ADHABU KALI: Yagunduliwa Kigamboni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,738
155,421
WEZI A ambao wamekuwa wakiwasumbua wakazi wa Kigamboni kwa muda mrefu sasa, wameanza kukiona cha mtema kuni baada ya adhabu mpya kugunduliwa.
Jana mchana nilishuhudia wezi walioiba tangi la kuhifadhia maji wakiwa wanaadhibiwa mchana kweupeeee.
WEZI.JPG
 
Hii si adhabu wala nini, ule Australia watu 5,000 wamelala chini uchi by the Sydney Opera House just for fun. Ukiwakuta wenye shughuli yao watachekelea tu.

Upumbavu mtupu.
 
Hii imetokea wapi, ambako vyommbo vya dola vimelala fofofooooooooooooooooooooooooooooo! Wanakoroma, wakiwaachia wananchi wajifanyie wanavyotaka! Si kosa lao! Hawana jinsi! Kwa hiyo wananchi wezi wanaiba, wengine wanatoa adhabu, halafu kodi wanatoa kuwalipa waliolala!
 
daaah, lakini inatia huruma, ingawa wezi nao wanarudisha sana nyuma maendeleo yetu.
angalia jamaa walivyomajabali, mashababi hasa, majitu ya afya, ila wako uchiii wa mnyama.
Africa moto.
 
Teh teh teh,lakini tuko kama tumelaaniwa, wevi wakubwa twawapokea kwa vigelele maana na visualize EL, RA, AC na wenzi wao wakiwa wamebebeshwa MAHELA na VIJISENTI vyetu na nanihii zao shoto kulia
 
Jana ilikuwa kimbembe mitaa ya kwetu.
Walizungushwa tangu saa nne asubuhi hadi saa tisa.
Nilikutana nao mitaa ya jeshini, ilikuwa safi sana.
Kwa aibu waliyoipata nadhani itasaidia kupunguza wezi.
Sijui nifanya nini niibe halafu nivuliwe nguo, nizungshwe mji mzima halafu unakutana na wakwe zako na wanao, sijui sura utaificha wapi??
 
Jana ilikuwa kimbembe mitaa ya kwetu.
Walizungushwa tangu saa nne asubuhi hadi saa tisa.
Nilikutana nao mitaa ya jeshini, ilikuwa safi sana.
Kwa aibu waliyoipata nadhani itasaidia kupunguza wezi.
Sijui nifanya nini niibe halafu nivuliwe nguo, nizungshwe mji mzima halafu unakutana na wakwe zako na wanao, sijui sura utaificha wapi??
kwa hiyo kwenye hiyo picha wewe ni yule unaetabasamu kwa mbele, mwenye singlend ? ama ? maana Kiranja nawe umeshiriki kwenye tukio la aina yake.
Afrca moto
 
hahahahahahaha
bora hawajawaua maana hakuna adhabu nisiyoipenda kama kuua mwivi.
afadhali na wakome. walipaswa pia kubeba tangi lenye maji japo nusu ili kuwatia adab zaidi.

Anayesema polisi wapo wapi nadhani hajui kwamba hawa vibaka wanakiba hata ktk nyumba za hao polisi lakini hawana cha kuwafanya... teh teh
 
This is too sad. Yaani jamaa Midhakari na ****** nje nje. Sasa vitoto vidogo kweli kuona vitu kama hivyo ni sawa? Halafu tunajifanya kuruhusu biashara ya Mapenzi (sex busness) ni dhambi. Ovyo kabisa.
 
Lakini kipi kipya hapa?
Wenda uchi, ukosefu wa ajira, uwizi au ukatili? Ni kipi hapa tunaeza kuita 'ugunduzi'?
 
nasikitika kwamba vijana wamezungushwa for five hours bila polisi kuingilia kati, na hapo ni kigamboni tu!!! three minutes kutoka ikulu!!!

Lakini nadhani kwa adhabu ile, hawatarudia tena

Hata kama kukaa uchi australia ni sawa, kwa jamii yetu ni aibu sana na hii imewadhalilisha, i hope watoto walizuiwa kuona kengele za watu
 
walishaniibia tanki na pump ya maji baada ya kuvuja kisma changu cha kisasa na kuichomoa ikiwa chini kabisa (50m) huko huko kigamboni. hii adhabu sawa lakini ningependa wangechapwa na hamsa ishrini kila mmoja on top of that ili wakawasimulie wapenzi wao wanaokula nao hizi pesa wakiuza mali za wizi.
 
Adhabu Kali: Kweli ni adhabu lakini inadhalilisha utu. Wafikirie tu hao wanaume waliofanya hivyo, hawaoni kuwa nao wanajikashifu maumbile yao? Pia sidhani kama itasaidia chochote katika kutrekebisha tabia. Tuna haja ya kufikiria zaidi adhabu mbadala.
 
Dunia] imefika mwisho, Binadamu tumegeuka kuwa Wanyama hatuna utu kabisa.

Jiulize Watoto wadogo wakike na kiume walioona laivu kituko hiki, watakuwa wamejifunza nini pamoja na taswira ya picha iliyoko kichwani mwao?
 
Dunia] imefika mwisho, Binadamu tumegeuka kuwa Wanyama hatuna utu kabisa.

Jiulize Watoto wadogo wakike na kiume walioona laivu kituko hiki, watakuwa wamejifunza nini pamoja na taswira ya picha iliyoko kichwani mwao?
Wanajifunza kuwa Wizi ni mbaya, na ni mwiko kuiba, hahhahhahaaa, inanikumbusha ule wimbo wa kikojozi na nguo Tuzitie moto, enzi zilee unazungushwa mtaa mzima.
Africa moto
 
Back
Top Bottom