Adam Kimbisa ndio alikuwa mtoa rushwa au wanamsingizia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adam Kimbisa ndio alikuwa mtoa rushwa au wanamsingizia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 18, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Adam alihojiwa wiki kadhaa kuhusu tuhuma za rushwa ilikuwa kwenye mojawapo ya vikao vya kujiuza pale jijini Dar; alikanusha na kusema hayo ni maneno ya kisiasa tu na kuwa hakuna wakati ambapo kuna kampeni kama hizi ambapo watu hawatodai kuna rushwa. Lakini siku zilivyokwenda hadi jana jina lake limekuwa likitajwa pembeni kuwa alitumia fedha nyingi!

  Watu wanapozungumzia "rushwa" wakati mwingine watu wanasahau kuwa hata baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma na taasisi mbalimbali huwa wamekuwa wakitoa kitu kidogo (si lazima iwe fedha tu, bali pia nafasi, n.k) kwa wabunge ili wazungumze vizuri. Hii ni pamoja na kupeleka miradi kwenye majimbo yao au kuwapa 'shukrani fulani'. Rushwa hizo za kitaasisi mara nyingi hazisikiki sana kwa sababu hazihusiani moja kwa moja na kampeni za kisiasa lakini pia zipo na watoa rushwa wakubwa wa kitaasisi wanajulikana au bora zaidi wanapaswa kujulikana kwani hawana siri!

  Lakini la Kimbisa inaonekana kama vile ni "common knowledge" lakini hakuna mtu ambaye ameweza kusema kwa uhakika alimuona Kimbisa akitoa rushwa wapi na akimpa nani! Isije kuwa ni yale yale ambayo mtu mmoja alianzisha rumors kuwa "kimbisa katoa rushwa" na kutoka hapo kila mtu amekuwa akirudia hilo. Kama ni kweli ina maan kuna wabunge kama 210 ambao ni wala rushwa!! yaani 2/3 ya Bunge ni wala rushwa!!!! Hilo linatisha!!

  Lakini kama siyo yeye ni kina nani hawa ambao wanadaiwa kutoa rushwa na wamempa nani....

  Kama ulitoa rushwa kwenye kampeni ya EALA, kupokea au kumuona mtu akitoa na kupokea na unauhakika kuwa ilikuwa ni rushwa siyo mtu alikuwa "analipa deni fulani!"
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Na W. Malecela atakuwepo kwenye ilo kundi au unasemaje?
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,020
  Trophy Points: 280
  sasa mwanakijiji unajishushia heshima hapa deni liache siku zoooote bali kulipwa wakati wa kampeni sio? halafu Dodoma wakati huyo Kimbisa si mkazi wa huko, kwa biashara gani anazofanya huko? hivi unajua M-pesa wewe? rushwa imeenda kidigitali sasa huoni hata sumni ikibadilisha mikono bali elctroniki zikifanya kazi! Ukitaka kujua tafuta namba ya Kimbisa au washirika wake halafu jaribu kuangalia uhusiano na namba za Wabunge wa CCM utaona kuna namba common zimelipa saaana madeni kipindi hiki! BTW u went too low ku-support mtu ambaye hajui lolote kuhusu economic blocks!
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji wameku rusha nini cha juu chako, maana wewe nasikia unavutaga kubwa kupita wengi ...

  Halafu unaanza kuandika vi-essay zako hapa kuwatetea hasa wale wenye majina ya upande wako???

  Wamekupa dau ndogo nini mbona kelele mapema (mkirushana ndio sisi wanyonge mnatuambia HA!)
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  juhudi zako zimesaidia kijana kupata kura 42!!!!

  hizo tuhuma za rushwa binafsi sizijui...
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwenye thread yake jana William alisema

  Kwenye thread yake ya leo amesema baadhi ya wabunge upinzani nao wanapokea rushwa

  Kwa maana hiyo anawajua hao wabunge waliopokea rushwa lakini hajawataja. Kwa vile nyie mlikuwa nae kwenye kampeni si mtakuwa mnawajua hapo wabunge wala rushwa? William hajawapatia majina ya hao wabunge wa upinzani waliopokea rushwa? Kwa maana nyingine na nyie through Willima mlikuwa mnajua kuna wabunge wanadai rushwa lakini mkaamua kukaa kimya mpaka baada ya uchaguzi kumalizika?
   
