Adai fidia ya Sh700,000 kwa kunyimwa unyumba

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,320
17,822
Adai fidia ya Sh700,000 kwa kunyimwa unyumba

Glory Kimath

MAHAKAMA ya mwanzo Temeke imeanza kusikiliza kesi ya madai iliyofunguliwa na Juma Ally, ambaye anadai fidia ya Sh700,000 kutokana na mkewe, Fatuma Seleman kumnyima unyumba. Wanandoa hao wamefikishana mahakamani hapo baada ya mke kuchukuliwa na wazazi wake miaka mitatu baada ya kufunga ndoa yao.

Kesi hiyo, inayosikilizwa na hakimu Silvesta Nyanda, ilikuwa kivutio kwa watu wengi ambao juzi walifika kuisikiliza. Wawili hao walianza maisha ya ndoa Januari 28,2006 lakini ndoa yao ikafikia kikomo Machi 30, 2008 wakati Fatuma alipochukuliwa na wazazi wake, mahakama iliambiwa jana.

Mdai kwenye kesi hiyo ya aina yake, Juma aliieleza mahakama hiyo kuwa ameamua kufungua kesi ya madai ya kiasi hicho cha fedha kama fidia ya usumbufu ya kutopata haki yake ya unyumba kwa kipindi cha miaka mitatu. Alisema fidia hiyo pia inajumuisha gharama za mavazi na matunzo mbalimbali aliyokuwa anampa mkewe kwa kipindi hicho chote kabla na baada ya kuchukuliwa na wazazi wake.

“Tangu nimwoe hajawahi kunipa haki yangu ya tendo la ndoa kwa kipindi chote tulichokuwa kama mke na mume na nimemhudumia kwa mambo mengi kwa hiyo nina haki ya kudai fidia kwa sababu sijawahi kumtumia," alisema. Mkewe alikuwepo mahakamani hapo na akakataa kumnyima unyumba mumewe kwa maelezo kuwa aliyeshindwa kutumia haki yake ni Juma mwenyewe.

“Mimi nilikuwa mke wake kwa kipindi chote hicho," alikiri Fatuma. "Niliishi naye kwa uvumilivu tu kwani huyu kijana ana upungufu wa nguvu za kiume... yaani hajiwezi kabisa. Huo ndio ukweli mheshimiwa.

"Nilipochoka kuvumilia wazazi wangu walikuja kunichukua.” Maelezo hayo yaliibuka mjadala mpya baada ya mume huyo kuyapinga, akisema kuwa ni ya uongo kwa kuwa ameshawahi kuwa na mke na amezaa naye. "Ni kweli kwamba hauna nguvu za kiume," Hakimu Nyanda alimuuliza Juma.

“Sio kweli mheshimiwa huyu msichana ananisingizia. Mimi nilishakuwa na mke na tulipata mtoto mmoja wa kike, lakini kwa sasa siko nayee tena,” alijibu.

Alieleza mahakamani hapo kuwa awali alifungua madai ya mahari yake ya Sh50,000 lakini hadi sasa hajalipwa, kitu ambacho aliieleza mahakama kuwa kimechangia kuongezeka kwa kiwango cha madai hayo. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba mosi, siku ambao mdai atatakiwa kuwasilisha uthibitisho kuwa ana nguvu za kiume.

Source: Mwananchi Read News

My Take:

wadau kumbe haya mambo yanaweza kuwa mazito kiasi hiki! walio na ujuzi wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 watualeze isije ikawa wengi wanakufa na tai zao shingoni kumbe haya mambo yanatatulika mahakamani

Sijui jamaa akienda hospitali vipimo gani watachukua kuthibitisha uwezo wake wa nguvu za kiume? LOL
 
Si anadai kuwa na mtoto? na aliwahi kuwa na mke kabla, hao watasaidia katika ushahidi, aidha huko kwa dokta labda ataambiwa apige ngunga...
 
Si anadai kuwa na mtoto? na aliwahi kuwa na mke kabla, hao watasaidia katika ushahidi, aidha huko kwa dokta labda ataambiwa apige ngunga...
..Kupiga ngunga ndio nini, Nyeto??
Lakini na hao wazazi wa huyo mwanamke nao hawana busara pia kwenda kumchukua binti yao toka kwa mumewe sidhani kama ilikuwa sahihi kama binti alikuwa amezidiwa na matatizo katika ndoa yake sana sana angekwenda kwa wazazi wa mume awaeleze kama kweli jamaa mpingo wake choka mbaya wangemshauri ikiwemo kumuuliza mhusika (mume) juu ya madai ya mke. Lakini kwenda tu na kumbeba huyo mwanamke kienyeji hivyo si sawa. Kwa mtazamo wangu jamaa anastahili kulipwa fidia.
 
