Adaiwa kufa kwa kunywa 'Viagra' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adaiwa kufa kwa kunywa 'Viagra'

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MJI wa Arusha mwishoni mwa wiki ulizizima baada ya kutokea habari za kifo cha kutatanisha cha mkazi wa Levolosi, Omari Salim, 44, aliyefariki dunia wakati akipelekwa Hosptali ya Mt Meru baada ya kuzidiwa akiwa nyumba ya wageni na mpenzi wake.

  Tayari Jeshi la Polisi mjini hapa limeshathibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililoibua maswali mengi kwa wakazi wa mjini hapa. Polisi imedai uchunguzi wa awali umebaini kifo cha marehemu huyo kimetokana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume.

  Polisi imezitaja dawa hizo kuwa ni aina ya Muco zilizokutwa ndani ya chumba alichokodi kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.

  Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Akili Mpwapwa aliiambia Mwananchi kuwa Mei 26 majira ya saa 8;30 Salim alimpigia simu mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Caren Isaack, 20, ili wakutane. Alisema wote kwa pamoja walikubaliana na kwenda kukodi chumba katika nyumba ya kulala wageni ya Rhino.

  Alisema baada ya wapenzi hao kuwasili ndani ya chumba hicho, mpenzi wake alimwambia Salim kuwa wapande kitandani kwa lengo la kufanya mapenzi, lakini marehemu alilalamika kuwa alikuwa akijisikia vibaya na ndipo alipoomba kwenda bafuni kuoga.

  Kwa mujibu wa Mpwapwa, marehemu aliingia bafuni kuoga, lakini ghafla alitoka akiwa ameshika taulo mkononi huku akitetemeka, ndipo mpenzi wake alipopatwa na mshangao.

  Alidai kuwa kadiri muda ulivyokuwa ukienda, ndivyo hali ya Salim ilivyozidi kubadilika na ndipo akaamua kumbeba na kumweka kitandani na baadaye kumfunika shuka, lakini ghafla akaanza kutapika mfululizo.

  Kamanda Mpwapwa alifafanua ya kuwa Caren alilazimika kuomba msaada kwa mlinzi wa siku hiyo ndipo walipofanikiwa kumtoa chumbani na kukodi teksi kumuwahisha hospitalini, lakini akakata roho wakiwa wakiwa njiani.

  Alidai ya kuwa jeshi la polisi lilikuta vidonge mbalimbali vya dawa zinazosadikiwa kuwa ni za kuongeza nguvu za kiume zilizokuwa katika pakiti na kwamba huenda Salim alimeza vidonge hivyo kabla ya kushiriki ngono.

  Kamanda Mpwapwa alisema polisi wanamshikilia Caren kwa uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo

  Adaiwa kufa kwa kunywa 'Viagra'
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  mmh ahha aaahh tee teh teeh teeh!
   
 3. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sijambo la kufurahia hili ndugu..inasikitisha mno
   
 4. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii habari nayo ni tangazo?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana ..
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Masikitiko jamani. Hawa watengenezaji wa hizi dawa ni vipi? Mbona kwa wengi inaonekana zinadhuru au kuna kanunu ambazo watumiaji hawazingatii?? Sasa Umri miaka 44 Vs 20!! Inabidi mashine ichangamke ili kuweza kupambana na chick huyu! Yaani naamaanisha umri sawa na mtoto wake. Ni majonzi ila nalo ni fundisho kwetu wanadamu, maadili yametoweka na adhabu ya Mungu i juu yetu.
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dhambi juu ya dhambi..
  Umetumia hela kutafuta mchuchu..
  Ukatumia hela kukodi chUmba KWA AJILI YA SHUHULI..
  Hela ikatoka kununua Muco ILI KUJIWEKA FITI MWANAUMEEE...
  Hela nyingine IKATOKA ya vocha kuupigia mchuchu ulete mzigo eneo la tukio..
  Hela ikakutoka kwa kuwa Mchuchu umewahisha mzigo kwa kukodi Taxi.....
  Hela ya kinywaji na nyama choma au supu..
  Hela ikatumika kutafuta zana za kujilinda na janga hili hatari...
  Uenda ukatoa hela kwa ajili ya kulipia huduma ya mchuchu...

  Na hela ndo imekupeleka.........mungu ampe rehema.
   
 8. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Too sad... Hapo jamaa ana familia yake, labda ana mke wa maana tu na watoto... dah, aibu!!
   
Loading...