Adha za Mwendokasi: Abiria wamejaa kituoni, magari yamepaki

mkuu,
sayansi ni:
The intellectual and practical activity encompassing the systematic study of the structure and behaviour of the physical and natural world through observation and experiment.

na matumizi ya sayansi katika kutatua matatizo ya wanadamu ndio inaitwa technology

hivyo basi, neno technology haliishii kwenye flow of electons na digital appliances kama unavyofikiri, bali hata kwenye miradi kama Dsm Rapid transport facilitation, ndiomaana ulibuniwa na kujengwa na watu wanaoitwa ma Engineers waliokaa darasani kwa miaka minne au zaidi kusomea hyo tecnology unayoikana hapo!

however, i stand to be corrected, buy FACTS!

au kama vipi tuseme mwendokasi ni siasa au sanaa! au sio
Kwa kukubali kuelekezwa nachukua nafasi hiyo adhimu.
Mwendo kasi ni mfumo unaohusisha barabara, (miundombinu na mifumo ya kompyuta) mabasi (magari) na nguvukazi.

Sitakopi wala kupesti chochote kutoka kokote!
 
Ni aibu sana mkuu mradi mzuri sana ule kama ungefanywa kitaalamu...

kuna swali hua linaulizwa sana na vijana, kwamba ivi tukiamishiwa marekani na wamarekani wakahamishiwa hapa mambo yatakuaje...ndio tunapata majibu kwenye mambo kama haya...kwamba baada ya mda mfupi tuu pale L.A pataanza kuvuja maji machafu katikati ya barabara, watu wataanza kuning'inia kwenye ma trum, yale ma empire state buildings yataanza kudaiwa kodi za malimbikizo ya umeme na tanesco mwishowe yatakatiwa umeme, watu wataanza kupanda gorofa ya 10 na ndoo za maji, zile treni za umeme zitalaza watu porini,mashirika ya ndege ya pan am yatafanya safari za ndani tuu, kuna siku kwenye ndege wtu wawili watapewa tiketi moja na baada ya kigombana mda mrefu itabidi tuu mmoja asafiri amesimama!

yote haya tatizo ni moja tuu....matumizi finyu ya akili ambayo MUNGU ametupa bureeeee

Uko sahihi kabisa. Tatizo letu ni discipline, na si kitu kingine zaidi ya hicho. Principally, ukifanya uchunguzi wa kina utakuta kwamba MARA NYINGI, KAMA SIYO MARA ZOTE, WENGI WETU HUWA HATUFANYI KILE TUNACHOTAKIWA KUFANYA. Unakuta mtu ameajiriwa na kapewa mwongozo wa namna ya kutimiza majukumu yake, lakini na yeye ana JOB DESCRIPTION YAKE KICHWANI KWAKE NA NDIYO ANAYOITUMIA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE. Most worse, ukute sasa mtu huyo kajaribu ku-excel akawa boss, kiasi kwamba ana surbodinates chini yake, yaani ni balaa. Sasa unakuta kundi la namna hii wapo sehemu nyingi tofauti tofauti na hawajuani, na kila mmoja anafanya akiwa anajua kuwa ni yeye tu anayefanya hivyo, kumbe kuna wengine pia wengi zaidi yake, nao wanafanya hivyo hivyo! Haya mambo yanarudisha nyuma sana maendeleo ya Nchi na ukinifuata mimi hapa nilipo, ndani ya dakika 5 naweza kukuonyesha watu wa aina hii wasiopungua 10!
 
hii ndio inaitwa typical usahili.....tunaletewa technology mpya, nzuri kabisa lakini itatushinda.....tatizo jamani sio kukosa mali tatizo letu ni kukosa akiliii.........hata ile airport mpya, si unaona ilivyo designiwa vizuri? ipe miaka 3 ya kuendeshwa kiswahili utaona...utasikia mara vyoo havifush! mara parking za ndani zimefungwa mkaparkie terminal 2, counter zimejengwa 20 lakini huduma zinatoa 3!...

huu mfumo wa mwendo kasi ni uliletwa kwa nia nzuri kabisa, lakini ukakutana na vichwa vyenye matatizo na majanga, umepoteza maana watu wamerudi kwenye daladala za kawaida.......
Wa tz kama were tupo wachaxhe sana,big up..nawaambiaga watu tz tunakimbilia vitu ambavyo uwezo wetu kama nchi bado,digital tutaiweza vipi ?Yale ma gate ya Udart Ku scan tickets hayafanyi sasa hivi,vituo karibu vyote toka vifunguliwe milango INA operate upande mmoja tu hii inaleta usumbufu kwa abiria wanaposhuka au kupanda...yaaani totally failures

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asalam alaikum
Hii project kwakeli ni nzuri sana, mara ya mwisho kupanda mwendokasi ilikuwa 2016 na kiukweli uongozi waliopewa hii project ni watu wa hovyo kabisa. Mabasi yamejaa tele lakini wanayapaki na kusubiri watu wajae ili waje, na muda mwengine unaweza kusubiri mpaka nusu saa. Ukienda nchi zingine na kuona public transportation zao wanavyoziendesha utafurahi, zinafanya kazi kwa muda uliopangiwa bila kuchelewa, kwasababu wanaheshimu muda ila bongo ni shida tuu.
Hao viongozi wa hii project wanatakiwa kujifunza kwa wengine kwa uhodari wa kuendesha vitu kama hivyo.

Wasalam
 
Back
Top Bottom