Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Makata kudai ambulance kuwepo uwanjani ni suala la kikanuni na Ambulance haikuwepo uwanjani bila kujali kuwa ilikwenda wapi kufanya nini. Ambulance ni gari maalumu lenye miundombinu inayoweza kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye afya mbaya wakati anakimbizwa kuwahi matibabu kamili ya hospitali.

Sio kila Prado inaweza ku-replace uwepo na umuhimu wa ambulance.

Kama kanuni inataja Ambulance na Ambulance haikuwepo basi kumfungia kocha kwa miaka 5 na kumpa pointi 3 mpinzani ambae hakuleta Ambulance uwanjani sio sawa.

Kama kanuni inasema Ambulance isipokuwepo uwanjani baada ya 15 minutes kupita ofisa anaahirisha mechi lakini yeye hakufanya hivyo, mechi hii sio sawa. Tayari kosa la kukosekana kwa ambulance limetendeka lakini, badala yake ofisa akapiga ramli kuwa Ambulance itarudi ilikokwenda, hivyo mechi iendelee kuchezwa nayo sio sawa, maana mchezaji angeweza kuumia uwanjani hata dakika ya 2 TU baada ya mchezo kuanza wakati Ambulance haijarudi ilikokwenda.

Kumuadhibu Makata kwa kutumia kanuni ya dk 30 badala ya ile ya dk 15 ni sawa na polisi kusubiri mhalifu atende kosa la pili ili amkamate.

Haki ingekuwa kuwaambia Namungo walete Ambulance on time bila kisingizio chochote maana tarehe na muda wa mechi ulifahamika mapema na uhaba na matumizi ya ambulance Yao wanaufahamu wao sio Mbwana na mbeya Kwanza.

Mwaka mmoja ungetosha badala ya miaka 5.
 
Timu za viongozi ndivyo zinavyokuwa. Kiongozi akimaliza muda wake timu inateremka daraja na hatimae kujifia.
Kanuni haisemi Prado, inataka ambulance ambayo ndani yake Kuna vifaa tiba, tiba na watoa tiba, je ndani ya Prado hilo kulikuwa na vitu hivyo? Mbona Simba na Yanga ziiligomea mechi na Simba na Yanga lakini hakuna aliyefungiwa hata mmoja?
 
Mbeya kwanza wameonewa kwa hili swala mechi ya Simba na Yanga ilivunjika hakuna mtu alifungiwa wala kuzawadiwa points hii TFF no dhaifu sana
TFF inatia kinyaa, kwa Simba, Yanga, Namungo na Azam inafanya tofauti kabisa. Hebu ona TFF haikufungua mdomo kuionya Simba walipoingia na vitochi kumulika wachezaji wenzao usoni, haikuonya Simba kuwasha moto kwenye uwanja wa Orlando, haichunguzi kwa kina kwanini timu kwenye ligi zinakataa kuingia vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mechi dhidi ya Simba.
 
Ila hii adhabu imejaa uonevu mwingi sana! Yaani Wilaya mzima ina gari moja tu ka wagonjwa! Mara kabla ya mchezo kuanza, kulitokea dharura!! Sasa hii inahusiana vipi na mchezo!

Mara ililetwa prado kwa ajili ya tahadhari! Sasa prado ni ambulence! TFF na Bodi ya Ligi ni zaidi ya takataka. Halafu uzembe wa kwenu, mnakuja kumwafungia watu miaka 5! Uonevu mtupu.
 
Wanaokaa kupanga hizi adhabu zakijinga hawana akili timamu.huwezi kumfungia mtu miaka 5 kwamakosa yakipuuzi yaliyochangiwa na mazingira ya kukosa umakini.Hao watoa adhabu wenyewe wanamapungufu mengi sana sasa inakuaje umfungie mtu miaka mingi ivyo.Kwa akili za namna hii tusitegemee soka letu kuendelea.Kwasababu kumfungia mtu miaka hiyo humkomoi kwasababu ataenda kufanya mishe zake zingine lakini je vip kuhusu weledi wakitaaluma aliokua nao,tunakubali taaluma ya mtu ambayo ingeweza kuinufaisha nchi ikae dormant for good five years kwa makosa ambayo yangeweza kutolewa adhabu ya kawaida na maisha yakaendelea.Mambo mengine yanasikitisha sana.
 
