Adai Milioni 800 baada ya kupasuliwa kichwa badala ya mguu

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,335
17,839
Mwanamchi 03/09/11,

Kijana Emanuel Didas Marshai (24), ambaye madaktari walikosea na kumfanyia upasuaji wa kichwa badala ya mguu wa kulia, anakamilisha mchakato wa kuishtaki Serikali na kuidai fidia ya Shilingi milioni 800.

Kwa sasa mgonjwa huyo ambaye alifanyiwa upasuaji huo Novemba Mosi, 2008 na madaktari bingwa wa Kitengo cha Mifupa (MOI) cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, amepooza upande wa kulia wa mwili wake.

Wakili wake, Cornelius Kariwa alisema jana kwamba mchakato huo umeanza ikiwa ni pamoja na kuwasilisha maombi mahakamani ili ateuliwe mtu atakayesimamia haki zake kisheria,*“Tunachofanya sasa ni kufungua maombi ili tupate power of attorney (nguvu ya kisheria) ya mtu atakayesimamia haki zake kwa sababu kwa sasa haongei na hana uamuzi,” alisema.
 
mbona hii habari ilishaletwa humu jamvini?nini kipya kilichojiri?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Pole sana emmanuel,kila la heri kati katika kufuatilia haki zako.
Sasa kama haongei kiasi hicho amekitaje lini,au alijua mapema atapooza akatamka mapema?.
 
Mwanamchi 03/09/11,

Kijana Emanuel Didas Marshai (24), ambaye madaktari walikosea na kumfanyia upasuaji wa kichwa badala ya mguu wa kulia, anakamilisha mchakato wa kuishtaki Serikali na kuidai fidia ya Shilingi milioni 800.

Kwa sasa mgonjwa huyo ambaye alifanyiwa upasuaji huo Novemba Mosi, 2008 na madaktari bingwa wa Kitengo cha Mifupa (MOI) cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, amepooza upande wa kulia wa mwili wake.

Wakili wake, Cornelius Kariwa alisema jana kwamba mchakato huo umeanza ikiwa ni pamoja na kuwasilisha maombi mahakamani ili ateuliwe mtu atakayesimamia haki zake kisheria,*“Tunachofanya sasa ni kufungua maombi ili tupate power of attorney (nguvu ya kisheria) ya mtu atakayesimamia haki zake kwa sababu kwa sasa haongei na hana uamuzi,” alisema.

Dah!madaktari wetu bwana ni kituko kweli
 
Sasa kwa nini akina Helen Kijjo Bisimba wa LHRC na Ananilea Nkya wasiingilie kati haki za mgonjwa Emmanuel? Au walikuwa wanajikomba kwa madaktari na kutaka kudraw public attention?
 
Back
Top Bottom