Adha za usafiri UDART/BRT zitaisha lini?

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
622
581
Hi adha itaisha lini? Hii ni leo asbh hapa Kimara Terminal
IMG-20171114-WA0001.jpg
IMG-20171114-WA0001.jpg
 
Huu mradi ni bora wangepewa wawekezaji tu,ama waturudishie daladala zetu
 
Hii kitu inahitaji kuweka washindani wengine, hawa udart naona kama wanakosa ushindani sasa wanajiona wamefika. Yawezekana wao wanajitahidi kadri ya uwezo wao ila kiukweli wanatakiwa waongeze mabasi mengi tu ma pia kuwe na mawasilianobya kutosha na traffic ktk makutano wasizuie gari za mwendokasi muda mrefu.
 
Huu mradi ni bora wangepewa wawekezaji tu,ama waturudishie daladala zetu
Udart pia ni muwekezaji, sio serikali!
Cha msingi waongeze wawekezaji, kuwe na kampuni tofauti zinatumia route hizi, jinsi ya ukusanyaji mapato na mgawanyo watajipanga ila wakiweka makampuni mengine ktk route kutakuwa na ushindani na matokeo yake ni huduma bora.
 
unakaa masaa mawilio kituoni, kwa asubuhi na mida ya jioni huu usafiri ni kero kweli
 
Hakuna namna wameshashindwa.

Leseni za daladala za posta, kariakoo, kivukoni na Muhimbili zitolewe kwa wenye mabasi makubwa kuanzia Mbezi.
 
Kumbe ulikuwepo nafikiri kunahitajika mtaalamu wa "Fleet Management " pale UDART kwani mabasi yalifurika pale abiria walipolianzisha. Pia kuna haja ya kuwa na askari wa kutosha pale kwani nilichokiona leo mtu mmoja anaweza kuanzisha "move" ikaleta madhara makubwa sana.

TUSISUBIRI MAJANGA KWANZA TUJIPANGE, Abiria pia tuwe na SUBIRA, Wazee walisema " SUBIRA YAVUTA HERI". Nilichokiona leo nimeogopa sana.

Kama kuna shida sana, yaani ipo nje ya uwezo wenu tafadhalini Daladala ziruhusiwe kwa route za POSTA na KARIAKOO.

Narudia yatatokea majanga tusipochukua tahadhali, kama kuna mtu humu anafanya UDART awaeleze viongozi mapema kwani kwenye website yao sehemu ya kutoa maoni/feedback inasema " Coming sooon....."
 
Nimeona kwenye "clip",kuna mtu kanitumia hiyo dhahama,kwamba abiria wamekaa muda mrefuuu bila magari na huku magari yameegeshwa tu eneo la Kimara Terminal.

Ule upande ambao abiria hawaruhusiwi kufika,leo wamevuka na kutaka kuleta vurugu,polisi wapo wachache na wamezidiwa kuwatuliza abiria,vurugu zimesababisha watu wengi kuingia upande wa waliolipia bila kulipa,hivyo wengi wamesafiri bure leo kuelekea Morocco,Kivukoni na K'koo.

Huu mradi sijui unaogopwa na nini?Huyu Simoni Kisena amekuwa sugu,JPM anagusa kwingine koteeeee,lakini huu ufisadi wa UDART anauogopa!!Hapa yupo Kisena,yule aliyefisidi Nyanza Chama cha Ushirika,huyu ndiye mwenye New Era na kafisidi "Ginneries" za Magu...Aibu sana sana
 
Uda kwa nini ilokufa?
Mashirika ya umma yalikufa kwa upuuzi huu huu.

Waliopewa mamlaka kujisahau
 
Naungana na mleta mada. Kuna usumbufu mkubwa na kubananishwa kama nyanya kwenye hayo mabasi yao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom