Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Oct 12, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Juzi Jumapili ilikuwa siku ya kupinga adhafu ya kifo duniani.

  Nimesoma andishi hili la Prof. Chris Peter Maina wa UDSM, nikagundua kuwa licha ya Tanzania kuwa na adhabu ya kifo, Zanzibar adhabu hiyo haijawahi kutekelezwa hata mara moja tangu baada ya Mapinduzi yale matukufu ya Januari, 1964.

  Huku bara, Nyerere alisaini hati 3 za adhabu ya kifo, Mwinyi alisaini hati 85 ila Mkapa na Kikwete hawajasaini hata hati moja!

  Hii imenishawishi kuuliza tena, hivi kweli kwa Tanzania ya leo, bado tunaihitaji hii adhabu ya kifo, ambayo utekelezwaji wake kwa Tanzania ni very barbaric, kunyongwa mpaka kufa!.

  Lengo la hukumu nyingi ni punitive na penitentiary, yaani kutoa adhabu na kufundisha, sasa mtu aliyeuwa, ukimhukumu kufa ndio unakuwa umemuadhibu vipi zaidi ya kumpotezea uhai wake, na kwa upande wa mafunzo, unakuwa umempa funzo gani ili ajirekebishe?.

  Public execution ni adhabu ya kidhalimu iliyotumiwa kwa lengo la kutisha na kuogofya wengine wasifanye kosa kama hilo.

  Marekani bado inatoa adhabu ya kifo, kasi ya vitendo vya mauaji iko juu kuliko nchi nyingine yoyote duniani, hivyo ni uthibitisho kuwa adhabu ya kifo haipunguzi makosa ya mauaji.

  Uingereza imeifuta adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji vimeshuka kwa kiasi kikubwa.

  Kwa nchi za Afrika, Namibia imeifuta adhabu ya kifo na vitendo vya mauaji vimeshuka sana, lakini Afrika Kusini ambayo imeifuta adhabu hii ya kifo lakini vitendo vya mauaji bado viko juu maradufu.

  Jee sisi Tanzania, tusimame wapi?, tuifute au tuendelee kuilea huku mamia wakihukumiwa bila kujua hatma yao ni lini hivyo wanaishi kwa kihoro huko magerezani. Kwa nini tusiifute tukajua moja?.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ni uwazi kwamba sheria zetu zinathamini sana haki ya kuishi, na wala hairuhusu kuuana kama wanyama. Nafsi ya mwanaadamu ni thamani Anayoijua ni Mwenyezi Mungu tu pekee na wala hakuna mwengine anayeweza kuileta thamani hii. Ndivyo kwa utoaji wake uhai, yabidi kanuni thaabit zifuatwe. Hivyo, Sheria inatoa adhabu ya kifo kama vile ilivyo kwa Katiba na Sheria ya Jinai. Haki ya kuishi yaweza kutenguliwa kwa kuuliwa ikiwa atapatikana na hatia ya kuua.

  Tuelewe kwamba huko Magharibi wanajidai mno kutetea kuondoshwa adhabu ya kifo kwa sababu hao wauaji ni waathirika wa jamii iliyojaa rushwa, matatizo ya saikolojia na maradhi ya maadili mabovu ambayo wameshindwa kuyaondosha. Hii yote imesababishwa na kuondosha mzizi mkuu wa sheria, nayo ni maadili! Hivyo, mataifa kama hayo wanajilazimisha kupunguza adhabu hadi kufikia uamuzi wa kwamba kuua sio tena adhabu halisi ya kosa la jinai.

  Tukae tufikirie, wapi tunakwenda? Mabadiliko mangapi tunayahitaji kwenye sheria zetu? Tuchambue na kuweka makini akilini mwetu. Hizo nchi zilizo endelea ambazo kila kukicha tunatamani kuiga kila kitu chao, wao wana sheria zinaruhusu utoaji mimba,wana sheria nyengine za kuruhusu maingiliano ya jinsia moja. Je tupo tayari pia kuzifuata hizi? Kama ni hivyo, tujitayarishie kufikiwa na makubwa zaidi kuliko vile tunavyoweza kufikiria.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Adhabu ya kifo haifai na ni ukatili mkubwa. baadhi ya sababu za kutoikumbatia adhabu hii:

  a) Baadhi ya wahukumiwa kifo, hata kama si wengi, huhukumiwa kwa makosa;
  b) Tunawapa tabu maraisi wetu kama Mkapa na Kikwete, na wengine watakaokuja, ambao kwa hakika adhabu hii inawakwaza;
  c) Njia zenyewe za kuwaua mara nyingi hazina utu na husababisha mateso makubwa;
  d) Uuaji wa binadamu ni kinyume cha maadili, ukifanywa na mtu moja au hata ukifanywa na jamii (serikali). Kumuua mwuaji ni kurudia kosa la kuua;
  e) Najua waliouliwa ndugu hupata uchungu mkubwa, lakini jee uchungu huo hupungua mwuaji akiuliwa?

  Kifungo cha maisha ni mbadala mzuri wa adhabu hii.
   
 4. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Jee wale ambao wameuliwa na watu wenya tamaa ya mali, kama vile Maalbino, watoto wachanga waliouliwa kwa sababu za kiushirikina, kitoto cha miaka mitatu kilichobakwa hadi kufa , ajuza chungu nzima waliouawa huki Shinyanga kwa sababu tu walikuwa na macho mekundu, mabwana fedha chungu nzima waliouliwa na majambazi tena kwa pesa zisizo zao, hao wote hatuwatetei kwa sababu washakufa, hivi wwewe ikutokezee mtoto wako wa miaka mitatu amebakwa hadi kufa utamsamehe kweli huyo mbakaji? kwa kweli kama mtu ameuwa kwa dhamira hasas ya kuua, basi na yeye auliwe, naomba kuwasilisha:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:
   
 5. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Je kuna magereza ya kutosha???
   
 6. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Mkuu kama mhusika akikutwa na hatia kwa kufanya hayo ambayo umeyataja, mi sioni adhabu nyingine mbadala zaidi ya kifo. Inakuaje unamtetea mtu aliyeua?.......hii hainiingii kichwani kabisa....utetezi utautoa endapo kama hayajakutokea (coz ya huruma ya kibinaadamu) ila yakitokea kwa ndugu au mwanafamilia yako ndio utajua umuhimu wa hii adhabu maana utakuwa umeshapata uchungu wa hali halisi ya kupotelewa ndugu au jamaa ktk hali ya kinyama.
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Wanaohukumiwa adhabu ya kifo si wengi kiasi hicho. Kama magereza hayatoshi ni kwa sababu ya wafungwa wengine.
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kupendelea afungwe maisha badala ya kunyongwa sio kumsamehe.

  Na hata hivyo, akishafungwa, kumsamehe ni muhimu kwa afya yako wewe aliyekukosea.
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hilo lingekuwa kweli adhabu ya kifo isingalikuwapo.
   
 10. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Aliyeuwa mtu kwa makusudi na bila ya hatia yeyote ile hafai kutetewa kabisa,

  adhabu yake ni kifo tu.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, huu mjadala bado ni endelevu, wakati baadhi yetu tukipigania kufutwa kwa adhabu ya kifo Tanzania kwa sababu ni barbaric, jana nimemsikia mtu akiomba Watanzania watakaohukumiwa adhabu ya kifo, wanyongwe.

  Paskali.
   
Loading...