Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

The way you think your right but i now one thing adam na eva hawakuwa wawil tu kwa sabab tunaona mafuv ya kale na hayo yalikuwa ya wap kma walikuwa wawili tyuuu
 
Ukiwa mdadisi sana unaweza umiza kichwa, mfano, mwanzo alikuwapo Adam tu kisha akaja Hawa, wakazaa watoto 2 Abel na Cain, Abel akauliwa na Cain! Baada ya hapo Cain nae akapata watoto! Sasa KAMA HAKUMLALA mama yake, maana yake kulikuwa na mwanamke mwingine mbali na Hawa! Hivyo walikuwapo watu kabla ya hapo.
Nishajiuliza sana hili swali na sikupata jibu nikabaki kuamini kwamba kulikuwa na zaidi ya Adam na Hawa
 
The way you think your right but i now one thing adam na eva hawakuwa wawil tu kwa sabab tunaona mafuv ya kale na hayo yalikuwa ya wap kma walikuwa wawili tyuuu
Mkuu au unataka kusrma Adam na Hawa walikua mbingu ya ulaya na kuna wengine walikua mbingu yetu, hebu ongea katika lugha laini sheikh
 
Kwa kifupi tu biblia ni jipu maana imejaa uongo na ubabaishaji ukihoji wanakuambia omba roho mtakatifu akuongoze ndio utaelewa hii imani ni uchuro tu Duniani ndio maana kila mtu anatumia biblia kuishi ki ujanja ujanja hata shoga anatumia biblia kuhalalisha ushoga wake hiki kitabu kipuuzwe.
 
Watu wengine wanastajabisha, kama hukubali au huamini kuwa Adam na Hawa ndio binadamu wa kwanza!, hebu tueleze wewe unachojua au unachoamini kuhusu hiyo concept yako.
 
Mbona unawatukana waafrika bila sababu? kwani kuamini maandiko matakatifu ni utumwa? mbona waarabu/waislam nao wanaamini kuwa nabii adam ni binadamu wa kwanza? hata hao wazungu waliobobea katika science wanaamini maandiko matakatifu? Heshimu imani za watu
Slave mentality is the worst form of slavery...!!
 
Kwa kifupi tu biblia ni jipu maana imejaa uongo na ubabaishaji ukihoji wanakuambia omba roho mtakatifu akuongoze ndio utaelewa hii imani ni uchuro tu Duniani ndio maana kila mtu anatumia biblia kuishi ki ujanja ujanja hata shoga anatumia biblia kuhalalisha ushoga wake hiki kitabu kipuuzwe.
wew iman za watu hizo km unaona ni ulewi elewi we pita kushoto tu.. sio kuongea unayoyajua ww
 
Kwa kifupi tu biblia ni jipu maana imejaa uongo na ubabaishaji ukihoji wanakuambia omba roho mtakatifu akuongoze ndio utaelewa hii imani ni uchuro tu Duniani ndio maana kila mtu anatumia biblia kuishi ki ujanja ujanja hata shoga anatumia biblia kuhalalisha ushoga wake hiki kitabu kipuuzwe.
unaweza weka andiko linalotumiwa na mashoga ili kuhalalisha ushoga wao tafadhali!......
 
Taratibu....! Kwani uliambiwa Adamu hakuwa na watoto wengine wa kike? Na unajua ni miaka mingapi ilipita tangu Kaini amuue Habili hadi kupata mtoto?

Issue hizi msizozijua sio za kuingia kichwakichwa bila tafakuri ya kina na kuja na majibu yenu tayari tena ya kitoto.
Unadhani kama lengo lingekuwa kudanganya wangeshindwa kupanga uongo ili watu wapuuzi washindwe
Nipe maelezo nikuelewe, mimi nimefikiria hivyo, kama siko sahihi, niweke sahihi. Kwa hiyo Cain na Abel waliwatomba dada zao?? Ebu nipe maelezo! Inaonyesha "unajua" mengi kuhusu hii kitu, ebu tupe ubuyu nasi.
Kama ulichoobgea hapo juu ndo ushahidi wako, basi point yangu iko logical zaidi kuwa eidha kulikuwapo na wanawake wengine au biblia inasapoti INCEST, yaani kulalana na ndugu wa damu iliwamo mama mzazi kama wanyama.
 
