Mzee wa hat-trick
JF-Expert Member
- Nov 21, 2016
- 1,730
- 2,388
Wakuu,
Nimejiuliza hili swali hasa kutokana na adhabu waliyopewa Mdee na Bulaya.
Adhabu hii ni kama wamepewa na wabunge wenzao huku ikipewa baraka na spika wa bunge Mh Job Ndugai.
Binafsi sipingi adhabu za bunge kwa wabunge, lakini ninachopinga ni adhabu kubwa na kali kwa wabunge, awe wa CCM, CHADEMA, CUF au chama kingine chochote, hasa ukizingatia wabunge wote pale ndani ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo husika.
Kwa adhabu ya Bulaya na Mdee, naamini bila baraka za spika labda isingekuwa kali kama ilivyokuwa. Lakini je, TUMEJIULIZA NANI NI MWATHIRIKA WA ILE ADHABU..??? Hatuoni kwmb MWANANCHI ndo atakuwa muathirika namba moja kwan atakuwa kapewa adhabu kwa kukosa mwakilishi bungeni...???
Hakuna ajuaye dhamira ya dhati ya mgombea wa kiti chochote wkt wa uchaguzi, bali ni yeye mgombea husika na Mungu wake, ila kila mtu anajua shauku ya wapiga kura ni MAENDELEO ya maeneo yao, na naamini kabisa spika kwa nafasi yake, licha ya kusimamia shughuli za bunge, na yeye ni mmoja wa wadau wa maendeleo nchini bila kujali jimbo ni la mbunge gani, au wa chama gani. Yawezekana kumsimamisha Mdee na Bulaya ikawa umewakomoa wao tu na umekata mfereji wa pesa zao za allowance, bila kuwaangalia wananchi wanaowawakilisha. Kwahyo wananchi hawana tena sehemu ya kufikisha shida zao kwa kipindi chote walichosimamishwa.
Nadhani kuna haja ya kufikiria upya namna ya utoaji adhabu kali kwa wabunge huku tukiwaweka watanzania kwanza, na sio mihemko ya kichama. Tukumbuke aliyepata adhabu ni mwananchi na sio mbunge husika, yeye anaendelea tu kula bata kama kawaida, na hana shida.
Nawasilisha.