Adaiwa kujinyonga kukwepa usumbufu wa michango ya maendeleo kijijini

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
428
996
ajinyonga-pic.jpg

Maandalizi ya mazishi ya Sophia Mohamed (40) mkazi wa Kijiji cha Kipereza Kiteto akidaiwa kujinyonga kukwepa usumbufu wa michango sambamba na mimea yake kuathiriwa na jua. Picha na Mohamed Hamad.

Kiteto. Mkazi wa Kijiji cha Kiperesa wilayani Mkoa wa Manyara, Sophia Mohamed (40) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mtandio wake akiwa kwake ikidaiwa kukwepa michango ya maendeleo sambamba na mazao yake shambani kukauka kutokana na uchache wa mvua za mwaka huu.

Wakiwa katika maandalizi ya mazishi leo Machi 2023, baadhi ya majirani zake wameeleza sababu za Sophia kuamua kujinyonga kuwa ni usumbufu wa michango mbalimbali ya maendeleo anaopata wakati mimea yake shambani kuathiriwa na ukame.

"Huyu mama mazao yake shambani yamekauka na kila mara askari migambo wamekuwa wakipitapita kudai michango kwa ajili ya maendeleo, lakini sababu kubwa ni njaa mahindi yamekauka shambani na inawezekana ndio tatizo," alisema Mohamed Issa mwananchi Kijiji cha Kiperesa.

"Hapa kijijini suala la michango limekuwa tatizo na kama huna fedha, unakamatwa na kufungiwa ofisini. Askari migambo wanazunguka kutwa kukamata watu, vijana wengi sasa wameamua kutoroka kijijini hali ni ngumu, hii ndio iliyofanya hata mwenzetu huyu kujinyonga," amesema.

Ndugu wa marehemu wamezungumzia namna tukio hilo lilivyotokea wakisema ndugu yao huyo hakuwa mgonjwa kivile bali kafanya maamuzi hayo akijua kinachomsibu.

"Nilifika kwake na kukuta mlango umeegeshwa na nilipopiga hodi hakuitika na kusukuma ndani nikauliza mtoto na baadaye nikamwingiza kwa dirishani afungue mlango na alipofungua mlango tukamkuta mdogo wangu kajinyonga," amesema Iddi Mohamed kaka wa marehemu.

Menyekiti wa Kijiji cha Kiperesa, Omari Husein Mrekwa amezungumzia michango hiyo, huku Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa a Manyara, RPC George Katabazi akithibitisha tukio hilo na kuonya wenye tabia za kujinyonga kuacha mara moja.

Credit: Mwananchi
 
Hatari sana. Kwani walihitaji kufanya maendeleo gani?Shule,zahanati,barabara,daraja au ni kipi hasa?Na mchango wenyewe "dola" ngapi za Tanzania?Kama ni kweli,inasikitisha huku inatisha.Umasikini huu.
 
Nimezaliwa kijijini, Nayajua maisha ya vijijini, wazazi wangu waliwahi kujificha porini kisa kodi ya mendeleo kipindi kile ilikuwa shilingi ishirini nadhani kipindi cha Nyerere.

Watu walikuwa wanakuja usiku wanapiga watu ovyo wazazi wanadhalilika mbele ya watoto wao kwa kuwashurutisha walipe Kodi.

Nakumbuka ndani ya siku nne sikuwaona wazazi wangu nyumbani hata wazazi wa wenzangu pia.
Kisa ni TSH 20 za kitanzania.

I hate poverty
 
Back
Top Bottom