Adam, Musa, Ibrahim, Elia, Yesu, Isaya hawakupewa vitabu

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
1,472
1,828
Mie nitaendelea kulia na Akili zenu Waafrika Mna Akili Ila Akili Timamu bado Hazijakaa sawa

Waafrika tuwe na Akili timamu na Tuwe waamini wa Akili Timamu kweli kweli kupokea Mambo tu Kisa Yanakuja kwetu kutoka Nje tena Na Watu wenye Ndevu nyingi basi Ndio mnawaona Ni wa Kweli hamkai chini kufikiria Kwa Kina Mnajipotosha Sana Nyie

Kuna Baadhi ya Waafrika wanajinadi kabisa Mtume wetu alipewa Kitabu na Mungu na Wengine wapo wanasema Kuna Vitabu viliandikwa na Manabii mfano Vitabu vile Vitatu vya Kwenye Biblia vya Mwanzo. Wakati ukiangalia kwa Umakini na Kuchunguza na Kutumia Akili Timamu utagundua kwamba Vitabu vile si Vya hao Manabii bali ni Watu waliokuwa wanasimulia Kuhusu hao Manabii

Mfano mzuri

Isaya 1:1

Maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na mji wa Yerusalemu, nyakati za utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Mfano wa Pili

Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kila utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja atalipa fidia kwa ajili ya nafsi yake mbele yangu ili pasiwe na maradhi mabaya miongoni mwao wakati wa kuhesabiwa.

Kutoka 30:11‭-‬12

Sasa usikurupuke, chunguza kwa makini Hayo maandiko si ya Isaya wala Musa ila ni Mtu mwingine anasimulia Kuhusu Isaya. Sasa jiulize kwa Makini wewe Mtu mwenye Akili timamu. Kama Uliambiwa Kitabu hiki ni cha Isaya au Cha Musa kwanini Asiandike mwenyewe hayo maneno kwamba Mimi Isaya au mimi Musa niliona Maono haya na Haya ila Anaandika Mtu mwingine kwamba Yeye ndio kayaona Maono ya Isaya. Hivi hiki kitu kinaingia Akilini kweli. Unawezaje kuona Maono ya Mwingine na Ukayaandika!?

Kwanini Musa Asiseme Mimi Musa Nikaambiwa Hivi na Mwenyezi Mungu ila Inaandikwa Musa akaambiwa na Mwenyezi Mungu. Yaani Ni Kama Walikuwa Watu watatu Musa.. MUNGU na. Mwandishi wa Habari

Tukiyaacha Hayo Kuna Baadhi ya Waafrika wana kazana sana kwamba Mtume wao ndio wa Mwisho baada ya Hao Mitume wengine Wa Mungu wao. Je kwa kuangalia kwa Makini Hivi Baba Wa Imani kulingana na Maandiko ya kwenye Vitabu ambaye ni Ibrahim hakuachiwa kitabu cha Muongozo ila Mtume Wao ndio kaachiwa hilo linaingia akili kweli

Mtu ambaye ndie aliyekuwa Baba Wa Imani Hana Kitabu ila Mtu wa Mwisho ndio ana Muongozo wa Kitabu. Manabii na Mitume wote waliotangulia Kabla yake hawana Muongozo ila Wa Mwisho ndio anamuongozo sasa Wale wa Kwanza Walikuwa wanafundishwa nini na Walikuwa wanawafundisha Nini Hao. Wafuasi wao!?

Ndugu zangu Tumevurugwa Akili vya Kutosha. Wazee wetu walivurugwa vya Kutosha na Si Kwamba Walikubali haya Mambo wengine walipata Mateso maana zilikuja Kipindi cha Mateso ya Ukoloni Hata wazee wa Nyerere kina Kambarage walikataa hizi Dini zilizoletwa hawakuzikubali kabisa Na walikufa Bila Kuzikubali hizi dini zilizokuja na Wakoloni. Siyo Baba zake na Babu zake Julius tu bali hata Wazee wako huko Nyuma Hawakuzikubali ila Kutokana Na Kwamba Wapo Chini ya Utawala wa Kibabe na Wakoloni waliamua Kukubali.

Turudi katika Matumizi ya Akili timamu na Tuchambue kila Kinachokuja Kwetu si kukipokea Tu bila Kiufikiria kwanza. Afrika imekuwa sehemu ya Dumpo Place maana Sisi kazi yetu hatuchambui kila Jambo tunapokea tu na Tunalipigia Mpaka Kampeni na Kulilinda Kabisa bila Hata Kujua Undani wake. Nyie hamna. cha Kwenu ndio maana hamjui mfanye nini au mfuate Nini ndio maana mnakubali lolote linalokuja kwenu.

ASANTENI
 
Ndugu yangu rudi kasome upya DINI. Mungu alishusha vitabu vinne kwa manabii na mitume wake wanne.

1. Nabii Mussa ( a.s ) - alipewa Tourati

2. Nabii Dawud ( a.s ) - alipewa Zaburi

3. Nabii Eisa ( Yesu ) - alipewa Injili

4. Mtume Muhammad ( s.a.w ) alipewa - Qur'an

Mwenye - Ezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.
 
