Adaiwa kukamatwa kwa kuweka picha za "kudhalilisha" jimbo la Ndugai mtandaoni

TAARIFA

Baada ya kusambaa picha zimionyesha vyoo chakavu na madarasa yenye msongamano wa wanafunzi kamanda wetu Farance The Digital alipata vitisho kutoka kwa Mbunge wa Kongwa Job Ndugai ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania kuwa "anachokitafuta atakipata hivi karibuni kwasababu amekuwa akimwaandama kuanzia asubuhi hadi jioni".

Baadae mji wa #Kibaigwa zilisambaa taarifa za France The Digital kutafutwa hivyo alihama nyumbani kwa sababu za usalama wake,akiwa mafichoni alipata taarifa za nyumba yake kuvamiwa na askari polisi wa #Kongwa wakimtafuta bila mafanikio.....baadae walipigia simu ya wito wa kuripoti kituo cha polisi Kongwa jambo ambalo amelitekeleza leo J4.

Baada ya maohojiano kituo cha polisi kongwa wamemweleza kamanda France The Digital kuwa kosa lake ni kumkashifu Mh Job Ndugai hivyo wanamwamishia Mkoani Dodoma kwa RCO kwaajili ya mahojiano zaidi na wamemwambia hakuna dhamana.

Hivyo makamanda tuendelee kupaza sauti dhidi ya kamanda mwenzetu huyu wa Kibaigwa ili haki iweze kutendeka.

Tusambaze kwenye magroup na zile picha za vyuo na shule ya Karume jimboni Kongwa.

Na Peter Chagga Jr.View attachment 1049158View attachment 1049159View attachment 1049160
Lugoba sekondari watoto wanalala wawili kitanda kimoja,wanawapa waalimu 1000 ili wawafundishe topic
 
Watanzania suluhisho la haya matatizo ni kuitoa CCM, Lasivyo mtabaki kulalamika miaka yote, Miaka zaidi ya 50 CCM imeshadhihirisha kwamba imeshindwa kutatua shida za wananchi, matokeo yake viongozi wameamua kujilimbikizia mali wao na familia zao.

Cha msingi tuweni na uthubutu wa kuwatoa hawa na kuweka wengine nao tukiona hawafi tunawatoa na kuweka wengine pia.....Hapa inabidi watu tuingie mtaani tupiganie katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.....Tukufanikiwa hapo tutakuwa katka steji nzuri ya kutoa huu utawala wa kinyonyaji...Nchi nyingine wameweza kwann sisi tushindwe??? TUACHE KUWA MABWEGE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nataka wale jamaa wa ndio mzee niskie wanasema nini kuhusiana na hili tukio.

Viongozi wetu wanatuangusha sana,aibu aibu kabisa
 
Kwahiyo mkubwa hataki watu wapate habari hii?wakati ni msaada kwake kwa kutotembelea jimbo lake!.
Hii ndiyo misaada ambayo watu wanatakiwa waupe umma ili kupata manufaa.
 
Huyo Boot Licker hana lolote la maana, yeye ni kutii maagizo tu kwa kunyanyasa wapinzani. He's a poor excuse for a Speaker.
 
Back
Top Bottom