Kuna kasoro kubwa kwenye uendeshaji Ligi za TFF, ambazo huwa hazionge hata na wanaojifanya wachambuzi wa michezo hapa nchini . Baadhi yao ni : 1. Timu kupewa ushindi wa mezani. Ni aibu kwa Ligi yoyote inayojitambua kuwa na kanuni inayoruhusu timu kupata pointi bila ya kucheza mechi, kwa sababu yoyote iwayo. Huko ni kusababisha timu kupanga matokeo kwa kutoshiriki mchezo husika, jambo linalowezekana kwa timu iliyokwishajihakikishia kubaki msimu unaofuata inapokutana na timu inayopigania nafasi. Lakini ni aibu pia kwa Ligi makini kwamba pointi tatu za timu zinatolewa kwa kura. Zinaamuliwa kwa kura kwa sababu hatima ya yote, Kamati inayojadili mchezo huo itabidi isikilize maoni ya Wajumbe wake na ikibidi itaishia kuamua kwa kura. Hiyo ni Ligi au Uchaguzi wa Mshindi? Lakini hata Wajumbe wote wanapoamua kwa kauli moja, kuna uhakika gani iwapo maoni ya Wajumbe hao yanatokana na uchambuzi sahihi wa hoja na siyo utashi na uhusiano wa Mjumbe husika na timu husika? Si Siri kwamba TFF ya sasa ina viongozi wengi walio washabiki na hata wanachama wa Simba. Kadhalika Kamati wanazoziteua. Na nani asiyejua ukaribu wa Simba na Namungo? Wadau wasio upande watashawishika vipi kwamba hilo halikuchangia maamuzi hayo? 2. Hukumu za kuua uhai wa soka. Kiongozi wa timu anapofungiwa kwa miaka 5 au zaidi, ni kwa faida ya nani? Hata kwenye makosa ya jinai, hukumu huangalia pia iwapo mshtakiwa ni mkosa mzoefu ama la. Lakini huangalia pia iwapo aliingia hatiani kwa makusudi au kulikuwa na sababu za msingi zilizomfanya akosee. Kocha, kiongozI, mchezaji, anapofungiwa hivyo, mchango wake kwa soka letu utapatikana wapi? Hivi, mathalan, mke anayepika chakula sicho alichoamrishwa na mume wake, adhabu yake ni kurejeshwa kwao kwa mwaka mzima? Hukumu hiyo inaangalia makuzi ya watoto wa familia hiyo? 3. Kuchagua sheria za kusimamia na timu za kuziadhibu. Mojawapo ya makosa makubwa katika soka ni kusajili mchezaji aliye bado kwenye mkataba na timu nyengine. Ni kubwa kuliko hata la timu kugomea mchezo kwa kutokuwapo gari la wagonjwa. Kwa hivyo adhabu yake kwa mkosefu inapaswa kuwa kubwa zaidi ya hao waliofungiwa miaka mitano na kupokwa pointi. Kwenye wenye vyama makini vya soka na bodi adilifu za Ligi, adhabu ya kosa hilo ni timu husika kufungiwa kusajili kwa misimu kadhaa. Bodi ya Ligi, Kamati ya saa 72 na TFF zilikuwa wapi mchezaji wa Kagera Sugar aliposajiliwa na timu kubwa wakati akiwa bado na mkataba? Inawezekana hoja ikawa kwamba timu husika hatimaye zilikubaliana kuyamaliza. Lakini hiyo ndiyo sababu ya kosa kubwa kama hilo kufumbiwa macho? Basi hata onyo kwa wahusika? Au adhabu japo ‘ya kimagumashI’ kwa mchezaji husika ili kuwa katazo kwa wengine? Hiyo timu kubwa ingefanyiwa hivyo ingeridhika? Iliridhika Hassan Kesi aliposajiliwa Yanga mwishoni mwa msimu lakini kabla mkataba wake na hiyo timu nyengine haujaisha? TFF walikaa kimya kama ilivyokaa kwa swala la Kagera Sugar? 4. Kusahau ushuhuda wa umma. Tofauti na kabla ya Ligi kuoneshwa mubashara, makosa mengi yanapofanyika hivi sasa huwa yanashuhudiwa mubashara na watazamaji viwanjani na walioko kwenye TV zao. Linapofanyika kosa lisilohi taji tafsiri ya kisheria kama vitendo visivyo vya kiungwana baina ya mchezaji na mchezaji, hakuhitajiki Ripoti ya mwamuzi ama kamisaa kujua iwapo kosa limefanyika ama la. Ajabu ni kwa wahusika wa kutoa ama kusamehe adhabu kusahau hilo, wakaishia kuzingatia tu ripoti za waliochezesha na kusimamia mechi husika. Nani asiyejua ukweli wa marefa na makamisaa kuwa ni mawakala wa timu wazipendazo, na wakipata fursa huziasidia hata kupitia mechi zisizohusika a na timu zao hizo moja kwa moja? Mdau gani wa soka asiyejua kuwepo kadi za michango za manjanao kuelekea mechi za timu kubwa? Iweje mamlaka za kusimamia Ligi wasilijue hilo na wakabariki kila kilichomo kwenye Ripoti za wasimamizi wa michezo husika? Nani hakuona kwamba mwamuzi wa kati hakuwapo wakati kocha wa Yanga akiongea na waamuzi wasaidizi na makamisaa baada ya mechi ya FA dhidi ya Geita Gold? Nani hakuona msaidizi mmojawapo akienda kwa mwamuzi wa kati na kumnon’goneza jambo? Nani hakuona kuwa baada ya kunon’gonezwa hivyo, mwamuzi wa kati alienda kumpa kadi nyekundu kocha wa Yanga. Kamati iliyomwadhibu kocha huyo kwa kuwatolea lugha changu waamuzi, haikuliona hilo? Ilipata wapi uhakika kwamba mwalimu huyo alitoa lugha chaf.u? Kwani siku hizi waamuzi wa Ligi ya NBC wanawasilisha Ripoti zao kwa mikanda ya audio badala ya maandishi? Ikizingatiwa kwamba mechi 3 ambazo mwalimu huyo alifungiwa zinajumuisha ya watani wa jadi, kuna ugumu gani kwa asiye na upande kuamini kwamba adhabu ile ililengwa mahsusi kumziwia asihudumu kwenye mechi hiyo ya watani? Ufupi wa maelezo hayo marefu ingawa ni mifano michache tu kati ya mingi ni kwamba TFF, Bodi ya Ligi na Kamati ya saa 72 zinapaswa kwanza kuadhibiwa kwa kufanya kosa kubwa kupita yote mpirani: KUPANGA MATOKEO.
 
