Adhabu kwa wana-JF watoa PUMBA.

Status
Not open for further replies.

Moseley

Senior Member
Jul 10, 2010
186
225
JF inajitanabaisha ya kwamba "It is a home of great thinkers"..

Lakini hili limekuwa si kweli kutokana na ukweli kwamba, kuna watu wanatoa maoni, hoja na ushauri wa kipuuzi kabisa. Ingawa si wote..

Kuna watu wanapatwa na matatizo mbalimbali, yakiwemo ya ki-ndoa, kielimu, kiafya, ki saikolojia, ki siasa nk.. Watu hawa huja hapa kutaka ushauri ili uweze kuwasaidia ktk maisha yao. Badala yake wanapewa uharo na ushauri usiofaa. Hii inasababisha kuwaongezea matatizo watu hao, badala ya kuwasaidia.

Pia kuna watu huanzisha hoja za ajabu ajabu kabisa, kiasi ambacho wanachanganya akili za watu..

Pendekezo:
MODs waweke utaratibu wa kugawa credit kwa wanaotoa point nzuri hapa JF, pia credit kwa watoa pumba. Hii inaweza ikawekwa kama poll flani, I mean, kama mtu ataongea point basi kuwe na button kwenye profile yake ambayo uki-click itamwongezea credit katika upande huo..

Na kama mtu ataongea pumba kuwe na sehemu ya ku-click ili kumwongezea point katika utoaji pumba..

Baada ya hapo, kuwe na utaratibu ambao kila jina la member lioneshe yeye ni mtoa pumba au mtoa point kwa kiwango gani..

Tunaweza tukatumia rangi au asilimia.. Mfano mtu akiwa na rangi nyekundu, ina maana we ni mtoa pumba mkubwa. Rangi nyeupe, mtoa point mzuri..


FAIDA YA HUU UTARATIBU:

1. Itasaidia kupunguza frustration kwa watu wanaokuwa wanaomba ushauri hapa JF, maana kuna watu tunawaongezea frustration kwa kutoa ushauri mbovu kabisa.

2. Itapunguza utoaji pumba humu ndani.

3. Watoa pumba watakuwa wanajulikana, kiasi kwamba, mtu atakaeomba ushauri toka JF, ataweza kufahamu kuwa mwana-JF aliemshauri si mtoa ushauri mzuri. Au mwana-JF alietoa hoja flani, si mtu mwenye kutoa hoja nzuri

NAWAKILISHA..
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,247
2,000
Sasa kama kunawatu humu wanaongea pumba mbona sasa wewe umeongeza idadi??Kwanza kuhusu button zipo mbili,yakwanza kuna ya mkono wakushoto imeandikwa"Thanks"hii umfanya mtu kuonekana post yake ina meaning"Usefull post" fulani,ya pili upande wa kulia pc kuna two thumb up and down kama unaona thread ni meaningless un thumb down kama ni meaning una thumb up sasa wewe na MS wako mnatujazia kwa pointi mfu.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
mbona tayari kuna REPUTATION POINTS, ambazo unaweza kumpa mtu aliyetoa points nzur.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom