Adam Shafi katimiza miaka 80: Kalamu ya Shafi katika kuieleza Zanzibar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,910
30,253
ADAM SHAFI KATIMIZA MIAKA 80: KALAMU YA SHAFI KATIKA KUIELEZA ZANZIBAR

Nilikuwa nimeanza kukisoma kitabu ‘’Haini,’’ cha Shafi Adam Shafi na haikunichukua muda kutambua kuwa mikononi mwangu nina kitabu ambacho ni ‘’masterpiece,’’ yaani kitabu kilichosheheni ujuzi wa hali ya juu sana katika uandishi.

Hapo hapo ikanijia hamu ya kuzungumza na mwandishi.

Adam Shafi namfahamu kwa kumuona lakini sina mazoea na yeye na nikatambua na yeye akiniona atanitambua.

Nikampigia simu jamaa yake Mohamed Mshangama kumuomba simu ya Shafi Adam Shafi.

Nikampigia.

Baada ya salamu na kujitambulisha jina bila ya kuweka ‘’nicities,’’ nikamwambia, ‘’Sheikh Shafi hivi unadhani wewe utamdanganya nani?

Wewe unaandika kitabu cha historia ya kweli kisha unasema hii ni ‘’fiction,’’ hadithi ya kutunga.

Utawadanganya wengine mimi nishatambua kuwa hiki kitabu ‘’Haini,’’ni mambo ya kweli kabisa.’’

Ikiwa wewe si Mswahili na huna mazoea na huyo mtu aliyekupigia simu na lugha yake ni kama hii kali ya ‘’wewe,’’ utapata shida ya kutambua ujumbe ndani ya maneno yale na huenda ukaghadhibika kuona mtu humjui anakupigia simu ya kukushambulia.

MBALI NA NYUMBANI.jpeg
 
Nilisoma riwaya yake ya Vuta n'kuvute.

Mungu amtunze. Naona Hussein Tuwa ana uwezo mzuri kama wa Shafi katika kuandika.
 
Nilipenda sana vitabu vya Adam Shafi; kuna kimoja kilikuwa kinaitwa Kuli kilinisismua sana miaka hiyo ya sabini. Nadhani katika waandishi wa wakati ule nilipenda sana Faraji HH Katalambula kwenye kitabu chake cha Simu ya Kifo, Adam Shafi kwenye kitabu chake cha Kuli, na Penina Mhando kwenye kitabu chake cha Wakati Ukuta. Kuna vingine nimeshasahau titles zake vilivyokuwa chini ya East African Literature Bureau wakati huo sijui kama bado ipo.
 
Back
Top Bottom