Kitendo cha Mbwana makata kukataa kuingiza timu uwanjani sikiungi mkono kwa sababu ligi yetu bado ina madhaifu mengi sana kwa upande wa rasilimali na miundombinu

Hakuna timu wa chama cha mpira au mchezo wowote chenye ambulance yake....... HAKIPO
Panapo kuwa na mechi inabidi waende kwenye hospitali kuomba ambulance na ikitokea lina kazi inakua shughuli kulipata
Zaidi ya chini ya asilimia 30 ya game za NPL zinachezwa bila ambulance

Kama kweli timu haitaki kuingiza timu uwanjani basi haiwezi kukosa kigezo cha kikanuni kutokuingiza timu kama alivyo fanya Makata kwasababu ya udhaifu wa rasilimali na miundombinu

Kuna kanuni nyingi mmno hazitekelezeki au ngumu kuzitekeleza zote isipokua ni BUSARA tu za zinatumika na Makata angeachwa pengine tunge kuja kushuhudia matukio zaidi huku watu wamelipa viingilio muda wao na gharama za maandalizi
mengine ikiwemo tv right

Siungi mkono aina ya adhabu imekua KALI sana
Miaka mitano ni KUKOMOA na sio kuonya na kufundisha
 
Ndiyo ikosekane ambulance??
Basi bora tusiwe na ligi. Usipende kutetea mambo ya kijinga.
 
