Adam Chagulani: Upinzani wa Tanzania ni dhaifu

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
CCM ni nyumba mbovu inavuja wananchi wanakwepa matone ndani ya nyumba hawana cha kufanya ,ila kinachowapa shaka ni upinzani wetu wao siyo nyumba mbovu ila ni chini ya mti hakuna cha kukwepa matone lazima uloane.

Kiukweli mambo yanayoleta tofauti ndani ya upinzani wetu ni ya kijinga sana na ndiyo huleta tafrani na kuwakatisha tamaa wananchi wanafikia pahala bora tuendelee kukwepa matone ndani ya jumba bovu CCM, kuliko kwenda kukaa chini ya mti kuloana.

Ukiangalia hata Miungano iliyofikiwa huko nyuma iliishia kuvunjika kutokana na maslahi binafsi ya vyama , nakumbuka kulikuwa na UDETA umoja Wa demokrasia Tanzania ulivunjika kipindi cha uchaguzi Mdogo Bihalamulo baada ya kufariki mbunge Wa TLP ndugu Faresi Kabuye Mrema aliomba kwa kuwa mbunge aliyefariki ni wake ,kilichotokea vyama washirika Wa UDETA walikataa na kila chama kutaka kusimamisha mgombea matokeo yake CCM walishinda hawakushinda sababu ya kupendwa ila sababu ya ujinga, ubinafsi,ujuaji Wa upinzani.

Tukirejea kwenye uchaguzi mwaka 2015 kama kungekuwa na ushirikiano thabiti usio na unafiki,visasi, Leo Julius S. Mtatiro angekuwa mbunge Wa segerea angekuwa mbunge kutokana na washirika Wa UKAWA kutokuheshimu makubaliano walisimamisha wagombea kwenye jimbo hili nakurahisisha ushindi Wa CCM ,mifano iko mingi kila kona ya nchi hii ndiyo maana watu kama Profesa Lipumba wanapata watu kuwaunga mkono kutokana kuiona UKAWA kama chanzo cha wao kukosa fursa ya kuwa viongozi huu ni ukweli ingawa unaweza kuwa mchungu.

upinzani huungana kwenye mambo mengine ikifika ishu ya uwakilishi na fursa za kiuongozi kila mmoja huwa na shaka na mwenzie hapo huanza kusikia maneno kama anatumika ,mamluki siyo mpinzani huibuka ukiangalia chaguzi ndogo zilizopita kama vyama vya upinzni vingekuwa na ushirikiano wenye Uadilifu, ukweli, usiona ubinafsi,,ujuaji Leo upinzani wangeibuka videdea kwa baadhi ya Kata na majimbo lakini kilichotokea kila mmoja anakijua.

Leo kuna uchaguzi Wa Bunge la EALA ,(bunge LA Afrika mashariki) vyama ambavyo hapo nyuma viliungana kutetea ukandamizaji Wa Demokrasia ,imetokea fursa ya uongozi kutoa viongozi wanapigna vita wanashambuliana hadharani na kutoleana matamshi makali yanayotishia hata ustawi kidogo Wa kuona kuna haja ya ushirikiano, wameanza kutengeneza nyufa upya Kisa nafasi za Ubunge Wa Afrika mashariki, upinzni tunatakiwa kuangalia maalahi mapana ya Taifa letubkuliko maslahi ya vyama vyetu.

Bila ushirikiano Wa Maana chaguzi zijazo tutaendelea kusogeza siku mbele kwamba tutashinda uhaguzi ujao. Kila mmoja anajua kuwa bila Kuunganisha nguvu kwa dhati hakuna chama cha kujinasibu kinaweza kufanya hivyo Upinzani Wa dhati na wenye Maono ndiyo utaivusha nchi hii kuipeleka kanani ya kweli ,Tuwaite kina Chipaka na Tadea, kina Rungwe na Chauma,UDP, UMD ,ADC ,ACT ,CUF, CDM,Jahazi Asilia tumalize tofauti zetu ,yanayotuuunganisha ni mengi kuliko yanayotutenganisha . watanzania wako tayari tatizo ni sisi kuwapekela kwenye mbadala wa UHAKIKA.

