adhabu na mateso | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

adhabu na mateso

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MTOTO Jerry Martin [5] amelazwa katika hospitali ya MountMeru kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na adhabu na mateso aliyoyapata kutoka kwa baba yake mzazi.
  Jerry amekuwa akiteseka kwa muda mrefu kwa kupata adhabu kali kutoka kwa baba yake mzazi aliyetambulika kwa jina la Lema na kumsababishia majeraha makali maeneo yake ya mwili.

  Bw. Lema amekuwa akimtesa mtoto huyo kwa kile alichodai mwanae huyo amekuwa hajui kusoma wala kuandika na amekuwa akimuadhibu mara kwa mara kutokana na sababu hiyo aliyoidai.

  Imedaiwa kuwa Lema amekuwa akimuadhibu mtoto huyo kwa lengo la kumuua ili aweze kuoa mwanamke mwingine baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia.

  Imedaiwa kuwa, Lema amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa wanawake anaotaka kuwaoa kuwa hawataweza kulea mtoto wa kambo hivyo amekuwa akifanya hivyo ili mtoto huyo aweze kupoteza maisha ili aweze kuoa.

  Bw. Lema amekuwa akimuadhibu mtoto huyo kwa kumpa kipigo cha nguvu na hatimaye kumuunguza sehemu zake za mwili na wakati alipokuwa akifanya hivyo alikuwa akimfungia chumbani na kumziba mdomo ili sauti isiweze kusikika nje ya nyumba hiyo.

  Pia alikuwa akimlaza mtoto huyo nje ya nyumba mara kwa mara na kuthubutu kumnyima chakula .

  Na alimsihi mtoto huyo asitoe siri hiyo kwa majirani na watu wengine na akimbaini kuwa anatoa siri hiyo ya kumuadhibu alimuhidi kumtoa uhai wake.

  Hata hivyo mateso ya mtoto huyo yaligundulika na mwalimu wake wa shule ya awali kwa kumuona mtoto huyo akiwa dhofu na kusikia harufu kali ya vidonda vilivyotunga usaha yanayotoa harufu na ndipo alipomchunguza alibaini majeraha makali na ndipo papohapo alipokwenda kutoa ripoti katika kituo cha polisi cha Ngarinalo Arusha.

  Mtoto huyo amegundulika majeraha makubwa sehemu zake za makalio kuungua vibaya, maeneo yake ya kifua, mkono wake wa kushoto na imesemekana karibia mwili mzima ulikuwa na majeraha makubwa yaliyovilia usaha na kutoa harufu kali.

  Mtoto huyo alibainisha kuwa alikuwa akipata adhabu hizo mara nyingine kwa kupigwa na hata kuunguza na moto.

  Kutokana na hali ya mtoto huyo watu waliomuona wakati akikaguliwa waliweza kuangua vilio na hata askari polisi nao waliweza kutoa machozi kutokana na hali ya mtoto huyo.

  Asubuhi hii imedaiwa kuwa hali ya mtoto huyo imedaiwa kuwa ni mbaya na bado anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

  Kufuatia hali hiyo Lema anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 936
  Trophy Points: 280
  Taarifa za kiintelijensia(ya kwangu) zinaonesha kuwa CHADEMA wanataka kuleta uvunjifu wa amani kwa kumchochea(kiWASSIRA WASSIRA) huyo Lema ili amtie majeraha mwanae. Intelijensia zaidi imethibitisha kuwa mtoto wa Lema ameingia hofu. Wananchi wapenda amani tusikubali uchochezi huu kwani ni hatari kwa amani(pekee) aliyotuachia muasisi wa taifa hili. Uvumilivu ukimshinda Mhe. Rais tusilaumiane jamani(huku machozi yakinilengalenga)
   
 3. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Tamaa mbele, mauti nyuma!!
   
 4. n

  ntobistan Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muda wa mtot ukifika atawez kusom na kuandika hvy huwez kumlazimish pund kumywa maji!Huy mwanamke na mmew wote ni masnichi 2 kwan mtot ni mtot 2
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mwogope mungu wako nadhani wakati mwingine mzaha na siasa tuweke kando. Hapa tunazungumzia mtoto ambaye anapigania maisha yake halafu wewe unaleta mambo ya kiintelijensia watever. Pole nyingi kwa huyo mtoto mungu ni mwema na mwaminifu atakupigania. Uugue pole
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 936
  Trophy Points: 280
  We mkaka mbona una mwandiko mchafu hivyo, utafikiri peni yako umeiba na makwapa, jifunze sarufi uandike vitu kiGreatthinker bwana! Aaagh......
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Jamani.,.!!
   
 8. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Child abuse hiyo...ni kosa kubwa kumuabuse mtoto kwa namna yyte ile..sheria ichukue mkondo wake.
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  watoto kibao wanafanyiwa hivyo utashangaa mambo yanamalizwa kifamilia
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu leo aliuniuliza kuhusu Third world Countries. Ishu kama hizi ni common sana na zinapuuzwa. Sheria haziko wazi na kitengo cha sheria na haki za watoto kimelala. Walianza na Haki Elimu, Serikali ikawafungia. Pumbafu kabisa...
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  maumivu yana athari za kisaikolojia kwa mtoto!
   
 12. a

  atieno Senior Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hpa tuanajadili mtoto aliyejeruhiwa na baba yake siyo taarifa zako za kiinteligencia zisizo na mashiko, hakuna uhusianao kati ya mtoto kupigwa na baba yake,(lema) na cdm. acha kuchanganya madesa, kama ungekuwa na hoja ungeipost ili tuchangie na sio kuvamia.
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  jamaa kaingia kwenye siasa
   
 14. c

  chetuntu R I P

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali iamke kila siku watu wako ku seminars, workshops za child protection lakini hakuna hatua kali zinazochukuliwa kwa wazazi wakatili. Sheria na haki za watoto zipo maofisini tu. Hili nalo linahitaji UNICEF afund??? Haya mambo ya kumaliza kifamilia ifike mahali yakomeshwe.Nimechoka kusikia mtoto kachomwa mikono kwa kuiba au kosa lingine lolote.
   
 15. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  naomba nitumie au nipm ile ishu plz
   
Loading...