Adha,karaha,mateso na machungu ya siasa za majaribio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adha,karaha,mateso na machungu ya siasa za majaribio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Oct 8, 2008.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wana JF,
  Nadhani wengi wetu tumeshawahi kukumbwa na mateso au adha na karaha zilizotokana na majaribio ya wanasiasa na viongozi wetu toka tupate uhuru hadi leo. Nadhani kama tungepata wasaa wa kubadilishana uzoefu... basi tungepata mambo mengi sana - machungu, ya kuchekesha na kusikitisha.
  Mifano michache ni sera zifuatazo?
  1.Azimio la Arusha - Utaifishaji wa mali na njia kuu za uchumi - watu walipoteza mali zao na wengine hata kupatwa magonjwa kama presha n.k
  2.Mwongozo - Kiongozi asiwe mnyampala - matokeo yake hakuna aliyejisikia kuwajibika maana kumwajibisha mtu ilikuwa ni unyampara na consequences zake ziliweza kuwa mbaya
  3. Vijiji vya ujamaa - nadhani tumeshasoma mengi katika thread ya Dr Kleruu - japo tunahitaji kusikia visa na mikasa zaidi
  4.Operesheni Maduka - Watu walilazimishwa kuwa na maduka ya ushirika badala ya maduka binafsi
  5. Azimio la Musoma - Vijana walitakiwa kufanya kazi miaka miwili kwanza baada ya kidato cha sita ikabla ya kujiunga na chuo kikuu - na ilibidi upate barua kutoka tawi la chama na anayekuandikia barua hiyo pengine hata hajawahi kumaliza darasa la saba!
  6.Operesheni kuondoa nguo fupi, nguo za kubana, kuvaa mawigi n.k. Hii nimesahau ilikuwa inaitwaje kwa usahihi
  7.Nguvu Kazi -
  8.Uhujumu uchumi
  Na nyingine nyingi.
   
 2. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Womanofsubstanc,

  Hili swala la azimio mie halikai vizuri kabisa, kila mara kumekuwa na azimio maamuzi yaliofikiwa hayana mwelekeo mzuri wala strategy ya maendeleo, azimio la arusha ilikuwa ni disaster kwa nchi, azimio la musoma halikuwa na maana yoyote ya maendeleo na azimio la zanzibar ndio lililotuletea majanga makubwa ya akina richmond na epa na zinginezo.

  Kwa mtizamo wangu naona kama viongozi wanakuwa hawana mkakati wowote basi wakikaa huko wanakurupuka tu na azimio sijui la sehemu gani basi wanalishikia bango as if it was the best thing coming out of their sitting. Hakuna feasibility study, hakuna strategy, hakuna malengo na utekelezaji wa haya maazimio unakuwa ni kuwasukuma wananchi ambao hata hawaelewi hayo maazimio yana vitu gani ndani yake.

  Ukiangalia kwa haraka haraka kwa mfano azimio la arusho ilikuwa ni issue nyeti ambayo kwa namna moja iliwagusa wananchi moja kwa moja na kwa upande mwingine ilihitaji preparation, vyote hivi havikufanyika na wananchi hawakujua ni kwa nini wanahama! Kwa kifupi haya maazimio hayapaswi hata kuwepo kabisa!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  GM,
  Nakuelewa kabisa unachosema..ila hujasema kama wewe binafsi au hata familia yako iliathirika vipi na sera hizo.
  Binafsi nakumbuka kwa mfano katika kutekeleza sera hizo kulikuwa na propaganda nyingi sana...tena nyingine za kutisha. Nikiwa bado sijaelewa vizuri siasa, kulikuwa na nyimbo za kuwabeza watu kwa mfano akina Oscar Kambona waliokimbia Azimio la Arusha - licha ya kutuhumiwa kwa uhaini.. pia nakumbuka hadithi kama " Ndoto ya Ndaria" ambazo zilikuwa zinaeleza maisha katika vijiji vya ujamaa. Kwa kiasi kikubwa kama mtoto niliogopa sana kusikia ati watu wanaenda kuishi pamoja katika vijiji, wakilima pamoja, na kugawana sawasawa kila kinachopatikana! Nakumbuka pia mazungumzo baada ya habari kwenye redio RTD na sauti za kuogofya wakisema " ubepari ni unyama"..hii ni kutokana na kulenga ujumbe kwa kila mtu bila kujali uelewa wa wahusika.
  Kilichonishangaza zaidi ni baadae kuja kuona kuna matawi ya chama na UWT sehemu za kazi.Cha ajabu wenyeviti mara nyingi walikuwa ni aidha wahudumu au watu wa ngazi za chini sana..na hawa kichama walikuwa na nguvu sana hata kushindwa Executives...hii ilifanya uwajibikaji kazini kuwa mgumu sana.
  Pia nakumbuka kuona uendeshaji wa zoezi la nguvu kazi ambapo watu walikamatwa ovyo alimradi huna kitambulisho na kupelekwa Gezaulole.Mifano ni mingi tu na yote kama ulivyosema hakukuwa na mikakati mizuri au maandalizi.Mazoezi mengi yalijifia bila kuleta mafanikio.
   
 4. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Womanofsubstanc,

  Gezaulole inanikumbusha mbali kidogo hapo, anyway, kukujibu ni sawa na nilivyojibu katika thread ya Dr. Kleruu.

