Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
The Bold nadhani hii habari au story umeikopi na au kuitafsiri kutoka kwenye vyanzo vya habari vyenye mrengo wa Kishia.
Nasema hivi kwa sababu japokuwa sikubaliani sana na utwala wa Kifalme wa Saudia lakini pia nafahamu vizuri kadhia y Al Nimr na nafahamu sana propaganda za jamaa wa Kishia hasa serikali ya Iran dhidi ya Utawala wa Kifalme wa Saudia.
Inshort sisi waislam Sunni pamoja na kutokukubliana katika baadhi ya mambo,lakini Shia huwa na chuki zaidi na hutumia juhudi kubwa kufanya propaganda dhidi ya mataifa yenye Sunni wengi.
Tahadhari yangu kwako bwana The Bold sijui wewe imani yako lakini unatakiwa kuwa makini sana kwenye issue sensitive kama hizi manake unaweza kufanya kazi ya watu fulani bila kutambua.
Si ndio ata mimi nilitaka kushangaa,huyo mchinjaji napajua mpaka kwake pale Keko Machungwa alafu leo atokezee Saudia tena akiwa mchinjaji wakati hapa Dar ni muuza Supu pale Keko Veta?
 
Nlipata kazi saudi arabia. Nlikataa kwenda ingawa mjomba wangu alitaka sana niende ishi huko. Ni nchi yenye ukatili. Bahat nzuri yeye ni mwarabu mswahili hivi.mimi ni mwafrika ingawa nina weupe ila naonekana waz tu ni mwafrika.

Huwa anasimulia mikasa mingi sana ya kikatili kwa watu wa huko hasa kwa wageni.ingawa anasema pia good people wapo.ila anasema ni wakatili sana na hawaelew yaani hawatak kureason wana jazba sana.

Kuna baadhi ya waarabu anasema afadhari hasa misri huko anasema si kubaya sana kwa maeneo kadhaa. Otherwise ni kama waarabu wengi wana ukatili wa asili flan hivi. Na wengine wanajifichia kwenye dini ili kutimiza ukatil wao.

Nmesisimkwa sana kusikia mtu anachinja binadamu mwenzie na anaishi kama kawaida. Mungu aliamua makusudi aghairishe hukumu hizi za kikatili. Anayetubu atubu asiyetaka atengwe na binadamu wengine wema.afungwe.but kuchinjana tena hadharani? No comment.
Sijui kwanini ila nimejikuta nimefurahi tu kwa kuwa ulikataa kwenda..

Kuna baadhi ya nchi hutakiwi kukanyaga hata mguu..

Alafu takwimu zinakwambia karibia 50% ya wanaowachinja sio raia wao...
 
Ivi ni makosa ya aina gani SHARIA inahukumu kuchinja mkosaji ?

Ili tunaotarajia kwenda Saudia tujihadhali nayo.
 
Nlipata kazi saudi arabia. Nlikataa kwenda ingawa mjomba wangu alitaka sana niende ishi huko. Ni nchi yenye ukatili. Bahat nzuri yeye ni mwarabu mswahili hivi.mimi ni mwafrika ingawa nina weupe ila naonekana waz tu ni mwafrika.

Huwa anasimulia mikasa mingi sana ya kikatili kwa watu wa huko hasa kwa wageni.ingawa anasema pia good people wapo.ila anasema ni wakatili sana na hawaelew yaani hawatak kureason wana jazba sana.

Kuna baadhi ya waarabu anasema afadhari hasa misri huko anasema si kubaya sana kwa maeneo kadhaa. Otherwise ni kama waarabu wengi wana ukatili wa asili flan hivi. Na wengine wanajifichia kwenye dini ili kutimiza ukatil wao.

Nmesisimkwa sana kusikia mtu anachinja binadamu mwenzie na anaishi kama kawaida. Mungu aliamua makusudi aghairishe hukumu hizi za kikatili. Anayetubu atubu asiyetaka atengwe na binadamu wengine wema.afungwe.but kuchinjana tena hadharani? No comment.
Umenifurahisha hapo uliposema mungu alighairisha hizo hukumu

Inamaana mwanzoni alipoziweka hakujua consequences hapo baadae?
Au hukujui what will happen siku za baadae kwamba kuna watu watazitumia vibaya hizo hukumu

Neno la Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote huwa halibadiliki
 
Kuchinja watu

Hata kama ni adhabu, kitendo cha kuchinja watu hadhalani sio jambo jema hata kidogo.

Nchi nyingi wanapo nyonga watu hufanya kwa kificho wasiohusika wasione

Nakumbuka kitendo cha Sadam Hussein kunyongwa na kuonesha mubashara kwenye TV, kulilalamikiwa sana na mashirika ya kutetea haki za binadamu

Ivi unapochinja watu mbele ya watoto unawafundisha nini, kuwa wawe makatili, waone jambo hilo ni la kawaida tu, waweze kujaribu katika michezo yao, waweze kuwasimulia wenzao wasioona jambo hilo

Huyo mchinjaji mwenyewe ni katili.
Inaaminika nchi yetu yaani watawala wetu wanaogopa hata kuidhinisha adhabu ya kuwanyonga watu waliohukumiwa adhabu hiyo.

