Adaiwa kumuua mtoto wake na kumzika

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
MKAZI wa Kijiji cha Sekedidi, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, Lucia Mahazi (42), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kiume wa siku mbili na kisha kumzika, kwa madai ya kutelekezwa na mwanamume aliyempa ujauzito.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Mei 26, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni.

Alisema wananchi wa eneo hilo waligundua kuwa mwananke huyo hakuwa na mtoto aliyejifungua Aprili 17, mwaka huu na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo lilianza kumchunguza na kubaini mtoto huyo alishauawa na mama yake.

"Uchunguzi wa awali ulibaini mama huyo alijifungua mtoto huyo April 17 na kumuua April 19, na kisha kumzika mwenyewe katika eneo la shule ya msingi Ididi wilayani Kishapu, majira ya saa 12 jioni wakati mvua kubwa ikinyesha ili watu wasimuone," alisema Magiligimba.

"Mabaki ya mwili wa marehemu tumeyatoa Mei 26, kaburini na yamekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi, na mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi," aliongeza.

Vile vile, alisema chanzo cha mauaji ya mtoto huyo, ni mtuhumiwa kudai alikabiliwa na ugumu wa maisha, baada ya mwanaume aliyempatia ujauzito kumtelekeza.


Chanzo: Nipashe
 
Hamna tatizo hapo polisi wamuache aende zake ni bora amempoteza kuliko kumleta kwenye dunia ya mateso yasiyokwisha
 
Vile vile, alisema chanzo cha mauaji ya mtoto huyo, ni mtuhumiwa kudai alikabiliwa na ugumu wa maisha, baada ya mwanaume aliyempatia ujauzito kumtelekeza.

Jr
 
Hapana huo ni uamuzi mgumu na wa kikatili yani unaua mtoto anakulilia mpk anakauka unamuona kweli?????? aaaaghhhh
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kweli Dunia haishi vitendo vya ajabu. Mwingene huku hataki kupokea mahitaji ya mtoto kutoka kwa baba wa mtoto

Huyu anatamani angepata matunzo ya mtoto wake.hatari Sana .
Angemtelekeza tu kuliko kumkatisha uhai .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini alitomb@n@ kavukavu kama mwanaume alikuwa haeleweki?
Vaa kondomu kwa kila tendo hasa unapopiga gemu na wanaume wasela mafii.
 
Hamna tatizo hapo polisi wamuache aende zake ni bora amempoteza kuliko kumleta kwenye dunia ya mateso yasiyokwisha
Tatizo ni huyo mama na mtazamo wake juu ya maisha.

Hivi unadhani huyo mama baada ya kuona maisha yake ni magumu na hawezi kumuudumia huyo mtoto, angeamua kujiua na kumuacha huyo mtoto, baada ya watu kujua amejiua na kuacha mtoto nini kingetokea kwa mtoto?

Je na yeye angeuliwa eti kwa sababu mama yake kajiua?

Au angeuliwa eti kwa sababu baba yake kamtelekeza?

Na wangapi wanaishi bila ya wazazi?

Tatizo huyo mama alijiona yeye ndiye uhai wa huyo mtoto, na hajui ya kuwa Mungu ndiye anayetoa riziki na sisi wanaadamu ni asbabu tu.
 
Back
Top Bottom