“Tangu nimwoe hajawahi kunipa haki yangu ya tendo la ndoa kwa kipindi chote tulichokuwa kama mke na mume na nimemhudumia kwa mambo mengi kwa hiyo nina haki ya kudai fidia kwa sababu sijawahi kumtumia,"
Wana Beijing wa JF mpo?,hamjadhalilishwa hapo ina maana nyie ni mnatumiwa tu alafu...............

“Mimi nilikuwa mke wake kwa kipindi chote hicho," alikiri Fatuma. "Niliishi naye kwa uvumilivu tu kwani huyu kijana ana upungufu wa nguvu za kiume... yaani hajiwezi kabisa. Huo ndio ukweli mheshimiwa
Mhh.......
Sijui jamaa akienda hospitali vipimo gani watachukua kuthibitisha uwezo wake wa nguvu za kiume? LOL
Itabidi ajichue(punyeto) kukiwa na mashahidi lakini jogoo anaweza asiwike kwa uwoga wa mahakama u vinginevyo.
 
Hata mimi nimecheka sana kuambiwa kwamba siku hiyo anatakiwa akathibitishe kama kweli ana nguvu za kiume! Ataithibitishi vipi mahakama? Kwa kuonyesha uume wake uliomama mbele ya hakimu au?
 
Jamaa si angeuchomoa tu hadharani huku anapiga puchu...angeshamaliza ubishi..hehe..ingekua mie ningeuchomoa hadharani...ukiwa kama mkuki unasema niombee niombee hehe
 
Hata mimi nimecheka sana kuambiwa kwamba siku hiyo anatakiwa akathibitishe kama kweli ana nguvu za kiume! Ataithibitishi vipi mahakama? Kwa kuonyesha uume wake uliomama mbele ya hakimu au?

ndo hapo mkuu Masaki...unajua vitu vingine vinachekesha sana...lakini nahisi huenda mahakama ikataka uthibitisho wa daktari.....of course wanaweza kumipa hormones na nini lakini sijui.....
 
Itabidi ajichue(punyeto) kukiwa na mashahidi lakini jogoo anaweza asiwike kwa uwoga wa mahakama u vinginevyo.
__________________
YO YO YO WE NI DK nini?????????mimi jogoo lilishawahi kukataa kuwika kipindi fulani mke wangu pombe mtu akirudi hata mb*** inashindw akunyanyuka!!1
 
Hata mimi nimecheka sana kuambiwa kwamba siku hiyo anatakiwa akathibitishe kama kweli ana nguvu za kiume! Ataithibitishi vipi mahakama? Kwa kuonyesha uume wake uliomama mbele ya hakimu au?
Hilo ni tatizo la kiafya,hivyo ripoti ya dokta itatumika baada ya kumfanyia simple physical examination.
 
Hata mimi nimecheka sana kuambiwa kwamba siku hiyo anatakiwa akathibitishe kama kweli ana nguvu za kiume! Ataithibitishi vipi mahakama? Kwa kuonyesha uume wake uliomama mbele ya hakimu au?

Hapa mbona mchezo mdogo sana, wamkubalie huyo mkewe akalale nae siku moja huku wazee wa mahakama wakiwepo chumba cha jirani na asubuhi wakampime mwanamama kama kamwagiwa mbegu.

Kama ikishindikana apelekwe kwenye pornographic movies aangalie mbele ya wazee wa baraza halafu wazee wamcheki je kitu kipo nyuzi tisini?
 
Aaah yaani hiyo mbona ishu ndogo tu........Jamaa analalamika hapewi unyumba, mke analalamika jamaa hapandishi, si wapewe usiku mmoja tu kukiwa na mashahidi. Once and for All, jamaa akishindwa basi halipwi kitu, kikieleweka asubuhi mke arudi nyumbani, kesi imekwisha.
 
kwanza mahakama inaweza ikathibitisha vipi gharama ya hayo madai? kwani unyumba anaonyimwa hiyo ndio thamani yake? Na je ina maana kabla ya kuonana hawakufanya mazoezi na kujua kama jogoo wao wanawika? au waliamua tu kununua mbuzi kwenye gunia. hii ni kichekesho sana.
 
Aaah yaani hiyo mbona ishu ndogo tu........Jamaa analalamika hapewi unyumba, mke analalamika jamaa hapandishi, si wapewe usiku mmoja tu kukiwa na mashahidi. Once and for All, jamaa akishindwa basi halipwi kitu, kikieleweka asubuhi mke arudi nyumbani, kesi imekwisha.

Hufai kabisa kuwa hakimu walahi kwikwii kwichi kwaaaaa!!!!!!!
 
Aaah yaani hiyo mbona ishu ndogo tu........Jamaa analalamika hapewi unyumba, mke analalamika jamaa hapandishi, si wapewe usiku mmoja tu kukiwa na mashahidi. Once and for All, jamaa akishindwa basi halipwi kitu, kikieleweka asubuhi mke arudi nyumbani, kesi imekwisha.
hahahahaha
 
Back
Top Bottom