Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Nakiri kuchelewa kuleta hoja hii hapa. Lakini, mniwie radhi na kunisoma ninachokileta hapa kwa mjadala. Kimsingi, Bunge linaoongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Sheria na hasa kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la mwaka 2013.
Kanuni za Bunge ndizo hasa zinazoratibu shughuli na mwenendo mzima wa Bunge kuanzia uongozi; Kamati za Bunge; vikao na kadhalika. Kila jambo linalofanyika Bungeni huratibiwa na Kanuni za Bunge. Kanuni ndiyo nyenzo muhimu kwa kila Mbunge.
Nimejipa muda wa kuzisoma Kanuni husika (nitaziambatanisha hapa) ili nione uhalali wa adhabu aliyopewa Mbunge wa Kibamba John John Mnyika ya kutohudhuria vikao vya Bunge vya juma zima. Ni adhabu iliyotamkwa na Spika Job Ndugai wakati Mnyika akitolewa nje ya Bunge.
Katika Kanuni za Bunge, sikuona mahali popote ambapo Spika au Kiti cha Spika kwa ujumla kinapewa mamlaka ya kumfanya Mbunge asihudhurie, yaani kumsimamisha, kuhudhuria vikao vya Bunge. Nimeikosa Kanuni au Fasili fulani inayompa mamlaka hayo.
Kisheria na kikanuni, suala la Mnyika lilipaswa kupelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguzwa, kujadiliwa na mapendekezo kutolewa. Kumsimamisha vikao bila ya kumsikiliza ni kinyume na kanuni za haki za msingi za kusikilizwa kabla ya kuadhibiwa. Ilitosha kumtoa nje ya Bunge ili kulinda utulivu na amani Bungeni.
Katika kukosekana kwa Kanuni au Fasili inayompa madaraka Spika kumsimamisha Mbunge kuhudhuria vikao bila kusikilizwa au kujadiliwa na Kamati ya Maadili, adhabu ya Spika Ndugai ni halali? Au ndiyo batili tangu mwanzo (void ab initio)?