Mmmh! naona tunaanza kuhoji uumbaji wa Mungu. tunaweza kuhoji baada ya kifo ni wapi. kama hatuamini kuhusu uumbaji, tujiulize huu ulimwengu ulikuwa wapi, kwa nini kuna ulimwengu, kwa nini tunaishi na mambo kadha wa kadha. Nadhani wakati mwingine tunapaswa kuyakubali mapokeo kwa sababu kama ambavyo hatujui imekuwaje ulimwengu ukawepo na baada ya kifo ni nini, basi tukubali kwamba Adam na Hawa ndio watu wa kwanza kuumbwa.
Hayo maswali ulosema tujiulize, na wewe sasa utusaidie kutafuta majibu. Ndo tunataka majibu maana tuko njia panda, haya mambo ya woga woga wa kuhoji eti tusihoji kuhusu Mungu, ni uendawazimu!
 
Kwa kifupi tu biblia ni jipu maana imejaa uongo na ubabaishaji ukihoji wanakuambia omba roho mtakatifu akuongoze ndio utaelewa hii imani ni uchuro tu Duniani ndio maana kila mtu anatumia biblia kuishi ki ujanja ujanja hata shoga anatumia biblia kuhalalisha ushoga wake hiki kitabu kipuuzwe.
Ndo maana mkuu unaposoma unatakiwa umuombe roho mtakatifu akutangulie la cvyo hautaele tasfiri.

"Wao wanasems"
 
wakuu mie napingana sana na ukweli huu kwani ni UONGO mtupu kwani hawa jamaa ni watu katika watu!
Je UNAMJUA BINADAMU WA KWANZA HAPA DUNIANI! TAFADHALI FUNGUKA!

Sasa mkuu mbona unajipinga mwenyewe?
 
Sasa mkuu mbona unajipinga mwenyewe?
Sijipingi mkuu imani yangu ina amini kwamba zama zakale palikua na watu wengi yaani wazungu wachina wa afrika yaani dunia ilijaa ikajitosheleza kabisa na ndani yake hao tunaowaita adam na hawa walikuepo pia ...na wote hawa walikua hawamjui mungu kabla ya mungu kuwafunulia uwepo wake
..
So baada ya muda aliwajaalia ufahamu adamu na baadae hawa katika kumfahamu na ndipo maandiko yalipo anzia hapo
Hata ukisoma maandiko utaona yanaelezea historia kuwa kulikua na watu zaidi ya adam hapoo kabla
Ndio maana na jenga hoja palikua na watu zaidi ya hawa na adamu kuliko tunavyotafsiri maandiko matakatifu
 
Sijipingi mkuu imani yangu ina amini kwamba zama zakale palikua na watu wengi yaani wazungu wachina wa afrika yaani dunia ilijaa ikajitosheleza kabisa na ndani yake hao tunaowaita adam na hawa walikuepo pia ...na wote hawa walikua hawamjui mungu kabla ya mungu kuwafunulia uwepo wake
..
So baada ya muda aliwajaalia ufahamu adamu na baadae hawa katika kumfahamu na ndipo maandiko yalipo anzia hapo
Hata ukisoma maandiko utaona yanaelezea historia kuwa kulikua na watu zaidi ya adam hapoo kabla
Ndio maana na jenga hoja palikua na watu zaidi ya hawa na adamu kuliko tunavyotafsiri maandiko matakatifu

Ni wapi maandiko yanasema kulikuwa na watu zaidi ya Adam hapo zaman?
 
Ni wapi maandiko yanasema kulikuwa na watu zaidi ya Adam hapo zaman?

Mwanzo 2
1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.

11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;

12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.

13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.

14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.

20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.

21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
 
Mwanzo 4
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.

2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.

3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.

4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani].

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.

17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.

18 Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki.

19 Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.

20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama.

21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi.

22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama.

23 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;

24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.

25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.

26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom