ADC ni Mwarobaini wa Changamoto za Kiutawala Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ADC ni Mwarobaini wa Changamoto za Kiutawala Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omutwale, Sep 6, 2012.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Samahani kama nitamuudhi mtu. Lakini ukweli utajidhihiri baada ya uchaguzi hapo 2015. Kumekuwa na changamoto nyingi sana katika kuendesha Serikali ya Mseto huko Zanzibar. Mipango mingi hata ile ya maendeleo na maslahi kwa nchi haitekelezwi kama ilivyopangwa, hakuna siri za kiutawala zinazohifadhiwa na kubaki kuwa siri hata kama ni nyeti kiasi gani kwa usalama na maslahi mapana ya Zanzibar na Wazinzibari. Kila kitu kinaangaliwa kwa mtazamo wa kisiasa na kupimwa kwa maslahi ya kisiasa na kiitikadi kuelekea 2015. Pongezi kwa viongozi wa CDM maana hili waliliona mapema na kusema HAPANA kwa sauti kubwa.

  Ili kuondoa kabisa changamoto hii, serikaliya ccm imekwishaamua kwa dhati na iko katika utekelezaji wa uamuzi kuhakikisha katika uchaguzi wa 2015 kunakuwa hakuna ushindi wa kukaribiana na chama chochote cha upinzani huko Zanzibar. Na kanuni kama kawaida ni “Divide and Rule”. Carrier wa Mipango ya uamuzi wa serikali ya ccm si mwingine bali ADC. Hiki chama kitaendelea kufaidi rasilimali na mali kujengwa na kujijenga huko visiwani Zanzibar. Serikali ya ccm inaamini kuwa wanachama wake ni waaminifu na royal hivyo hawewezi kugeukia CUF wala ADC bali wale wana CUF ndo wanaweza kugeukia ADC. Na kwa wale wapya hasa vijana serikali ya ccm inao mpango madubuti utakaohakikisha inapata lion’s share. Haya yakifanikiwa, katika uchaguzi wa mwaka 2015, serikali ya ccm inataka kuhakiksha inaufanya uchaguzi kwa upande wa Zanzibar unakuwa kweli huru na wa haki ili kusiwe na sababu za wazi kupinga matokeo na kuanzisha vurugu. Ni imani ya serikali ya ccm kuwa karibu nusu au zaidi ya nusu ya kura za CUF zitakwenda ADC na hivyo CUF inaweza kuwa karibu sana katika matokeo na ADC wakati ccm ikiwa juu sana kwa kuwaacha wote hao wawili. Matokeo haya yatawekewa mazingira ya kisheria kuondoa serikali ya mseto na mgawanyo wa madalaka kati ya mshindi wa kwanza na wa pili.

  Icho Ukionacho, Sicho!.
  Fumbuka Uangaze Mbele Ufike kwenye Kilele!
  Acha Kupiga Kelele!
   
 2. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bwana Icho ni vyema katika kuleta HOJA zetu mtandaoni kutambua WaTanzania na hasa Wazanzibari wanahitaji wajengewe HOJA zenye ukweli na upeo sawia katika Medani ya Siasa za Zanzibar. Ili HOJA yako iwe na Mashiko lazima uwe na utambuzi na uchambuzi juu ya chanzo cha kuanzishwa kwa ADC ukIleta fikra kwamba ADC imeanzishwa kwa ajili ya Divide and Rule ili CCM iweze kuendelea kutawala Zanzibar HOJA Yako Inakosa Mashiko. Na HOja yako inaelea kwani ina fikra mgando ya Kujaribu kuwapotosha Wazanzibari juu ya NGUVU,UIMARA,UMAKINI NA UBORA WA ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE (ADC). ADC ni chama makini na Chenye nia CHANYA katika kuleta mabadiliko ya kweli NCHINI Tanzania imekuja na DIRA YA MABADILIKO ili kuweza kumletea MTanzania TUAMAINI CHANYA katika maendeleo ya jamii, uchumi na utamaduni. Ipo ili kuondoa aina zote za dhulma, ukandamizaji na rushwa hapa NCHINI mwetu. Nadhani ni muda KUAFAKA sasa kwa Watanzania kuiunga MKONO ADC kwa sera zake bora na zenye kutekelezeka.
   
Loading...