Adhabu ya kutetea wananchi ndani ya bunge la jmt kwa cdm ni kubwa mno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adhabu ya kutetea wananchi ndani ya bunge la jmt kwa cdm ni kubwa mno

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkwawa, Jul 29, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Wabunge wa CDM ndani ya Bunge la JMT inayotolewa kila kukicha ama na Spika, wenyeviti na waendesha bunge ni kubwa mno na inakera wananchi wote. Tunategemea wabunge watetee wananchi na wapiga kura wao kwa nguvu zao zote. Spika wa bunge akiongoza wenyeviti wake ndani ya maelekezo ya Magamba wamekuwa wakikiuka sheria za wabunge hasa wale wa upinzani hususani CDM.

  Hofu ya kuogopa hoja za CDM inawapagaza wana CCM hawa na kubakia kuwa na jazba na kutumia nguvu. Jazba hii na matumizi ya nguvu haya yalithibitishwa na waziri kivuli wa mambo ya ndani kwenye hotuba yake. Alisema serikali haina huruma kwa wananchi wake wala haiwathamini, inawauwa, inawapiga mabomu, inawabambikia kesi, inawafunga. Na kuonyesha ukweli wa hotuba ya Lema, bunge nalo linawanyanyasa wananchi, linawadhalilisha na kuwatukana kwa kuwatesa na kuwabughi wawakilishi wao bila kosa.

  Leo imekuwa kero kwa kiongozi yeyeote wa bunge akisikia sauti za wabunge wa CDM. Tukio la kuwatoa akina Wenje, Lema, Msigwa, Lissu nk linaonyesha jinsi bunge lisivyokubali upinzani ndani ya bunge la JMT.

  Ninawapa moyo wabunge wa Upinzani hasa wale walioko mstari wa mbele kumtetea mtanzania, wasikate tamaa, wasiogope, wasivunjike moyo. Watanzania wanaelewa na wanaona. Adhabu itakuwa kwenye sanduku la kura. Vipigo, aibu, fedheha mnayopata itazaa matunda tena mia mara mia mara mia maraelfu.

  Ni mimi
  Chief Mkwawa wa Kalenga.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  inasikitisha eti jeshi la polisi linapeleka FFU kupambana na wanafunzi wa shule ya msingi wanaoandamana wakitaka mfumo wa barabara urekebishwe kwa sababu wenzao wamegongwa, wanawakamata watoto na kuwaingiza kwenye makarandinga. still yet Lukuvi anaona kuwa ndiyo utekelezaji wa utawala bora....gademu!!
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hata wazee wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki walinyukwa mabomu wakidai haki zao.
  Hakuna kujali KIKONGWE wala KICHANGA.
  Nchi IMELAANIWA inahitaji maombi.
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Wabunge wanaowapigania wananchi mjengoni wanaonekana shubiri kwa wakubwa.
   
Loading...