kirudishwe tu. sitalaumu wema, rhoda na amina wangu wakikung'utwa viboko shuleni pale wanapobainika kukosea. tena akijileta kwangu kujitetea namzimua upya kujazia dozi.

udumu sana mwl. Alice Alfred Msambi ulinijaza 'mboko' za kutosha 1999 mbele ya parade na ukaniagiza nimlete mzazi bila kujali mimi ni kiongozi serikali ya wanafunzi. angalau leo najitambua.
Watoto wa kizazi hiki ni watukutu na kutwa nzima ni kuwaza ngono, kubeti, kuvaa kiupumbavu pumbavu tu na kutukana hovyo hovyo kila mahali bila ya kuwa na staha.

Bakora ziheshimiwe na zidumishwe milele.
 
1Ukweli utabaki kuwa ukweli,nidhamu ilikuwa juu wakati wa adhabu ya viboko.

Kwa hiyo wewe unawapongeza wachoma shule
NAdhani itabidi tuwe tunaulizana UMRI wa watu humu; nakubaliana na wewe, viboko virudishwe shuleni, hi habari ya kuwalea watoto kwa kiboko cha chelewa sio; zamani watu wazima wenye umri kama wa baba yako alikua anaweza kukuadhibu, Jafo yupo sahihi na Chalamila nae yupo sahihi, JAfo alizungumza kwa maana ya sharia ya leo ilivyo wakati Chalamila alifanya vile kwasababu ya Utazania wake. Viboko virudishwe shuleni, full stop
 
Back
Top Bottom