Kila mwanachi anastahili kupata utulivu nyumbani kwake. Hiyo ni haki ya msingi kwa kila raia. Mbali ya hayo wengine tuna wazee wenye matatizo mbali mbali, wengi wao wanahitaji utulivu majumbani mwao. Pia wengine tunawatoto wachanga, kina mama wajawazito etc etc.
Kelele za aina yoyote hazipaswi kufanyika katika maeneo waishio watu. Haijalishi ni matangazo ya nini. Hata kama ni matangazo muhimu kama vile dini, basi haipaswi kupita mitaani kupasua masikio yetu na nyimbo za dini kwa kisingizio cha Mungu. Mwenye kutaka kusikia hayo aende kanisani au misikitini. Sio haki kusumbua watu kwa kisingizio cha dini. Hata Mungu hapendi uwe msumbufu kwa wengine. Kama kweli wewe ni mtu wa Mungu basi hupaswi kuwa msumbufu kwa wengine.
Jambo la kushangaza hawa watu wanapewa vibali na watumia vibali hivyo kuwa adha kubwa kwa wananchi.
Tunaomba Serikali ya Awamu ya 5 ilichukulie hili jambo kwa karibu na kudhibiti utoaji wa vibali kiholela. Utulivu wa wananchi upewe kipaumbele na uzingatiwe.
Asanteni.View attachment New saved.mp4
Sent using Jamii Forums mobile app