 7. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, kwa kuanzia umekuwa implicated kuwa ulikuwa kwenye timu ya kampeni ya W.J Malecela, na yeye mwenyewe kasema hayo na papo hapo akaja na shutuma za Wapinzani kujihusisha na rushwa, sasa ukiwa kama mwana timu wa kampeni nadhani utakuwa na inside info, ebu unaweza ku elaborate?
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  interesting..........
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Inasemekana Bernard Murunya alitumia takriban mil 20 kusaka kura
   
 10. D

  Deo JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,191
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  MMK hii arithmetic ni simple. Ni wabunge gani walipata ubunge kwa njia ya rushwa? Je kama yeye alipata kwa rushwa si ni rahisi zaidi yeye kupokea rushwa?

  Baba wa Taifa alisema "rushwa ya tanzania haina aibu" hii ni wakati ule, sasa imekuwa kuwa ya kitaasisi na walarushwa wameshika hatamu ya nchi hii katika nyanja zote.

  Iwapo chama chetu tawala ni kinara wa kuvunja sheria, kutoa na kupokea rushwa za aina zote, waongo waliokubuhu, wabaguzi wa kila hali na wauaji wa raia wake unategemea nini mkuu wangu?

  Je tutafika?
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  It is very possible...historia yake inamhukumu; 2010 alimwaga pesa nyingi sana kwenye mbio za ubunge Dodoma, pia katika chama chake rushwa ni utaratibu, jana confidence yake illikua ya ajabu sana na zaidi alisema ana kila kitu kinachotakiwa kushinda hiyo nafasi including "TECHNICAL KNOW WHO"...
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Umeona hiyo link kati ya mwanakijiji na rushwa??

  Inaonekana dau lake leo limekuwa dogo au wamerushwa?

  Sasa wanakuja kujivua nguo hapa
   
 13. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kimbisa alikuwa kichwa sana kama katumia na rushwa pia basi ana vipaji viwili
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna msomo Misri...wanasema Misri itakufa siku bakhsishi ikifa.....
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Well hao TAKUKURU si wanaweza kuangalia hizo namba? hiyo bold.... ningekuwa napanga kwenda vitani nisingeenda na wewe!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  huyu aliyetuhumu ana matatizo yake; sijawahi kuwa kwenye timu ya mtu yeyote. Kwamba, nilimuendorse Malecela haikuwa na shaka na sikufanya siri.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wangeanza na wewe? ulipewa ngapi na william?

  Ulirushwa au kipi kimetokea this time; maana ukilipwa vema uantokwa na mapofu kuwatetea fulltime..nasubiria who is next kumtetea..
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Ili ni dau la kugombea udiwani CCM, usiwashushe hadhi wabunge wa CCM kiasi hiki.

  Jelly Silaa ili achaguliwe kuwa Meya wa Ilala kila Diwani alipewa rushwa ya shilling laki tano na wale wabishi walipewa viToyota Collola.

  Williama amepata hasara kubwa ni swala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi, halafu jambo la ajabu zaidi William alikuwa anawategemea watu wa Chadema zaidi kushinda kuliko CCM.

  Fedha fezea mpaka Masanilo etu naye leo anamuunga mkono Le Mutus Baharia!!.....ukweli utajulikana tu huyu jamaa aliwekeza kiasi gani kuununuwa huo Ubunge, just stay tune jukwaa la Siasa.
   
 19. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ok, haina shaka maana jinsi alivyoiweka kwenye ile thread yake baada ya kushindwa ilionyesha kama wewe na Invisible mlikuwa watu wa ndani jikoni kwe campaign team. Thank you for clarifying maana moyo ulivunjika kidogo.
  Back to the topic...
   
 20. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  .
  ........ very!

  .
   
Loading...