TWIZAMALLYA
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 397
- 81
Wadau mimi ni mmoja wa wahanga wa usafiri wa daladala hapa mjini. Hali ni mbaya sana kwa sasa, kwani inapofika jioni daladala nyingi zinakatisha route zake. Watu wa mbezi ya Kimara watakubaliana na mimi.Ukiwa posta mpya pale ikija dalada ya mbezi mara nyingi hawashushi abiria kituoni.Watapitiliza mbele na kuanza kushusha. Ukijidai kuikimbilia dala dala utakutana na kauli kuwa hatupakizi tunaenda gereji.Option inayokuwepo kwa mtu wa mbezi ni kupanda daladala mpaka ubungo pale napo huwezi kupata gari ya mbezi unachotakiwa ni kupanda daladala ya kimara,ukifika kimara pale utakuta gari za mbezi nyingi tu. Kwa kuangalia tu hili tatizo ni la kutengenezwa na madereva wa daladala.Hapa najiuliza hivi hawa SUMATRA kweli hawaoni hili tatizo?.Au hili si sehemu ya kazi zao na kama ni kazi zao naona hawa jamaa watakuwa wananuka rushwa sana. Maana wananipa kufikiria kuwa wenye daladala wanamchango wa hela kwa ajili ya sumatra.
Kipindi cha MAJEMBE AUCTION MART walipopewa kazi mambo yalikuwa tofauti sana. Kwa vile daladala zote nchini zinamilikiwa na wakubwa hasa viongozi wa ccm wanaoongoza kwa uchafu hapa nchini, Majembe waliondolewa kufanya kazi ile ambayo ilikuwa inawaletea ahueni wananchi wa kawaida.Hali inazidi kuwa mbaya hakuna mtu anayejali kwa hili, hapa siongelei foleni naongelea tatizo la kukatisha ruti kwa daladala.Mfanyakazi wa kawaida kima cha chini serikalini atawezaje kumudu garama za maisha kama analazimika kupanda dala sita kwa siku kwenda na kurudi kazini?. Wakati ambapo kama serikali yake ingekuwa inamjali ingeweka angalau udhibiti kidogo kwenye eneo hili.Kuleta maisha bora kwa watu si lazima kuongeza mishahara kila wakati ni pamoja na kuweka usimamizi mzuri kwenye mambo mbalimbali yanayomhusu raia. Nadiriki kusema ccm nchi imewashinda kabisa.