Adaiwa kumuua mwanawe kwa kumtupa chooni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adaiwa kumuua mwanawe kwa kumtupa chooni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 18, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MKAZI wa Ukonga mkoani Dar es Salaam, Zahara Abubakari (18) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini humo akikabiliwa na mashitaka ya kumuua mtoto wake kwa kumtumbukiza chooni.

  Zahara alifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kinyage.

  Wakili wa Serikali, Neema Haule alidai kuwa Oktoba 9, mwaka huu saa moja jioni katika eneo la Ukonga Madafu, Zahara alisababisha kifo cha mtoto wake mwenye siku 10 kwa kumtumbukiza chooni.

  Mshitakiwa hakutakiwa kujibu mashitaka kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa Mahakama Kuu na mshitakiwa alirudishwa rumande.

  Kesi itatajwa tena Oktoba 31, mwaka huu baada ya upande huo wa mashitaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

  Katika hatua nyingine, Christopher Michael (25) na Maulid Hassan (18) wamefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

  Mwendesha Mashitaka Mkuu, Naima Mwanga alidai mbele ya Hakimu Karim Mushi kuwa, Septemba 9, mwaka huu katika eneo la Mchikichini, washitakiwa hao walikutwa wakiwa na paketi 90 za mihadarati hiyo.

  Washitakiwa walikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Oktoba 23, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmh! huyu mwanamke katili yani kalea mimba mpaka kazaa halafu unatumbukiza mwanao chooni.
   
Loading...