  Mia binafsi au nisema familia yangu imeathirika sana na azimio la Arusha hasa upande wa ardhi. Kuna wale waliohamishiwa katika maeneo ya watu kwa mfano mimi katika ukoo wetu pamoja na eneo kubwa tulilokuwa nalo watu wengi walihamishiwa na kugawiwa maeneo ya kuishi hapo. Sasa baada ya miaka mingi na ujamaa kuanguka wengi wameweza kurudi katika mashamba yao huku wakiendelea kushikilia na maeneo ambayo walihamishiwa hapo kwetu, tatizo ni kuwa kama sisi familia yetu haina pa kuhamia, hatukutoka popote tulikuwa hapa hapa. Hatuwezi kuhamia maeneo hayo kwa sababu baadhi ya hawa jamaa wamerudi maeneo yao ya zamani na wamechukua mashamba yao na vile vile wamegoma kutoka katima maeneo yetu ambayo kwa haki walipewa na serikali. Kwa kiasi fulani kuna uhasama na uchungu na majirani zetu ambao tunaona kama wanakuwa so unfair kukataa kuhama wakati tayari wameishajichukulia maeneo yao ya zamani, sisi hatuna eneo la zamani la kuchukua. Hali kama hii nafikiri inaweza kuwa ipo sehemu nyingi na wakati mwingine ukifiriria hizi hostilities unaanza kuona kuwa huko mbele watu wanaweza kupigana au kuuwana bure!
   
 5. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mtizamo wangu Lengo la azimio la Arusha lilikuwa ni kutaifisha njia kuu za uchumi kwa kuwanyang`anya wale waliozitolea jasho na kuzikabidhi si mikononi mwa umma bali kuzikabidhi mikononi mwa viongozi ili iwe zamu yao kuzitafuna na kuzifaidi mali hizo.

  Azimio la Arusha lilikuwa na lengo la kuwaneemesha viongozi wafaidi vilivyotaifishwa.

  Walijiuliza swali wakitaka wafaidi mali za raia baada ya kupigania uhuru wafanyeje? Wakaona dawa ni kuzitaifisha kwa kusema ni za umma halafu wanaweka viongozi wapendwa na ndugu na marafiki na wapambe halafu wanazila hadi kufilisi.

  Lengo la Utaifishaji lilikuwa kuzitoa kwa wenye nazo kukabidhi kwa viongozi waafrika wazitafune,wahakikishe viwanda,mashirika na mali walizochukua zinafilisiwa mikononi mwao kwa kuzitafunna barabara hadi wahakikishe kama ni shirika au kiwanda kinakufa kabisa.

  Mali nyingi zilizotaifishwa zilifia mikononi mwa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mali hizo.Walioua viwanda na mashirika yaliyotaifishwa ni viongozi siyo umma wa watanzania wanyonge.

  Azimio la Arusha lilikuwa ni neema ya kuwaneemesha viongozi wafaidi vilivyotaifishwa.

  Na hata zile zilizobaki baki kama mali ya umma kama viwanda na mashirika ziliuzwa kwa bei za ajabu zinazoashiria mazingira kama ya ulaji rushwa vile kwa viongozi waliouza.Waliuza kwa kuambulia kafaida.

  Ndiyo maana hata mali kama nyumba za serikali ambazo Azimio la Arusha lilizitambua kama mali za umma Viongozi wengine waliamua wauziane bei za kutupwa ili zile zilizokuwa zikiitwa mali za kudumu za umma ziwe zao za kudumu.

  Wako wananchi maskini walikuwa hawajui ajenda ya Azimio la Arusha waliokufa kwa kutembea kwa miguu kushangilia hilo azimio la Arusha la kibwege kama akina Seth Benjamin.

  Kuna wengi walitunga nyimbo za kusifia azimio la Arusha na kucheza kwa nguvu kutikisa viuno kwenye ngoma za kienyeji waonekane wachezaji wazuri kwa Nyerere lakini ukweli unabaki pale kuwa leo wanaoweza kueleza uzuri wa Azimio la Arusha si waimbaji,wacheza ngoma na wakereketwa wa azimio la Arusha bali wanaolijua vizuri na wanaoweza kulisifia vizuri ni viongozi waliokula vilivyotaifishwa hadi wakafilisi.
   
 6. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Netenyahu,

  Hakuna kitu kilikuwa kinaudhi kama mameneja wa mashirika ya uma wakiboronga huku wanahamishiwa kule bora tu mchezo unaendelae na magari yao ya kipindi kile ya SU! kama vile mtu alikuwa anajua tu hapa nichote wakishtuka watanitupa kwingine tena.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  You had to belong! MITANDAO HAIKUANZA LEO... hao mameneja walikuwa wanateuliwa hakuna interview wala nini! Haikujalisha kama una qualifications wala nini maradi uwe kwenye circles.Nakumbuka kuna meneja mmoja alipelekwa kusimamia taasis moja ilhali hakuwa na sifa wala uwezo - ni kwa vile tu alikuwa mtoto wa kigogo! Wafanyakazi walitishia kugoma.Kuokoa jahazi alipelekwa crash programme on Industrial psychology! akarudi ila sikumbuki kama aliendelea na umeneja pale au alipewa ulaji kwingine!
   
 8. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndio kufa kufaana huko.............
   
Loading...