Kama kanuni inataja ambulance na ambulance haikuwepo basi kumfungia Kocha kwa miaka 5 na kumpa point 3 mhalifu ambae hakuleta ambulance uwanjani sio sawa.
Sio jukumu la timu kutoa maamuzi kama kanuni imekiukwa, ni jukumu la TFF. Mbeya Kwanza wangeweza kucheza under protest, na pengine wangeweza kunufaika kwa kupitia kanuni hiyo, lakini wao wakaamua kutoa hukumu kwa kutocheza kabisa, jambo ambalo sio jukumu lao
 
Makata kudai ambulance kuwepo uwanjani ni swala la kikanuni na ambulance haikuwepo uwanjani bila kujali kuwa ilikwenda wapi kufanya nini. Ambulance ni gari maalumu lenye miundombinu inayoweza kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye afya mbaya wakati anakimbizwa kuwahi matibabu kamili ya hospital.

Sio kila prado inaweza ku replace uwepo na umuhimu wa ambulance.

Kama kanuni inataja ambulance na ambulance haikuwepo basi kumfungia Kocha kwa miaka 5 na kumpa point 3 mhalifu ambae hakuleta ambulance uwanjani sio sawa.

Kama kanuni inasema ambulance isipokuwepo uwanjani baada ya 15 minutes kupita ofisa anaahilisha mechi lakini yeye hakuahilisha mechi hii sio sawa. Tayari kosa la kukosekana kwa ambulance kwa dk 15 limetendeka lakini mechi haikuahilishwa, badala yake ofisa akapiga ramli kuwa ambulance itarudi ilikokwenda hivyo mechi iendelee kuchezwa nayo sio sawa, maana mchezaji angeweza kuuamia uwanjani hata dk 2 TU baada ya mchezo kuanza wakati ambulance haijarudi ilikokwenda.

Kumuadhibu Makata kwa kutumia kanuni ya dk 30 badala ya Ile ya dk 15 ni sawa na polisi kusubiri mhalifu atende kosa la pili ili amkamate.

Haki ingekuwa kuwaambia namungo walete ambulance on time bila kisingizio chochote maana tarehe na muda wa mechi ulifahamika mapema na uhaba na matumizi ya ambulance Yao wanaufahamu wao sio Mbwana na mbeya Kwanza.

Mwaka mmoja ungetosha badala ya miaka 5
Exactly..hii Nchi ina vitu vya kipumbavu sana yaani mtu anafikiri Ambulance ni sawa na Prado...
Huu ni upuuzi uliopitiliza...
Huyu Karia ni mtu wa hovyo sana...
Haya ni mambo ya ajabu sana...Elimu ya bongo sijui ina nini aisee...

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kitendo cha Mbwana makata kukataa kuingiza timu uwanjani sikiungi mkono kwa sababu ligi yetu bado ina madhaifu mengi sana kwa upande wa rasilimali na miundombinu

Hakuna timu wa chama cha mpira au mchezo wowote chenye ambulance yake....... HAKIPO
Panapo kuwa na mechi inabidi waende kwenye hospitali kuomba ambulance na ikitokea lina kazi inakua shughuli kulipata
Zaidi ya chini ya asilimia 30 ya game za NPL zinachezwa bila ambulance

Kama kweli timu haitaki kuingiza timu uwanjani basi haiwezi kukosa kigezo cha kikanuni kutokuingiza timu kama alivyo fanya Makata kwasababu ya udhaifu wa rasilimali na miundombinu

Kuna kanuni nyingi mmno hazitekelezeki au ngumu kuzitekeleza zote isipokua ni BUSARA tu za zinatumika na Makata angeachwa pengine tunge kuja kushuhudia matukio zaidi huku watu wamelipa viingilio muda wao na gharama za maandalizi
mengine ikiwemo tv right

Siungi mkono aina ya adhabu imekua KALI sana
Miaka mitano ni KUKOMOA na sio kuonya na kufundisha
Mkuu unaelewa umuhimu wa ambyulensi lakini??
Yaani ni Bora hata kamisaa wa mchezo asiwepo ila ambyulensi iwepo.