Mie nitaendelea kulia na Akili zenu Waafrika Mna Akili Ila Akili Timamu bado Hazijakaa sawa

Waafrika tuwe na Akili timamu na Tuwe waamini wa Akili Timamu kweli kweli kupokea Mambo tu Kisa Yanakuja kwetu kutoka Nje tena Na Watu wenye Ndevu nyingi basi Ndio mnawaona Ni wa Kweli hamkai chini kufikiria Kwa Kina Mnajipotosha Sana Nyie

Kuna Baadhi ya Waafrika wanajinadi kabisa Mtume wetu alipewa Kitabu na Mungu na Wengine wapo wanasema Kuna Vitabu viliandikwa na Manabii mfano Vitabu vile Vitatu vya Kwenye Biblia vya Mwanzo. Wakati ukiangalia kwa Umakini na Kuchunguza na Kutumia Akili Timamu utagundua kwamba Vitabu vile si Vya hao Manabii bali ni Watu waliokuwa wanasimulia Kuhusu hao Manabii
Una nia njema ila unakosea kupakua chakula halafu unawasimanga walaji hata kabla hujakiombea hicho chakula.
  1. Unadhani watakila? Hata wakila unadhani watashiba na kukifurahia?
  2. Wewe ni mtumishi gani usiyekuwa na lugha ya upendo na mvuto kwa wanaojifunza kwako?
 
Ndugu yangu rudi kasome upya DINI. Mungu alishusha vitabu vinne kwa manabii na mitume wake wanne.

1. Nabii Mussa ( a.s ) - alipewa Tourati

2. Nabii Dawud ( a.s ) - alipewa Zaburi

3. Nabii Eisa ( Yesu ) - alipewa Injili

4. Mtume Muhammad ( s.a.w ) alipewa - Qur'an

Mwenye - Ezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.

1. Jambo la Kwanza Ndugu yangu. Mungu alishusha Vitabu hivyo halafu akaacha Kumshushia Binadamu wa Kwanza Kitabu!? Akaacha Kumshushia Ibrahim kitabu. Akaacha Kumshushia Nuhu kitabu. Akaacha kumshushi Elia kitabu au hao si Watu wake Muhimu

2. Halafu kitabu kinashushwaje Halafu Kinasema Mungu akamwmabia Musa au Mungu akamwambia Yesu. Huoni Hapa ni Mwandishi tu ndio anasimulia Msimulizi ambayo hata Yeye hana Uhakika nayo. Kwanini kisiseme Mimi Mungu Nikamwambia Musa ila Kinashushwa Ila Kinamaandishi ya Kujichanganya Tena

Wewe Unajionyesha Wazi kabisa Umekariri tu Mambo hayo Yamekuja Kwako ukayameza kama Yalivyo
 
Una nia njema ila unakosea kupakua chakula halafu unawasimanga walaji hata kabla hujakiombea hicho chakula.
  1. Unadhani watakila? Hata wakila unadhani watashiba na kukifurahia?
  2. Wewe ni mtumishi gani usiyekuwa na lugha ya upendo na mvuto kwa wanaojifunza kwako?
Sijasimanga Mtu nimesema Watu watumie Akili zao Timamu si Kupokea Mapokeo tu Bila Kuyatafakari kwa Kina.

Unaambiwa kitabu ni cha Musa ila Huyo Musa Siyo Yeye tena Aliyeandika kumbe ni Mtu mwingine amesimulia. Hicho kitabu kina Uhalali gani wa Kuitwa kitabu cha Musa
 
Naona watu kidogo mnaanza Toka mapangoni walikoficha Akili zenu,taratibu Tutaelewana tu,

Huu Ndio muda wa Mwafrika kuamka na kufunguka Akili tumechezewa sana Akili na hekaya za wayahudi na Waarabu wa middle east!
 
Waafrika tumebeba vitu vingi sana kichwani ndo maana maisha yetu yamekua magumu sana, tungefokasi kwenye elimu dunia pengine tungeshaunda nyuklia yetu na sisi. Elimu dunia pekee ndo tunaruhusiwa kuhoji na kuchallenge kila jambo. Lkn hii elimu ya dini ukihoji wanakuambia una upungufu wa imani, mara uambiwe unakufuru ili mradi ukate tamaa. In short dini haitaki utafiti, inataka upokee na kumeza yaliyoandikwa kwenye vitabu vyao hata kama vina ukakasi
 
1. Jambo la Kwanza Ndugu yangu. Mungu alishusha Vitabu hivyo halafu akaacha Kumshushia Binadamu wa Kwanza Kitabu!? Akaacha Kumshushia Ibrahim kitabu. Akaacha Kumshushia Nuhu kitabu. Akaacha kumshushi Elia kitabu au hao si Watu wake Muhimu

2. Halafu kitabu kinashushwaje Halafu Kinasema Mungu akamwmabia Musa au Mungu akamwambia Yesu. Huoni Hapa ni Mwandishi tu ndio anasimulia Msimulizi ambayo hata Yeye hana Uhakika nayo. Kwanini kisiseme Mimi Mungu Nikamwambia Musa ila Kinashushwa Ila Kinamaandishi ya Kujichanganya Tena

Wewe Unajionyesha Wazi kabisa Umekariri tu Mambo hayo Yamekuja Kwako ukayameza kama Yalivyo
Vitabu vingi isipokuwa Qur'an vimefanyiwa editing, binadamu katia mawazo na matamanio yake.

Mwenye Ezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.
 
Ibrahim alishushiwa maelekezo machache yaliyonakiliwa kwenye page chache ( karatasi za kipindi hiko)
 
Semea mani yako,
Hii nyingine huijui na hata ukifundishwa hutakubali na matokeo yake utaleta ubishi na kuudhi imani ya watu,
Usikosoe kitabu cha dini isiyo yako wasije wakakosoa yako ukazusha ugomvi unaoweza kuepukwa
Unaweza kudai kwamba huna dini lakini huko kutokuwa na dini ndiyo dini yako hiyo
 
Nauliza huyu Musa Richard Mwacha ni nani?

Au tukawaulize Benjamin Mkapa na Muhimbili national hospital?
 
Kuna uhusiano wowote kati ya manabii na mitume weupe na sisi tuliotokea kolelo?
Inawezekana hata miungu yetu ni tofauti!
 
Back
Top Bottom