Adhabu kubwa na kali kwa mbunge, ni nani anaathirika zaidi..???

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Wakuu,
Nimejiuliza hili swali hasa kutokana na adhabu waliyopewa Mdee na Bulaya.

Adhabu hii ni kama wamepewa na wabunge wenzao huku ikipewa baraka na spika wa bunge Mh Job Ndugai.

Binafsi sipingi adhabu za bunge kwa wabunge, lakini ninachopinga ni adhabu kubwa na kali kwa wabunge, awe wa CCM, CHADEMA, CUF au chama kingine chochote, hasa ukizingatia wabunge wote pale ndani ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo husika.

Kwa adhabu ya Bulaya na Mdee, naamini bila baraka za spika labda isingekuwa kali kama ilivyokuwa. Lakini je, TUMEJIULIZA NANI NI MWATHIRIKA WA ILE ADHABU..??? Hatuoni kwmb MWANANCHI ndo atakuwa muathirika namba moja kwan atakuwa kapewa adhabu kwa kukosa mwakilishi bungeni...???

Hakuna ajuaye dhamira ya dhati ya mgombea wa kiti chochote wkt wa uchaguzi, bali ni yeye mgombea husika na Mungu wake, ila kila mtu anajua shauku ya wapiga kura ni MAENDELEO ya maeneo yao, na naamini kabisa spika kwa nafasi yake, licha ya kusimamia shughuli za bunge, na yeye ni mmoja wa wadau wa maendeleo nchini bila kujali jimbo ni la mbunge gani, au wa chama gani. Yawezekana kumsimamisha Mdee na Bulaya ikawa umewakomoa wao tu na umekata mfereji wa pesa zao za allowance, bila kuwaangalia wananchi wanaowawakilisha. Kwahyo wananchi hawana tena sehemu ya kufikisha shida zao kwa kipindi chote walichosimamishwa.

Nadhani kuna haja ya kufikiria upya namna ya utoaji adhabu kali kwa wabunge huku tukiwaweka watanzania kwanza, na sio mihemko ya kichama. Tukumbuke aliyepata adhabu ni mwananchi na sio mbunge husika, yeye anaendelea tu kula bata kama kawaida, na hana shida.

Nawasilisha.
 
WABUNGE WENGI WA CHADEMA WANAKOSA ELIMU ?

NaThadei Ole Mushi.

Kitendo cha Mdee na Bullaya kutolewa njee ya bunge kwa mwaka mzima kwa sababu ya vurugu ni kukosa utashi wa kisiasa.

Wataalamu wengi wa mambo ya kiuongozi wanaamini kuwa kiongozi mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kukamilisha malengo yake na kusimamia kile anachokiamini kwa kutumia hoja nzito

Tangia nimewajua CHADEMA NA UKAWA ndani ya bunge kama kambi kuu ya upinzani hawajawahi kupitisha hoja hata moja wakafanikiwa mara nyingi wakizidiwa hukimbila njee ya bunge.

Tatizo kubwa la upinzani nchini kwetu ni kwamba hawajawekeza kwa wasomi.Ngoja niwafundishe kitu wagiriki waliamaini sana kuwa mtu huzaliwa na skills za kiongozi kama wanavyoamini kuwa mbowe ni mmojwapo wa mtu aliyezaliwa kwa ajili ya kuwa kiongozi bila hata ya kupata training na yeye mwenyewe anaamini hivyo ukiwa na muda pitia "trait theory of leadership na charismatic theory of leadership"

Dunia ya sasa wanapinga sana nadharia hizo za kizamani za kigiriki dunia ya sasa inaamini zaidi kwenye EXPERIENCE ya mtu na ELIMU YAKE. Maana yake ni lazma mtu asomee uongozi ili aweze kufanya interaction na anaowaongoza vizuri, kufanya tafakuri ya kina ya mambo, kuamua kwa kutumia utashi nk.

Mfano duniani kwa sasa tunaamini contingency theory of leadership zaidi kuliko nadharia za kizamani za kigiriki, wanakuambia kuwa kiongozi atafankiwa katika uongozi wake tu endapo ana uwezo wa kuyafanya majukumu yake. Hapa hakuna longo longo ya sijui uongozi ni kuzaliwa ama laaa,kinachoangaliwa ni uwezo wakuyafanya majuku yako.

[HASHTAG]#HOJA[/HASHTAG]

Halima na Bullaya sijui elimu zao ila inawezekana wamehudhuria madarasa tu. Vitendo wanavyovifanya ndani ya Bunge huwezi kumkuta Zitto au Mbatia akivifanya.

#Je wananchi wa Kawe na Bunda wanahitaji watu wenye uwezo wa kupigana na askari au wanahitaji watu watakaoweza kuwaletea maji na huduma nyingine za kijamii??

[HASHTAG]#Heshima[/HASHTAG] aliyoipata mzee wetu Ndesamburo Jana huko Moshi si kwa sababu alikuwa hodari sana wa kupigana bungeni bali alifanikisha malengo na kuwatumikia wananchi wake kwa asilimia 100.

[HASHTAG]#Mifugo[/HASHTAG] ya lowassa (Nyumbu) karibuni kwa matusi maana hamuwezi kuelewa kilichoandikwa.

Ole Mushi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom