adhabu kwa mawaziri wezi wa mali ya umma hairizishi kabisaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

adhabu kwa mawaziri wezi wa mali ya umma hairizishi kabisaa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tango73, May 27, 2012.

 1. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Jamani tumechoka kufanywa watoto katika nchi yenye amani na utulivu. Adhabu ya kuvunja baraza la mawaziri na kutowateua mawaziri wa badhilifu hailizishi kabisaa. Kama hawa watu wamefanya makosa makubwa ya ubadhilifu wa fedha za mali ya umma , kwa nini hawafikishwi mahakamni? Mbona waziri mkuu wa Ukraine mwanamke hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka minne kwa kutokuwa mwaminifi akiwa ktk offisi ya umma.

  waziri kigoda naye kaja na mpya. eti kamsimamisha mkurugenzi wa bureau of standard kwa tuhuma nyingi za kutokuwa mwaminifu. halafu kutufanya sisi ni watoto,anasema mambo mengine yatafuata mara uchunguzi utakapo fanyika. Hakusema uchunguzi huo unaanza lini na kwa nini haujaanza mara moja.

  Heshima tunayopoteza nchi za nje ni mara mbili ya kukojoa kitandani ukweni. serikali haioneshi hasira yeyote kwa wabadhilifu wa mali ya umma. serikali iko tayari kuonesha hasira zake kwa taifa la israel eti kwa nini wapalestina hawana nchi kuliko kuonesha hasira kwa watu ambao wanaturudisha nyuma kiuchumi na ustawi wa jamii. jamani sasa tufanyeje? miaka 50 ya uhuru, working class ya taifa ni 21%! wakulima wa kilimo cha ziki na umasikini 81% watu wasiolipa P.A.Y.E 85% kweli tumeachwa pabaya sana na siasa za ujamaa na kujiegemea halafu unakuta mwana siasa badala ya kupambana na hali halisi hiyo yeye ndio kwanza anaiibia serikali mali yake.

  wizi wa kuover bajeti ndio kwanza umashamili na umakuwa mtaji wa mawaziri. Jamani tuandamane kama wanavyofanya wa giriki na wahispani. la sivyo maharage yatabakia ni mboga ya anasa kwa walio wengi. !
   
Loading...