Inasemekana aliyenyongwa ni mmoja tu aliyemuua kwa kumpiga risasi Mkuu wa mkoa aliyejulikana kama Dr. Kreluu. Mkulima aliyeitwa Mwamwindi

Ona jinsi baadhi ya Serikali zinavyoogopa kunyonga watu.
Sasa Nchi inachinja wakosaji hadharani tena kwa uwingi (mass behadings) ni ukatili usiotakiwa kushabikiwa.

Halafu kuna tendo la mtu kuhukumiwa kifo kwa makosa,
au kwa kushindwa kujitetea au kwa kusingiziwa au kwa visa vya chuki binafsi
Kama atakaa muda fulani anapata fulsa ya kukata rufaa na kuweza kushinda rufaa yake hivyo kukwepa kifo

Kama mtu anahukumiwa, halafu adhabu ya kumyonga kufanyika harakaharaka basi wako watuhumiwa wengi walio chinjwa kimakosa, hivyo kuuawa kwa kuonewa, au jambo hilo linafanyika kwa hila.

Nadhani mashirika ya kutetea haki za binadamu ambayo yanapinga adhabu hiyo yamekata tamaa kukemea jambo hilo kwani yanapuuzwa na mamlaka ya nchi hiyo

Poleni wananchi wa Saudi Arabia,
mimi siendi Saudi Arabia naogopa naweza nikasingiziwa kosa au nikafananishwa na mkosaji nikawa BEHADED

Chao.
Dunia imebadilika hii Mkuu kuna watu wanatumia madaraka yao vibaya
 
Mkuu The Bold, hii imenisikitisha mno. Hasa ikitiliwa maanani watu kutoka nchi masikini wanavyodhulumiwa huko saudia. Mkuu nitag kwenye mabandiko yako.
 
sheikh napenda kuishi....why nikachinjwe kama mbuzi? mpaka leo huwa ananambia njoo utembelee nchi takatifu....namwambia ....inshallah ntakuja sheikh....
Sijui kwanini ila nimejikuta nimefurahi tu kwa kuwa ulikataa kwenda..

Kuna baadhi ya nchi hutakiwi kukanyaga hata mguu..

Alafu takwimu zinakwambia karibia 50% ya wanaowachinja sio raia wao...
 
ugumu wa mioyo sheikh...hapo mwanzo kulikuwa na adhabu kali sabab watu waliishi chin ya sharia sheikh, abadan muhari ulikuwa juu sana. lakin majira ya mbele tuliletewa neema...allahamdullilah twaish kwa neema. soma vitabu sheikh upate ilimu.

Umenifurahisha hapo uliposema mungu alighairisha hizo hukumu

Inamaana mwanzoni alipoziweka hakujua consequences hapo baadae?
Au hukujui what will happen siku za baadae kwamba kuna watu watazitumia vibaya hizo hukumu

Neno la Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote huwa halibadiliki
 
Na ndio maana kunakuwa na discipline ya hali ya juu kabisa,hakuna ukimwi,wizi,na mambo ya ajabu sana,hukumu hizo zinawatia watu khofur sana na kufuata sheria,ningependelea na kwetu zije alau tuwe na nidhamu.
Wewe nenda kwa waarabu ukajifunze na kufwata hiyo sharia. Kwanza wabaguzi hawapendi weusi. Kwahiyo, watakata kuume ili husichukue tena wanawake zao.
 
hapo ka chinja mwaraabu basi ni tatizo ila ange chinjaa USA wala aina tabu, kwa tarifa yenu nchi zenye ni dhamu ya hali ya ju ni saudia hakuna rape kule, USA kila dakika unambiwa ana bakwa mwanamke Mungu kaleta hizi adhabu so wacha itekelezwe i support kabisa hi hali. hapo chinji mtu kaiba andazi au kuku, hapo ni makosa makubwa, the death penalty has been part of human society for millennia, understood to be the ultimate punishment for the most serious crimes sio uislamu au mwarabu izo issue tokea hata enzi za noah watu wanachinjaaa,In the simplest form, the Bible condemns murder and calls for the death of the murderer. The one who intentionally takes life by murder forfeits the right to his own life. ndo maana inchi hio hakuna ushenzi wakijinga kama madawa ya kulevya, pombe hadharani, kubaka, kutembea na wake za watu au waume za watu, ila angalia inchi ambazo zina jifanya haki za binadamu uone zilivyo shamiri ushenzi wahali ya juu eti usagaji, ushoga, transgender etc...
 
Mkuu ni ajabu sana hii hali. Ila tu napenda niulize hii ni sheria ya kiislamu au ya serikali na kama ni uislamu basi mimi nitakuwa wa kwanza kuhamia dhehebu jingine maana inatisha mkuu.
Iwe mwisho kuquote uzi mrefu namna hii

Unatupa tabu tunaotumia simu
 
Sasa Bosi

kama Saudi Arabia hakuna, Rape, Ushoga,Usagaji, Wizi, Ugoni,
Hao wanaoendelea kuchinjwa wanatenda hayo makosa wakiwa nje ya Saudia ?
Ujue mwanadamu anapoishi ni lazima anafanya makosa, ndiyo maana Mungu ameruhusu toba.
Na kila jamii inatunga adhabu mbalimbali ili kuwaogofya wakosaji kutenda kosa flani.
Jambo linalojadiliwa ni ukubwa wa adhabu dhidi ya kisa husika,
Ndo maana Nchi nyingi zinatoa adhabu ya kifo kwa mtuhumiwa aliyefanya mauaji kwa makusudi, kwa kukusudia.

Sasa ndugu kama hata makosa ya kawaida ya kufumaniwa, kuzini, kumsema kiongozi kwa kumkosoa tu, kuiba pete ya dhahabu nk, hukumu yake iwe kuchinjwa hadharani ?
Tunaambiwa adhabu hizo kali zinawapata haswa wageni na wananchi wa daraja la chini na wanaoonewa kwa chuki za kisiasa na visazi
Matajiri na viongozi wa Saudia wao hawaguswi na ahabu hizo kwani wanauwezo wa kujificha na kujilinda

mfano
Bwana Yesu Kristo alivyopelekewa mwanamke mzinzi ili apigwe mawe hadi kufa. Wauaji hao walikimbia baada ya kuambiwa asiyewahi kutenda kosa hilo awe wa kwanza kumpiga mawe na kumwua binti huyo.
Binti huyo aliletwa peke yake ivi alijizini mwenyewe ?
Mwanaume aliye zini naye alikuwa mtu maarufu, kiongozi, mtu tajiri, ndio maana aliachwa asiuawe.
Hata huko Marekani majimbo mengine hayauwi walioua kwa makusudi.
Huwezi kuzuia makosa kwa kuchinja watu.
njia nzuri ya kuzuia uhalifu ni kuielimisha jamii iweze kumudu maisha, iweze kustarabika, iweze kujitegemea kimaisha, iweze kuzijua haki zake na kuzidai nk
Pia Serikari inatakiwa kutimiza majukumu yake ya, kutoa huduma za jamii kwa kiwango cha kuridhisha.
Kama Elimu, Afya, Ulinzi, Haki,
Demokrasia nk.
Adhabu ya kuua aliyeua kwa makusudi bado wanaopigania haki za binadamu wanapinga ulipaji huu wa kisasi.

Uchinjaji watu hadharani ni udhalimu.
Hauna nafasi katika nchi zilizostarabika kama Nchi yetu nzuri.
 
Ngoja abakwe mwanao au ndugu yakoo afanyiwe ndivyo si vyo ndo utaona faida ya kuchinjwa, inchi ambzao zina practise sharia uwa aziangali wewe ni nani au mtoto wa nani sheria ni msimeno, kama kweli watu wanafanya hivyo basi mbele ya mungu wana tabu isio na mfano, kukubali punishement ya Mungu wako basi ndo toba enyewe, umezini na ili umethibitika kua umezinni kuna takiwa kuwe na mashaidi wanne yani umeona mke wako analiwa mzigo ukaite jirani yako, ndugu na mtu mwingine yoyote hakitimia wanne na wakaona live kweli mkeo ana pakuliwa ndo ina apply pale sharia sio kukurupuka kuna mengi mpaka mtu anapatikana na hatia. usione watu wana chinjwa ukaonoa wanaonewa, mwisho wasiku man must die piga ue kufa kupo.
 
Mimi

Siwezi kumchinja aliyembaka mwanangu au ndugu yangu

Mungu amenifundisha nisamehe saba mara sabini bila kujali aina ya kosa

Mungu ameniagiza NISIUE hata nitendewe kosa la namna gani.

Mungu ameniahidi kuwa ni yeye peke yake ndiye anayelipa kisasi

Ndo maana nampenda sana Mungu wangu huyo,
bila yeye ningesha chinja watu kama kumi hivi waliowahi kunikosea makosa makubwa mno.

Laki niliwasamehe, huwezi amini mmoja wao ndiye anayenisaidia sana kwa sasa.

Amekuwa rafiki yangu mkubwa na siyo mhalifu tena, ametubu na Mungu amemsamehe.

Kama wewe hujawahi kutenda dhambi hebu uwe wa kwanza kumrushia jiwe huyo unaye mwona ni mtenda zambi, mkosaji

Rusha jiwe tuone
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom