Adhabu ya kifo ifutwe TZ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adhabu ya kifo ifutwe TZ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Apr 20, 2010.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau, nilikuwa nasikiliza BBC Swahili leo asubuhi na ndipo ilipokuja habari kuhusu adhabu ya kifo kwa upande wa nchi yetu. Takwimu zinaonesha kuwa kipindi cha awamu ya kwanza na ya pili walinyongwa wafungwa 204. Ripoti ikaendelea kusema kuwa awamu ya tatu mheshimiwa Mkapa alitoa msamaha wa wafungwa 101 wa kunyongwa na mheshimiwa Kikwete mpaka sasa 73...

  Jeh! Kuna haja ya sheria hii kuendelea? maana ni kama inakiuka HAKI ZA BINADAMU...
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,632
  Likes Received: 1,662
  Trophy Points: 280
  Hili la adhabu ya kunyonga ni dilema kubwa. Kwa maoni yangu si vema kuifuta. Kuifuta kunaweza kuongeza watu kujichukulia sheria mikononi na kulipiza visasi kwa watuhumiwa wa mauwaji.

  Hivi, jaribu kufikiria una bunduki/bastola halafu unamkuta mtu amemchinja mkeo na anamalizia kumchinja mtoto wako kipenzi....unafanya nini hasa ukijua kuwa hata muuwaji huyo akipelekwa mahakamani atafungwa maisha tu na si zaidi ya hapo?
   
 3. Mchapaji

  Mchapaji Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh! Kazi ipo then... Usemayo ni sahihi mkuu
   
Loading...