Adam Kimbisa ndio alikuwa mtoa rushwa au wanamsingizia?

Kwa hali ilivyo iko complex sana, nani wa kumfunga paka kengele sasa, TAKUKURU na wengine wanaishia kukimbizana na bahasha ili hali wanajua michezo inavyochezwa. Nashangaa watu wana guts za kusimama na kutoa tuhuma. Tuhuma tu?
 
sasa mwanakijiji unajishushia heshima hapa deni liache siku zoooote bali kulipwa wakati wa kampeni sio? halafu Dodoma wakati huyo Kimbisa si mkazi wa huko, kwa biashara gani anazofanya huko? hivi unajua M-pesa wewe? rushwa imeenda kidigitali sasa huoni hata sumni ikibadilisha mikono bali elctroniki zikifanya kazi! Ukitaka kujua tafuta namba ya Kimbisa au washirika wake halafu jaribu kuangalia uhusiano na namba za Wabunge wa CCM utaona kuna namba common zimelipa saaana madeni kipindi hiki! BTW u went too low ku-support mtu ambaye hajui lolote kuhusu economic blocks!

Wewe, Kimbisa ni mrangi wa Kondoa, sasa sijui kwako Kondoa inapatikana mkoa gn!
 
kimbisa fisadi yake maghorofa tank bovu-mbezi beach moja lina nbc yote mawili ni ya kwake!
 
hata kama alitoa rushwa,mie aliniimpress vya kutosha bungeni...he deserves the title....
 
huyu aliyetuhumu ana matatizo yake; sijawahi kuwa kwenye timu ya mtu yeyote. Kwamba, nilimuendorse Malecela haikuwa na shaka na sikufanya siri.

Mwanakijiji, usijaribu kutoa Majibu Mapesi kwenye hii issue, Acha Kabisa, Hiyo Endorsement yako uliyoifanyia hapa kwa ni very light ukilinganisha na support ambayo BEN alikuwa anampa humu Janvini William, Jinsi William alivyokushukuru ni ushahidi tosha kabisa mmefanya mengi sana nje ya JF wakati wa Mchakato huu, tunaomba ututajie wabunge wa upinzani waliotoa RUSHWA Kama William anawajua na wewe unawajua Lazima, achana na Kimbisa kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ni kweli kimbisa alitoa rushwa na ni mlaji mkubwa wa rushwa ukianzia red cross lakini kuna wale waliotumia nafasi zao kitaasisi ka Shy Rose Banji ile misaada iliyokuwa inatolewa na NMB na yeye akiwepo pale kutokana na nafasi ilikuwa rahisi kujijenga kumbuka rushwa ya kitaasisi siyo lazima pesa itoke mfukoni najua pointi ya mwanakijiji ilikuwa inataka tuizungumzie rushwa kiupana zaidi
 
Adam alihojiwa wiki kadhaa kuhusu tuhuma za rushwa ilikuwa kwenye mojawapo ya vikao vya kujiuza pale jijini Dar; alikanusha na kusema hayo ni maneno ya kisiasa tu na kuwa hakuna wakati ambapo kuna kampeni kama hizi ambapo watu hawatodai kuna rushwa. Lakini siku zilivyokwenda hadi jana jina lake limekuwa likitajwa pembeni kuwa alitumia fedha nyingi!

Watu wanapozungumzia "rushwa" wakati mwingine watu wanasahau kuwa hata baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma na taasisi mbalimbali huwa wamekuwa wakitoa kitu kidogo (si lazima iwe fedha tu, bali pia nafasi, n.k) kwa wabunge ili wazungumze vizuri. Hii ni pamoja na kupeleka miradi kwenye majimbo yao au kuwapa 'shukrani fulani'. Rushwa hizo za kitaasisi mara nyingi hazisikiki sana kwa sababu hazihusiani moja kwa moja na kampeni za kisiasa lakini pia zipo na watoa rushwa wakubwa wa kitaasisi wanajulikana au bora zaidi wanapaswa kujulikana kwani hawana siri!

Lakini la Kimbisa inaonekana kama vile ni "common knowledge" lakini hakuna mtu ambaye ameweza kusema kwa uhakika alimuona Kimbisa akitoa rushwa wapi na akimpa nani! Isije kuwa ni yale yale ambayo mtu mmoja alianzisha rumors kuwa "kimbisa katoa rushwa" na kutoka hapo kila mtu amekuwa akirudia hilo. Kama ni kweli ina maan kuna wabunge kama 210 ambao ni wala rushwa!! yaani 2/3 ya Bunge ni wala rushwa!!!! Hilo linatisha!!

Lakini kama siyo yeye ni kina nani hawa ambao wanadaiwa kutoa rushwa na wamempa nani....

Kama ulitoa rushwa kwenye kampeni ya EALA, kupokea au kumuona mtu akitoa na kupokea na unauhakika kuwa ilikuwa ni rushwa siyo mtu alikuwa "analipa deni fulani!"
Ndio sababu rushwa haitaisha TZ......kinachonishangaza sana ni kwamba...kwanini hizi tuhuma za rushwa zinakuja baada ya matokeo ya ubunge??...tena baada ya watu kushindwa?????....wakati wa kampeni mbona kelele zilipigwa watu wakawa kimya tu????..kwani rushwa inaonekana wakati gani????....mbona wakati wakutoa/kupokea watu hawasemagi??????.....na kuna vyombo kama TAKUKURU vipo?????......kwa mtindo huu kweli rushwa TZ itaisha???....kipi kinamfanya mtu aonekane shujaa kwa jamii.....kutoa taarifa kwa vyombo husika wakati mtu anapokea/kutoa rushwa ili hatimae akamatwe(ready handed)au kupiga kelele baadae wakati rushwa ishatolewa na hata kutumika??
 
Habari za ndani nilizo zipata ni kwamba big name wote kutoka CCM walitoa rushwa, wachache sana waliokwenda wenyewe bila kutumia nguvu ya mfuko na ndio hao waliishia kupata kura kidogo

Jina la Kimbisa linatajwa zaidi kwasababu ya makeke na mbwembwe zake, ni mtaalam wa fitna tofauti na akina Malecela waliokwenda kichwa kichwa kwa kupumbazwa na wapambe
 
Back
Top Bottom