Adhabu ya kumfukuza mtoto nyumabani baada ya kufanya kosa. Je, Ni sahihi au sio sahihi?

Jiggy El Jefe

Senior Member
Aug 10, 2017
143
170
Adhabu ya kumfukuza mtoto nyumbani baada ya kufanya makosa, unadhani inamjenga au inambomoa? Toa maoni
 
Umfukuze nyumbani aende wapi?Na huko atapataje uwezo wa kutofanya makosa makubwa zaidi? Au atakosaje kuweka maisha yake hatarini?
 
Minshafukuza watoto watatu ... Afu kuna mmoja namliatimming tu anletee ukilaza namfukuza akaungane na wenzake mitaani.
 
Jiggy El JefeKOSASpost: 24131915 said:
Adhabu ya kumfukuza mtoto nyumbani baada ya kufanya makosa, unadhani inamjenga au inambomoa? Toa maoni
SIO SAHIHI NA PIA NI KOSA LA JINAI.
 
Kulea kunahitaji uvumilivu mkubwa, busara na hekima. Hakuna siku uliwaudhi wazazi wako? He wangekufukuza Leo ungekuwa na uwezo wa kupata huyo mtoto. Watoto wanakanywa hawafukuzwi una mziria nani ?
 
Sio sahihi hata kidogo.mfano kavunja kikombe cha chai au grass. Hivi ukimfukuza akaenda kubakwa au kulawitiwa huko nje.
Thamani ake ni ndogo sana than kikombe alichokivunja?
Aisee wazazi tuombe Mungu. Nitakuwa naomba Kila siku Niwe mama Mwema kwa wanangu.
 
50% /50% ila kama hujawahi kula esp wale vijana wanaopitia "fulish age" huwezi kuyajua haya. Ila malezi yataka moto sana kama una roho nyepesi unaweza Fanya jambo mamii inayokuzunguka ikabaki na butwaa.
 
Kuna mtu wangu wa karibu kijana wake akiwa 14-16 alihangaika nae sana. Dogo kukutwa na bangi boarding ilikuwa kama kawa. Alifukuzwa shule kama tatu hivi za aboarding.

Jamaa alikomaa nae tu, kila siku anampa maneno mwanangu hakuna career ya kuvuta bangi duniani. Dogo alipofika form VI alichange kabisa.

Sasa hivi ana life yake imenyooka vizuri. Mtoto akinyea mkono haukatwi.
 
Hivi mnaongelea mtoto wa umri gani? Mjue mtu wa miaka 40 ni mtoto kwa mzazi wake? Je, huyo akifanya ya ajabu hafukuziki nyumbani?
 
sio sawa kwani huwa chanzo cha kuongezeka kwa vibaka, malaya na watoto wa mtaani.
 
Naongea nikiwa muhanga wa kufukuzwa nyumbani na walezi wangu ikiwa ni mwaka 1979 nilifukuzwa na baba yangu mkubwa na matusi juu niende kwa baba yangu ili hali alishatangulia mbele za haki nilihangaika sana kimaisha niliuza kuni nichoma mkaa nilivuta kokoro nilichunga mifugo ya watu nilisota sana pamoja na hayo sikuweza kuharibika kiakili hatimaye mwanga niliuona wale wale walionitimua wakaanza tena kunivuta wabaya wangu wakajifanya kuja karibu yangu kumbe wanafiki tu mpaka leo hii nina bifu na hao watu walinitesa wakijua wananikomoa kumbe walikuwa wananipa akili za kuijua dunia na watu wake ahimidiwe aliye juu ngoja niishie hapa machozi yananitoka
 
!
!
Sio sahihi.... Tunazaa ili tuwasaidie watoto wetu wawe responsible citizens. Unamfukuza aende wapi?
Kaku shida, au? Mwanangu nakomaa nae
 
Back
Top Bottom