Acheni kutetea ujinga. MbK wameonewa
 
Wanaokaa kupanga hizi adhabu zakijinga hawana akili timamu.huwezi kumfungia mtu miaka 5 kwamakosa yakipuuzi yaliyochangiwa na mazingira ya kukosa umakini.Hao watoa adhabu wenyewe wanamapungufu mengi sana sasa inakuaje umfungie mtu miaka mingi ivyo.Kwa akili za namna hii tusitegemee soka letu kuendelea.Kwasababu kumfungia mtu miaka hiyo humkomoi kwasababu ataenda kufanya mishe zake zingine lakini je vip kuhusu weledi wakitaaluma aliokua nao,tunakubali taaluma ya mtu ambayo ingeweza kuinufaisha nchi ikae dormant for good five years kwa makosa ambayo yangeweza kutolewa adhabu ya kawaida na maisha yakaendelea.Mambo mengine yanasikitisha sana.
Gari ilikuja kabla ya dakika 30 wakakataa kuingiza timu uwanjani ili wapate mbeleko ya point za bure. Na hiyo adhabu waliopewa ni ndogo ilibidi wafungiwe maisha kabisa.
 
Wanaokaa kupanga hizi adhabu zakijinga hawana akili timamu.huwezi kumfungia mtu miaka 5 kwamakosa yakipuuzi yaliyochangiwa na mazingira ya kukosa umakini.Hao watoa adhabu wenyewe wanamapungufu mengi sana sasa inakuaje umfungie mtu miaka mingi ivyo.Kwa akili za namna hii tusitegemee soka letu kuendelea.Kwasababu kumfungia mtu miaka hiyo humkomoi kwasababu ataenda kufanya mishe zake zingine lakini je vip kuhusu weledi wakitaaluma aliokua nao,tunakubali taaluma ya mtu ambayo ingeweza kuinufaisha nchi ikae dormant for good five years kwa makosa ambayo yangeweza kutolewa adhabu ya kawaida na maisha yakaendelea.Mambo mengine yanasikitisha sana.
Huyu ni kocha mzawa, adhabu hii hailingani na namna kosa lilivyosababishwa na kutendeka, hii ni mara yake ya kwanza kufanya "kosa" kama hili. Hii ina maana kuwa hii sio tabia yake wala tabia ya Mbeya kwanza, kwanini uiadhibu timu nzima kwa kosa la kusababishiwa. Adhabu hii ingekuwa sawa kwa timu za Simba na Yanga maana zenyewe zina mazoea ya kufanya makosa ya aina hii bila kujali.

Unamfungia kocha mzawa na kuruhusu makocha wa kigeni (wa Simba na Yanga) watende makosa ya aina hiyohiyo, ni ujinga mtupu.

Mchawi kwenye kosa hili ni uhaba wa ambulance huko Lindi na uzembe wa waliopaswa kuhakikisha ambulance ipo available full time uwanjani kwaajili ya wachezaji na watazamaji wa mpira. Hii ni hatari sana kudai kuna ambulance uwanjani ambayo inategemewa kutumiwa na hospital na wadau wengine kwa wakati huohuo mchezo ukiendelea. Ambulance kama hii ni kama vile haikuwepo, maana hata kama ingekuwepo wakati wa kuanza mchezo lakini kuna ushahidi wa wazi kuwa ingeweza kuondoka uwanjani wakati wowote kuwahi dharura nyingine wakati mchezo ukiendelea. Hii ingekuwa shida kama mchezaji angeumia vibaya na ambulance haipo kiwanjani.

Kifupi TFF angalieni upya kanuni na adhabu zenu hizi, hii haikuwa mechi ya kombe la mbuzi mitaani, hatuwezi kuweka rehani maisha ya wachezaji na wanamichezo wetu kwa assumptions tu.
 
Back
Top Bottom