Ndimi Chagulani Adams
 
wewe si ndio Diwani msaliti wa CDM igoma mwanza au majina yanafanana, kama ni wewe kwa taarifa yako watu kama nyie ndio mnaturudisha nyuma kuiondoa CCM mana ulipewa udiwani ukataka na ubunge hapo hapo na ukalewa madaraka ya udiwani , upinzani upo mzuri lakini watu wa dizaini kama wewe ndio mnatuangusha wapenda madaraka na vyeo vya haraka haraka.
 
wewe si ndio Diwani msaliti wa CDM igoma mwanza au majina yanafanana, kama ni wewe kwa taarifa yako watu kama nyie ndio mnaturudisha nyuma kuiondoa CCM mana ulipewa udiwani ukataka na ubunge hapo hapo na ukalewa madaraka ya udiwani , upinzani upo mzuri lakini watu wa dizaini kama wewe ndio mnatuangusha wapenda madaraka na vyeo vya haraka haraka.
Hata mimi nimeshtuka chagulani huyu huyu nayemjua leo hii kawa supporter wa upinzani alioshiriki kuua mwanza??? kaz kwelikweli.

Anyway umoja unahitajika kwenye upinzani ila nashangaa mtoa mada anang'ang'ania jimbo la mtatiro anasahau success ya CUF bara baada ya kutoka majimbo 2 mpaka kufika 10!! hilo halioni kma ni faida ila anaangalia changamoto ya jimbo moja tu!!! kma huyu naye yupo chadema bado then tuna safari ndefu sana ya kufkia mageuzi ya kweli
 
Huyu msaliti alishiriki mpaka kumn'ngoa meya wa jiji la Mwanza kupitia chama chake CHADEMA kwa kushirikiana na madiwani maccm!
 
Adam Chagulani hili jina sio geni... Wakati naanza form one Edmund Rice miaka hiyo nakumbuka hili jina nilikuwa naliskia.. Ameshakuwa kiongozi mkubwa kumbe..
 
Mataahira nao WAPOO! Wanafiki nao WAPOO! Wasaliti wa Watanzania na Tanzania pia WAPOO! Waganga njaa na wachumia tumbo nao WAPOO na hata mapunguani akina Chagulani Adams pia WAPOO

 
Nini maana ya ukawa kama tu ubunge east africa kila chama cha upinzani kimeweka watu wake. Si wangekaa pamoja na kuelewana watu wa kuwaweka. Umoja ni nguvu
 
Ni mtu mjinga tu ndio anayeshindwa kubashiri ya huko mbele.

Kiuhalisia, upinzani unakwenda kupotezwa jumla. Hadi 2020 tunaingia kwenye uchaguzi wapinzani wengi wa mda mrefu hawataingiza timu uwanjani.

Viongozi wa upinzani walijitoa maisha yao kwa ajiri ya kusaidia na kuokoa maisha ya wengi lakini kinachoonekana ni kwamba watanzania bado hawajawa tayari hivyo ningekuwa mimi kiongozi ningetangaza rasmi kuachana na siasa za kipinzani na baadala yake nisingejiunga na chama chochote na kuwaambia watanzania tuishi bila upinzani kwa miaka kadhaa ili tuone kwanza faida yake halafu baada ya hapo tuje tufanye tafakuri iliyosahihi.
 
Siasa za tanzania nilisha acha kushabikia tangu miaka mingi sana hii ilitokana na sababu ambazo mimi niliziona ni za muhimu ikiwa ni pamoja na figisu figisu nyingi
 
Hivi ndiyo ilivyokuwa katika serikali ya Mobutu. Chama chake ndiyo kulikuwa chama tawala na viongozi wa upinzani walinunuliwa kwa pesa au hongo ya vyeo serikalini.

Aliamini usemi wa 'keep ur friends close and ur enemies even closer'.

Wananchi walivaa vitenge vyenye picha ya Mobutu.
 
Ibaki ccm kwani ndivyo wanataka na bora iwe hivyo ili wawe huru maana kila siku hawalali wakiihofia upinzani utadhani chadema ni nchi nyingine waache tu na naoma ujamaa unarudi
 
Serikali zinazokandamiza upinzani zinaongozwa na madiktekta na Mara nyingi mwisho wao huwa ni wa aibu.
 
Uchaguzi mdogo wa marudio (madiwani) umethibitisha wazi kabisa kuwa mpaka sasa CCM bila nguvu ya dola haiwezi kushinda popote. Na hicho ni kimoja tu kinachoiweka CCM pale ilipo, ila dola sio mashine ni watu ambao kuna wakati wanachoka (kama Zimbabwe)... Wakati huo historia itabadilika. Nguvu iliyotumika kwenye udiwani ilikuwa ya nini wakati upinzani Tanzania unakufa? Ina maana uzalendo wa Mh. Magu hautoshi kuipa ushindi CCM? CCM mpya inayoimbwa kila siku ndio hii ya kutoa mawakala wa vyama vingine nje wabaki wao?.... Ni upinzani unakufa au CCM inakufa?.
 
Back
Top Bottom