Adha tuzipatazo abiria wa daladala

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
11,734
12,024
Pamoja na changamoto, machungu, hasira, manyanyaso, nauli, kukatishwa kwa route, msongamano, kukosa hewa hasa nyakati za foleni, uhatari kwa wanafunzi na watoto wadogo.

Nini kifanyike?
 
mara nyingi adha za abiria zinachangiwa na abiria wenyewe mtu anapoanza kudai haki yake utaona badala ya abiria kumsapoti wao ndio wanamsapoti dereva au konda
 
Adha nyingine ni pamoja na:
  • Hao makonda wa daladala na kutofua nguo zao za ndani na hasa wale wa vipanya, utakuta pale wanapochungulia nje kupitia dirisha la mlango harufu kali inakuja kwa abiria wanaokaa viti viwili vya mlangoni
  • Kugonga bodi la gari kama ishara ya kumwamuru dereva asimamishe gari au aondoe gari badala ya kumwambia kwa mdomo "simama" au "twende"
  • Kufungulia muziki kwa sauti kubwa bila kujali mchanganyiko wa abiria waliomo kwenye bus husika kama wanaupenda au kutoupenda huo muziki
  • Mwendo kasi hasa pale itokeapo wanawahi abiria katika vituo vinavyofuata
  • Kuegesha daladala kwenye makutano au njiapanda za barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hizo
  • Kusimama kupakia abiria kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa kupakilia abiria
Nini kifanyike
  • Mamlaka husika kama SUMATRA na wanaumoja wa wamiliki wa hizo daladala zianzishe utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mwili na mavazi kwa kushitukiza
  • Kila kondakta na dereva wawe na vitambulisho vyenye picha zao na namba zinazoonekana ili abiria waweze kuwareport kwa mamlaka husika pale wanapokwenda kinyume cha taratibu za kazi zao
  • Mamlaka husika ziwahamasishe wananchi kutumia mtandao wa whatsapp kurekodi na kutuma picha na video za madereva na makondakta wao pale wanapokiuka sheria
 
Sa nyingine daladala burudani mbona... acheni wengine tuenjoy hasa route za jioni na asubuh
 
Pamoja na changamoto,machungu,hasira,manyanyaso,nauli,kukatishwa kwa route,msongamano,kukosa hewa hasa nyakati za foleni,uhatari kwa wanafunzi na watoto wadogo.

Nini kifanyike?
Tatizo ya hizi kero ni sisi Abiria wenyewe na wa kuzitatua ni sisi wenyewe. Serikali ilishapiga marufuku kwa daladala kusimamisha Abiria ....lakini Abiria Wakaja juu kwamba wanachelewa na safari zao. Mbona Kenya imeweza kutatua hili suala!!???
 
Adha nyingine ni pamoja na:
  • Hao makonda wa daladala na kutofua nguo zao za ndani na hasa wale wa vipanya, utakuta pale wanapochungulia nje kupitia dirisha la mlango harufu kali inakuja kwa abiria wanaokaa viti viwili vya mlangoni
  • Kugonga bodi la gari kama ishara ya kumwamuru dereva asimamishe gari au aondoe gari badala ya kumwambia kwa mdomo "simama" au "twende"
  • Kufungulia muziki kwa sauti kubwa bila kujali mchanganyiko wa abiria waliomo kwenye bus husika kama wanaupenda au kutoupenda huo muziki
  • Mwendo kasi hasa pale itokeapo wanawahi abiria katika vituo vinavyofuata
  • Kuegesha daladala kwenye makutano au njiapanda za barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hizo
  • Kusimama kupakia abiria kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa kupakilia abiria
Nini kifanyike
  • Mamlaka husika kama SUMATRA na wanaumoja wa wamiliki wa hizo daladala zianzishe utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mwili na mavazi kwa kushitukiza
  • Kila kondakta na dereva wawe na vitambulisho vyenye picha zao na namba zinazoonekana ili abiria waweze kuwareport kwa mamlaka husika pale wanapokwenda kinyume cha taratibu za kazi zao
  • Mamlaka husika ziwahamasishe wananchi kutumia mtandao wa whatsapp kurekodi na kutuma picha na video za madereva na makondakta wao pale wanapokiuka sheria
Wewe wafaa kuwa KIONGOZI
 
Sa nyingine daladala burudani mbona... acheni wengine tuenjoy hasa route za jioni na asubuh
NI kweli ila kwa upande wa kero mara nyingine ktk vyombo hivi kuna wagpnjwa na wazee pia walemavu......kwa hali hii MAISHA HUWA MAGUMU SANA ....
 
Back
Top Bottom